Nape: Wabunge waache kuisifia na kuipigia makofi serikali sio kazi yao

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,059
Nape alikuwa akijibu maswali mbalimbali aliyokuwa akiulizwa na mojawapo kuhusu bunge amesema bunge mkutano wa wananchi, wabunge wapo pale kwa niaba ya watanzania majimboni na kazi yao ni kuisimamia na kuishauri serikali na sio kuipigia makofi na kuipongeza kila kitu na wakifanya hivyo basi tutapiga hatua
Amesma pia vyombo vya dola visitumie mabavu kwani hii italeta chuki kwa vyombo hivyo na kwa rais na kusema Tanzania hatujazoea mabavu akatolea mfano wa tukio la Malima na kusema yeye alikua akiulizia tu ajabu polisi akamtishia vile
Pia amesema sasa yupo huru zaidi baada ya kuacha uwaziri na anafurahia maisha

 
Yaani nashindwa kabisa kuelewa hawa wabunge pindi wanapo teuliwa kua mawaziri, sijui akili hua zina hamia tumboni....

Onasasa leo huyu Nape anayalamba matapishi yake aiseeeee.....
 
Aiseee kweli MTU ukiwa Na madaraka unakuwa kama kipofu!
Huwezi amini kama ndio nape yule yule aliyekuwa mbogo kwa wenzio wakati wa muswada wa habari

Kuna yule aliyeimba ..............'Umenipa madaraka ya kulevya oh baby.............' Ndiyo watanzania wenzetu wakishapewa Uwaziri wanasahau wametoka kwenye nyumba ya NYASI
 
Nape by Nature ni Mpinzani

Wakat wa Jk japo alikuwa Chamani lakin Moja ya kazi yake ilikuwa kutukana Serikal kwa kusema Mawaziri ni Mizigo lakin Jk akapotezea huu utawala ataujua vizuri kwny Uteuzi wa Mgombea Ubunge 2020, Bunge likiisha aage kwaheri ya kuonana
 
Ukiwa pale juu huwezi jua kama watu wana njaa maana unapata kila kitu kwa kutumia hao watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…