Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,594
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ameibua mjadala kwenye mtandao wa X baada ya kusema kuwa amefanya kazi makao makuu ya CCM kwa takriban miaka 20, na mtanzania atakayepata takwimu zozote zinazokihusu chama hicho na akazimini atakuwa mtu wa ajabu.
“Mpaka report ikufikie wewe ya CCM bado ukaamini iko hivyohivyo utakuwa wa ajabu sana. CCM haifanyi Kazi hivyo, nimefanya Kazi makao makuu miaka Karibu 20, CCM ni zaidi ya unavyoiona nje” amesema Nape.
Waziri huyu ametoa hoja hii wakati akijibu hoja ya mtumiaji mwingine wa mtandao huo aliyekosoa takwimu alizotoa Septemba 19, 2023 mbele ya Raid wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwanba ni 16% pekee ya Watanzania ndio hutumia mitandao, na kati yao 40% ni diaspora hivyo asiwe na wasiwasi na kelele zao, hivyo atashinda uchaguzi ifikapo mwaka 2025.
“Mheshimiwa umeridhika sana, unatema mambo ya ajabu mtandaoni, now unathibitisha kwamba CCM ni wataalamu wa kudanganya au kupika data, huoni unakipika chama chetu?? Unafeli sana, unajali maslahi yako tu, hujali maslahi mapana ya nchi, ma raia wake. Nyie ndio mnaharibu chama chetu” alisema mchangiaji mmoja akikosoa hoja hii ya Nape.
“Hatupiki lakini ikikufikia wewe document Kama hiyo lazima iwe fake” alijibu Nape.