Naombeni mchanganuo wa gharama na idadi ya materials ya kujenga fensi ya ukuta 20m x 20m

Hapo perimeter =80m bila hilo geti. Kwamba umezungusha eneo lote.
Roughly 1m =2 tofali.
So kozi moja ni tofali 160
Piga kozi 8. 160 x 8 =1280 tofali.

Cement = 1280/70 = 18.28 bags...so tufanye ujiandae na mifuko 20 ya cement.
 
Hapo perimeter =80m bila hilo geti. Kwamba umezungusha eneo lote.
Roughly 1m =2 tofali.
So kozi moja ni tofali 160
Piga kozi 8. 160 x 8 =1280 tofali.

Cement = 1280/70 = 18.28 bags...so tufanye ujiandae na mifuko 20 ya cement.
Naomba ufafanuzi kuhusu hii estimate:

Roughly 1m = 2 tofali

Tofali 2 zinajenga 1 m ?
 
Tofali moja ni wastani wa ~50cm,tofali 2 ndio wastani 1m na kuchapia
Kwa cement ya gauge 32,tofali 50 = mfuko 1
Kwa cement ya gauge 42 tofali 60-70 = mfuko 1,
Lenta ya chini kwenye udongo(cement + mchanga+kokoto)
Mawe + cement
Zege/mkanda wa juu yake(cement + mchanga + kokoto + nylon +/-)
Eneo lako ni 20×4=80m-3m =77m,
Nguzo 2 za kushikilia geti + nguzo za ku support ukuta kila 4m = nguzo 18(tofali 2,2 unaziweka kwa kizikatisha)
Utaweka kozi 8 na kofia(kuepusha ukuta kuchafuka na michirizi ya maji - hii sio lazima).

Assume eneo lako ni tambarare kabisa

Idadi ya tofali piga hivi; Kozi 8 x (72×2) + (18x2x8) =1440 + 10 za kuvunjika vunjika = 1450
Cement piga hivi; (1440/50)gauge 32 = 29 fanya ~ 30bags na kwa gauge 42 fanya 1440/65 = ~22bags
Cement ya nguzo za geti 6bags
Cement ya zege la chini 20bags =(4mtrs/1bag)
Cement ya mkanda/zege la juu 20bags =(4mtrs/1bag)
Nondo za nguzo za geti 2 za Y'12(nondo 1 ni 40ft)
Mchanga na kokoto ka jiongeze kwa ratio fundi atakayokushauri kutokana na quality ya mchanga na size ya kokoto

Natumai umepata ka mwanga kidogo

Napendekeza uchore sketch yenye maelezo hayo hapo juu
Alafu ndipo
Uulize ambapo hujaelewa kweli kweli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom