Nape Nnauye, waziri wa habari, michezo na vijana katika kile anachoonekana kuwahasa au kumhasa mtu amejikuta akiandika maneno yenye kufikisha ujumbe mahali fulani.
Kwenye maneno hayo ametumia mfano wa samaki ambaye amefunga mdomo wake kamwe hawezi kunasa kwenye ndoano. Nape anaenda mbali zaidi kwa kuhasa kuwa ni vyema tukafunga midomo pale tunapokuwa katikati ya wabaya.
Hata hivyo Nape Nnauye anasahau kuwa alipokuwa msemaji wa CCM alikuwa akisema "hovyo" mara kwa mara kiasi cha kutoa lugha za maudhi kwa wapinzani wakubwa wa CCM hasa Chadema huku mara kwa mara akilengwa Dr. Slaa ambaye Nape alikuwa akimkejeli kutokana na mambo mbalimbali yaliyokuwa yakimkabili.
"Samaki aliyefunga mdomo wake kamwe hawezi kunasa kwenye ndoano ya mvuvi. Ni vizuri tukafunga midomo yetu pale tunapokuwa katikati ya maadui zetu" -Nape Nnauye.