Naombeni msaada Wa kisheria mwajiri ananionea

MKONGORO

JF-Expert Member
Jun 15, 2014
338
300
Wakuu habarini za majukumu,

Naombeni msaada Wa kisheria ili mwajiri huyu anilipe mshahara wangu alio uzuia ili familia yangu iweze kuishi.

Wakuu mwajiri huyu amevizia Mpaka siku 2 kabla ya Siku ya kunilipa mshahara wangu wa mwezi akaamua anisingizie kesi ya wizi lengo anidhulumu mshahara wangu niliovujia jasho mwezi mzima.

Amefanikiwa kunitupa polisi kwa nguvu ya pesa aliyo nayo hatimae mahakama ya mwanzo lakini Mungu mkubwa mahakama imetenda haki nipo nje kwa dhamana.

Wakuu naombeni msaada wa kisheria ili mwajiri huyu anilipe mshahara wangu aliozuia kunipa ili familia yangu iweze kuishi wakati Mimi naendelea na kesi yake ambayo haihusiani na mshahara wangu niliouvujia jasho mwezi mzima.

Pia mwajiri huyu ametamba kuwa siku nikienda ofisini kwake kudai mshahara ataniitia polisi na hata nikienda Polisi siwezi kupata msaada wowote kwani wakuu wa vituo vya polisi vilivyo karibu in rafiki zake.

Wakuu mimi sina msaada zaidi ya kukimbilia kwenu kuomba msaada Asanteni 0765544791

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umefanya kazi kwa muda gani hapo? Mshaara ni wa huo mwezi mmoja tu au kuna endelevu? Mlikua na makubaliano gani mliandikishana au mlikubaliana tu kwa maneno? Ulitakiwa ufanye kazi lini mpaka lini?


Wakili.
 
Mkuu samahani Kwa kuchelewa kujibu nimefanya Nazi kwa muda wa miezi 13 na mkataba ilikuwa ufike ukomo wake tar 7/6/2020 baada ya mkataba kila mmoja angekuwa huru kuendelea au la asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakili naomba msaada, Nikweli mwajiri anaweza kusitisha huduma za matibabu yani (Medical Insurance) zilizo kwenye makubaliano ya kimukataba..!!? Pasipo kukupa taarifa zozote juu ya hilo nanukimuuliza anakwambia ameshindwa kukuhudumia kwa sababu za kiuchumi, naomba kuelewa hapa.

Maana Mimi mwajiri kasitisha huduma hii na nimemuandikia demand notice anilipe fidia ya M 200/ kwa kunisababishia usumbufu Mimi na familia yangu.
 
Back
Top Bottom