Naona la tukio la Ali Kibao limeshatusahaulisha ghafla sakata la binti wa Yombo aliyeingiliwa kote kote na waliotumwa na Afande

Na hapa ndiyo utajua kuwa Watanzania hatujui tunataka nini na huenda Watawala wameshatujua Udhaifu wetu na wala hawana kabisa wasiwasi na Sisi huku wakitufanyia wanachokitaka pale wanapojisikia.
Wako watu wengi na hususani Watoto wakifanyiwa unyama ila hakuna kelele kisa sio Wanasiasa na hawana wa kuwasemea.

Kwangu Mimi Wanasiasa wakitoana korodani Wala sishituki sana sana Waendelee maana siwataki kabisa
 
Wafata upepo,..leo wataongea hili, kesho lile,..

Vichwa vidogo,watu walikaa week nzima kujadili makonda yuko wapi,.

Hawajachagua kusimamia kimoja,katiba,muungano,utekaji,tume huru,vita ya ufisadi, ajira or nepotism

Walalamishi ambao hawajawahi kuthubutu kuchukua hatua..

Wananchi wanacheza muda gani???
 
Na hapa ndiyo utajua kuwa Watanzania hatujui tunataka nini na huenda Watawala wameshatujua Udhaifu wetu na wala hawana kabisa wasiwasi na Sisi huku wakitufanyia wanachokitaka pale wanapojisikia.

Yote ni muhimu lakini la Kibao ni la dharura zaidi.

Kuna kina Soka, na wengine wanaweza kuwa wangali hai nasi tunaweza tukajinusuru na kuendelea kuwa hai.

Kushughilika na Kibao sasa kutaokoa maisha mengi yaliyoko hatarini yakiwamo yako mleta mada na hata huyo binti.

Yote mengine yakiwamo ya binti wa yombo yanaweza kupiganiwa na watu walio hai na yeye akiwa hai.

Hadi hapo, kwa hakika: "uzwazwa ni kutoliweka la Kibao kipaumbele."
 
Na hapa ndiyo utajua kuwa Watanzania hatujui tunataka nini na huenda Watawala wameshatujua Udhaifu wetu na wala hawana kabisa wasiwasi na Sisi huku wakitufanyia wanachokitaka pale wanapojisikia.
Ni kama tukio la mulamula kutenguliwa mambo ya nje na kijana majaliwa precision air ilivyotusahaulisha kugongewa na Masanja. Yani Matukio hayo yalimsaidia sana Masanja bila kutarajia.
 
Back
Top Bottom