kwisha
JF-Expert Member
- Sep 9, 2021
- 1,739
- 4,729
Mwaka 2014 baba yangu na mama yangu waliachana tena kwa talaka baba akaenda kuoa mwanamke mwingine uko
Mama tukabaki naye nyumbani akabaki analea watoto wake kwenye familia yetu tuko watoto 8 wa kiume 6 wakike 2 sasa mama alioana akiolewa na watoto hao hakuna mwanaume ambaye anaweza kuvumilia au kulea watoto ambao sio wake tena wakiume. Tuliishi na mama yetu kwa bahati nzuri tulifanikiwa kununua nyumba yetu. Tukawa tunaishi wote
Sasa kule ambako baba alikuwa anaishi na yule mwanamke sio kwamba alikuwa ameoa ndoa huyo mwanamke alikuwa anaishi naye tu ivo kama wachumba tena alikuwa anaishi nyumbani kwa huyo mwanamke
Alimfukuza sasa baba yangu hana sehemu nyingine ya kwenda amekuwa kama homeless jana alikuja kulala hapa nyumbani nilimuingiza ndani ya Nyumba bila Mama kujua kimbelembele chake kikampoza asubuhi si alikwenda kumsalimia mama yangu chumbani kwake
Mama alivyojua tu amelala hapa alianza kufoka na kuniambia kuwa hatiki kumuona nyumbani hapa na kuanza kusimulia mengi kuwa alimtelekeza na watoto yaani mengi ya ndani ambayo sisi watoto tulikuwa hatujui ameyasema mpaka nikashindwa kuamua nifanye kama mtoto mkubwa na kibaya zaidi amerudi akiwa Mgonjwa
Sisi kama watoto tumejaribu kuomba msamaha Mama amekataa kabisa wanafamilia nao wamekataa kumsaidia kuwa walimshauri kipindi cha nyuma saana lakini hakutaka kusikia familia eti avune alicho kipanda
Yaani ningekuwa na uwezo ningelimchukulia nyumba ya kupanga uwezo zina sasa
Naombeni msaada wenu wa ushauri maana haya mambo mimi naona yako juu kabisa ya akili yangu na kibaya zaidi sio kwamba tuko Afrika tupo katika Nchi za wenzetu