Napata maumivu upande wa kushoto wa kifua

Abbas jr

New Member
Jul 29, 2018
3
1
Napata maumivu upande wa kushoto wa kifua (moyo) lalkini yanakuwa ya aina ya kichomi sasa natak kujua yanasabibishwa na nn na linaweza kuwa ni tatizo kubwa??
 
Mara nyingi linakuwa tatizo la kurithi, lakini hii pia husababishwa na vitu kama vile; I) kutokufanya mazoezi ii) aina ya vyakuka unavyokula kutokana mahitaji ya mwili ,,, mfano mwili unahitaji kiwango Fulani cha sukari na mafuta, lakini vikizidi au kupungua sana husababisha matatizo ya moyo, iii) mikao isiyostahili kwa mfano kuegemea upande mmoja wa mwili kwa muda mrefu na kutokubadilisha mtindo au namna ya ulalaji.
 
Ili kuondoka na tatizo hilo ni muhimu kumuona daktari kwa ushauri na uchunguzi zaidi wa kimatibabu. Hii ni kwa sababu ni vigumu kufahamu kiwango cha tatizo kwa wakati husika hivyo inashauriwa kumuona daktari mapema kadri inavyowezekana.....hata hivyo inashauriwa kufanya mazoezi kila Siku kwa dakika zisizopungua 30 kila siku kama vile kukimbie, kupiga push ups, kutembea haraka haraka au mazoezi mengine yoyote unayoyafahamu, pia ni muhimu kupendelea kula mboga mboga na matunda kwa wingi ili kuweza kurahisisha msawazo wa chakula kwenye mwili.
 
Napata maumivu upande wa kushoto wa kifua (moyo) lalkini yanakuwa ya aina ya kichomi sasa natak kujua yanasabibishwa na nn na linaweza kuwa ni tatizo kubwa??
Hayo maumivu yanaenda sehemu nyingine kama kwenye taya,Shigo au mkono wa kushoto au nyuma ya mgongo?
Unayapata ukiwa unafanya kazi au hata ukiwa umepumzika?

Mara nyingi maumivu ya hivi yanaletwa na Moyo kukosa Oxygen ya kutosha either kwa sababu mirija inayo supply kwenye moyo imeziba au tu basi moyo unaenda mbio wakati mwili wako hauwezi supply kiwango cha Oxygen kinachoendana na matumizi ya moyo!

Hii ni hatari sana iwapo mshipa huo umeziba maana inaweza kupelekea moyo kuharibika kabisa i.e Myocardial Infaction.

Nakushauri uende hospitali ya Mkoa ukafanye kipimo cha ECG na kama itapendeza watakufanyia vipimo vingine vya damu kama Troponin levels.
 
Sawa ntafanya hvyo nashukuru
 
Mara nyingi linakuwa tatizo la kurithi, lakini hii pia husababishwa na vitu kama vile; I) kutokufanya mazoezi ii) aina ya vyakuka unavyokula kutokana mahitaji ya mwili ,,, mfano mwili unahitaji kiwango Fulani cha sukari na mafuta, lakini vikizidi au kupungua sana husababisha matatizo ya moyo, iii) mikao isiyostahili kwa mfano kuegemea upande mmoja wa mwili kwa muda mrefu na kutokubadilisha mtindo au namna ya ulalaji.

Lakin huwaga yanakuja kwa kipndi tu cyackii kila siku hili unalionaje?
 
Back
Top Bottom