Nape Nnauye, laana za goli la mkono la 2015 na kusimamishwa kwa matangazo ya moja kwa moja ya bunge zitakuandamana maisha yako yote

Freesoule

JF-Expert Member
Jun 18, 2013
269
272
Wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2015, aliyekuwa katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) wakati huo, Bw Nape Nnauye, alidai kuwa CCM ingeshinda uchaguzi huo hata kama ingekuwa kwa goli la mkono.

Bw Nnauye alikuwa akiufananisha uchaguzi huo na mchezo wa mpira wa miguu. Katika mpira wa miguu, mchezaji anatakiwa kucheza kwa kutumia miguu, labda uwe ni mpira wa kurushwa au mchezaji awe ni mlinda mlango (goal keeper). Katika mazingira mengine yoyote, kamwe mchezaji wa ndani ya uwanja hawezi kufunga goli kwa kutumia mkono na likawa ni goli halali. Bw Nape Nnauye analijua hilo vizuri.

Katika uchaguzi mkuu wa 2015 tulishuhudia udanganyifu katika kuhesabu kura na ujumlishaji wa matokeo. Katika vituo vingi vya kupigia kura matokeo yalionyesha vyama vya upinzani kupitia umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) vilikuwa vimeshinda, lakini tume ya uchaguzi (NEC) ilipokuwa ikitangaza matokeo ya jumla ilionyesha kuwa CCM ndiyo ilishinda. Bila ubadhirifu wa kura wa CCM na NEC, nchi hii isingekuwa inaongozwa na CCM hii leo. CCM walifunga bao la mkono kama Bw Nnauye alivyosema itakuwa.

Kama hilo halikumtosha Bw Nnauye, baada ya kuteuliwa kuwa waziri wa habari alipeleka musawda bungeni kupitia wizara yake kusimamisha matangazo mubashara (ya moja kwa moja aka live) ya bunge, ambayo yalikuwa yakiwapa wananchi nafasi ya kufuatilia uchumi wa nchi yao, hali ya nchi, pamoja na kujua kama wabunge wanayasimamia yale ambayo wananchi wamewatuma kuyasimamia bungeni. Bunge mubashara likasitishwa kwa muswada uliopelekwa bungeni na Bw Nnauye. Cha kushangaza ni kuwa wabunge wa CCM ambao waliupitisha huo muswada kuwa sheria kwa kauli za ndiyo na makofi mengi ya kinafiki, leo hii huwa wanatoa kwenye mitandao ya kijamii 'clip' zao wakiwa wanazungumza bungeni. Kama wanataka kuonekana, kwa nini walikubali kufuta matangazo ya moja kwa moja ya bunge? Unafiki mkubwa. Dhambi ya CCM kwa wananchi kupitia kwa Bw Nnauye.

Sasa Nnauye 'kapigwa benchi' na kocha wake, sijui kocha hakuridhishwa na bao la mkono? Bw Nnauye ametumika na CCM na Bw John Magufuli kama vile mpira wa uzazi (condom) na kutupwa. Lakini laana ya alichokifanya haitaacha kumfuata hata huko jalalani aliko, maadam hatajitokeza kuwaomba msamaha Watanzania na kukiri kuwa alikosea sana. Unafiki wa kujifanya kondoo huko mitandaoni kumbe ni nyoka mwenye sumu hakumuondolei rekodi yake mbaya ya udanganyifu na ushiriki katika sera za ukandamizaji na uminywaji wa uhuru wa mawazo na demokrasia wa Rais mtawala John Magufuli. Watanzania hatutasahau kamwe.
 
Binafsi, namlaumu kwa kauli zake za kejeli. Hebu msikie kwenye ule mkutano wa kampeni (uchaguzi mkuu uliopita) kule Iringa, matusi, kufuru aliyotoa, HUTAMSAMEHE kwa lolote!
Ila, kwenye Bunge live, hayo hayakuwa matakwa yake. Ni matakwa ya yule yule aliyezuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.
 
Binafsi, namlaumu kwa kauli zake za kejeli. Hebu msikie kwenye ule mkutano wa kampeni (uchaguzi mkuu uliopita) kule Iringa, matusi, kufuru aliyotoa, HUTAMSAMEHE kwa lolote!
Ila, kwenye Bunge live, hayo hayakuwa matakwa yake. Ni matakwa ya yule yule aliyezuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa.

Alikuwa waziri, mbona hakujiuzuru kuoneshana hakukubaliana kulihujumu bunge live?
 
Alikuwa waziri, mbona hakujiuzuru kuoneshana hakukubaliana kulihujumu bunge live?
Ndugu yangu weeeee……… mkate wake alikuwa anaupata hapo! Kama ilivyo sasa kwa Polepole na na Katibu wake Mkuu, bila kumsahau Kitilya Mkumbo!
 
Naomba kujinasibu humu kama mtaalam wa karma. Mtu yoyote akitumwa na bosi wake kufanya jambo lolote, mtu huyo anakuwa ametimiza wajibu wake, karma hamhusu, bali ya aliyemtuma ndio itamhusu.

Kwenye bao la mkono, kama Nape alihusika kwenye kupanga, ni kweli karma itamhusu, na mapito ya Nape hapo alipo tayari ni karma tosha.

Kwenye kusitisha matangazo ya Bunge live, mhusika mkuu sio Nape, Nape ni mtekelezaji tuu. Hivyo karma ya dhambi ya Bunge live haimhusu.

Mwisho sio kila jambo lina karma, mambo yenye big karma ni matters of life and death, matangazo live ya Bunge, sio issue ya life and death, hii ni issue ya starehe tuu, leisure and the right to information.

Kwa mfano hata shambulio la Lissu, karma inawahusu waliopanga, na sio waliotekeleza, kama waliotekeleza walipokea amri halali toka kwa boss wao.

P
 
Back
Top Bottom