real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,295
Dodoma. Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amekosoa utaratibu wa kufungia magazeti, akihoji kuadhibiwa chombo kizima badala ya mwandishi aliyeandika.
Nape ambaye aliwahi kuwa waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amehoji ni kwanini daktari anapompasua mgonjwa mguu badala ya kichwa haifungiwi hospitali nzima.
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu nyumbani kwake Kisasa mjini hapa juzi, Nape alisema lengo la sheria mpya ya huduma za vyombo vya habari ya 2016 si kufungia magazeti.
Septemba 29, Serikali ilisitisha uchapishaji na usambazaji wa gazeti la Raia Mwema kwa siku 90 ikisema taarifa yake moja ilijaa nukuu za kutunga zikimsingizia Rais John Magufuli.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyopingwa na baadhi ya wanazuoni na wanahabari, mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo) ambaye ni msemaji mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi alisema agizo hilo linahusu pia toleo la mtandaoni.
Dk Abbasi alisema adhabu hiyo inatokana na toleo namba 529 la Septemba 27 hadi Oktoba 3 lililochapisha habari ya uchambuzi yenye kichwa cha habari “Urais utamshinda John Magufuli”.
Kwa mujibu wa Dk Abbasi, habari hiyo ilisheheni nukuu za uongo, kutungwa na zenye nia mbaya.
Oktoba 24, Serikali ililifunga kwa siku 90 gazeti lingine la Tanzania Daima kwa madai ya kuendelea kuandika habari za uongo na za upotoshaji kinyume cha sheria hiyo.
Katika taarifa yake, Dk Abbasi alisema gazeti hilo katika toleo namba 4706 la Oktoba 22, liliandika habari iliyobeba kichwa cha habari “Asilimia 67 ya Watanzania wanatumia ARVs”.
Taarifa ya Serikali ya kulifungia gazeti hilo iliorodhesha habari nyingine nne ilizosema zilikuwa na makosa na akisema Serikali imejitahidi kuwakumbusha wahusika kuzingatia maadili bila mafanikio.
Alichosema Nape
Nape aliyetimiza umri wa miaka 40 jana, alisema bado anaamini sheria ya huduma za vyombo vya habari aliyoipigania hadi ikatungwa ni bora zaidi.
Alisema sheria hiyo hailengi kufungia magazeti, bali kushughulika na mwanataaluma anayefanya makosa kama zilivyo taaluma nyingine za mawakili, madaktari, wakandarasi na wahasibu.
“Changamoto kubwa iliyopo na ambayo naamini Serikali inaifanyia kazi ni kutoanzishwa kwa zile taasisi za kusimamia vyombo vya habari. Zisipoanzishwa hizi misuguano itaendelea,” alisema Nape.
“Nimekuwa nikiwasikiliza wanahabari, nimekuwa nikisikiliza Serikali mgongano unaotokea na kelele zinazotokea za kufungia magazeti, kutishiana ni kwa sababu hizi taasisi hazijaanzishwa.” Nape alisema sheria imeeleza lianzishwe Baraza Huru la Vyombo vya Habari na limewekewa kazi zake. “Usipokuwa nalo wakati shughuli za habari zinaendelea, nani atashughulikia? Migogoro itabaki. Tumesema iwepo bodi ya Ithibati, isipokuwepo nani anashughulikia?” Alihoji Nape.
Waziri huyo wa zamani alisema sheria hiyo iliyopitishwa na Bunge na kusainiwa na Rais Magufuli ililenga kusaidia kuondoa majukumu makubwa kwenye Serikali kusimamia habari.
“Wabaki (Serikali) na mambo machache ambayo yanalinda nchi yetu. Ndiyo maana kwenye ile sheria yamebaki makosa mawili peke yake ambayo Serikali inatakiwa iingilie,” alisema.
Nape alisema, “Ni public safety (usalama) na uchochezi ambayo ni lazima uyathibitishe pia na tukaweka mle kipengele kwamba mkibishana lazima muende mahakamani. Sheria ililenga kuifanya iwe taaluma.”
Katika kipindi chake cha uwaziri, Nape aliyafungia magazeti ya Mawio na Mseto na redio mbili. Alisema alifanya hivyo kwa kutumia sheria ya zamani na ndio iliyokuwapo.
Aliongeza kuwa ifike mahala sheria itekelezwe kwa kuwa kanuni zipo na taasisi zilizotajwa kwenye sheria zianzishwe. “Zile taasisi zitatuondolea mgogoro kwa sababu Baraza Huru la Habari wanahabari wataitana wenyewe na kuonyana wenyewe kama wanavyofanya madaktari, wanasheria na wanataaluma wengine,” alisema.
Sheria ya Huduma za Habari 2016
Kifungu cha 10(1) cha Sheria ya Huduma za Habari ya 2016, kimeweka sharti la kuanzishwa kwa Bodi ya Ithibati itakayokuwa na wajumbe saba ambapo mwenyekiti atakuwa ni mwandishi mwandamizi. Ukiacha mwenyekiti ambaye atakuwa mwandishi mwandamizi, bodi hiyo itamjumuisha pia mkurugenzi wa Idara ya Habari, katibu wa bodi na mwanasheria kutoka ofisi ya mwanasheria mkuu wa Serikali.
Vifungu vya 23 hadi 31 vya sheria hiyo vimeweka sharti la kuanzishwa kwa Baraza Huru la Habari ambalo majukumu yake ni pamoja na kusikiliza malalamiko dhidi ya vyombo vya habari.
Chanzo: Mwananchi