Napata wapi mbwa wenye mikia mifupi

jiwekuu770

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
2,246
1,643
Kwa Mara ya kwanza Nawaona hawa viumbe !! Mbwa wenye mkia kama Mbuzi ilikua ni miaka ya 2009 mkoani Iringa nilipokwenda kuzuru!!Na ilikua n Mara yangu ya kwanza kwan kabla ya hapo nilikua nawaona kwenye movie tu...Sio siri hawa mbwa n wakali sijapata ona utadhan wanakichaa!!
Toka hapo nimekua nikijaribu kuwatafuta sijapata kuwaona .....
Ningependa kujua naweza wapata wapi
Wanauzwa shilingi ngapi!?
Wanaitwaje?
Na data zingine kuwahusu






NAWAKILISHA
 
Mkuu hapa home nina msumeno wa kukatia penbe za ng'ombe so chagua tu mbwa wa rangi uipendayo halafu umlete unipe na kigezo cha ufupi wa mkia u aouhitaji hata kama ni kukata wote nitakukatia ili moyo wako uwe na amani
 
Si urudi iringa ulikowaona mara ya kwanza?
Yaan mkuu ilikua kama nimeonana nao accidentally jamaa alikua anapita nao kipindi hicho cha kuchoma sindano za kichaa...usipochoma mbwa wanapigwa risasi....so sina hata idea wap Huyo jamaa alko
 
Hao wanaitwa rottweiller asili yao ni ujerumani. Ni security dog na ni wakali sana kama una watoto nyumbani ni hatari pia maana hana tofauti sana na american pitbull. Kukata mkia siku hizi imekuwa ni optional maana wataalamu wa mbwa wamefanya utafiti na kugundua kuwa kumkata mbwa mkia unampunguzia balance hasa anapokuwa anafanya shambulio au kupigana. Bei za hao mbwa kwa hapa Dar haipungui milioni moja na nusu kwa kinda la miezi mitatu. Kwa maelezo zaidi soma hapa Rottweiler - Wikipedia
 
Hakuna breed ya mbwa wenye mikia mifupi (kama hizo picha) kilichotokea ni kwamba hao uliowaona pamoja na picha ulizipost, walikatwa mkia wakiwa wadogo kwa imani kwamba mbwa akiwa hana mkia anakua jasiri na mkali kwa kuwa inaaminika uoga wa mbwa upo mkiani mwake!
 
Basi mi nikajua ndo breed ya aina yake ...kumbe wanakatwa daahh!!
 
Yaan hawa mbwa bei ni kubwa kuliko hata ya ng'ombe!!!... Lakin naamini hapa Tanzania wapo kwa baadhi ya watu!!..na sidhani kama itakua sawa na hyo bei ya nje
 
Hao sio Rotties boss, hao ni Doberman
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…