Right Way In Light
JF-Expert Member
- Jul 27, 2024
- 1,322
- 3,416
Wakuu heshima kwenu.
Polen na hongereni kwa majukumu yenu ya kila siku.
Niko kwenye hali fulani ya mkanganyiko kidogo. Nasema kidogo kwasababu ni kama niko njia panda japo kuna njia ambayo kwa mujibu wa misingi ya imani na utamaduni na maadili yangu najua nitaiendea njia hiyo japo naona ni ngumu sana ndio lengo la kusogea kwenu nipate mawili matatu.
Mimi ni mwanaume. Umri wangu ni 35 years. Nina mke yeye ni 36 years na Mungu katubariki kuwa na watoto wa 4 mpaka sasa hivi katika kipindi chote cha miaka 14 toka tujuane na mpaka kufunga ndoa. Tuna miaka 10 toka siku tufunge ndoa rasmi.
Mwanangu wa kwanza ana 13years yuko form 1, wapil yuko class 3, wa 3 yuko class 1 na wa 4 ana mwaka mmoja na miez kama 9 sasa. Katika hawa woote watoto wanne, ni mmoja tu wa kiume wa tatu kuzaliwa alieko clasa 1.
Sasa hapa juz kati tumekuja kufaham kuwa wife kanasa mimba tena. Ni baada mwezi kupita bila kuona kawaida ya kike ya kila mwezi na tukaamua kufanya vipimo tukagundua imoo.
Shida sio mtoto, shida ni mipango. Sikua na mpango wa kuzaa baada ya kufunga miaka 35 ya umri.
Hii imenifanya kuwa na reaction tofaut katika mapokeo ya taarifa ya ugen huu.
Na suala hil hata kwa wife pia lilimtoa machozi. Kiukwel hii taarifa ilitupa shock na imezua mgogoro mkubwa na wife, amenishushia lawama sana hasa kwakua nilipopata majibu haya sikuchukua hatua ya kum comfort. Nafikir ni kwakua hata mimi ilinichanganya. Amekua akinishutumu sana japo najua hii yote yaweza kuwa ni shock ya tukio ambalo hakuna aliyetegemea.
Kwa imani yangu, nimekua nikimuomba Mungu anipe amani na uamuzi sahihi na pia utayari wa kupokea suala hilibkwa mikono miwili. Anisaidie kusiwe na athari yoyote kiroho kwa mtoto kwa jiona kama hatuko tayari kumpokea. Namuomba sana Mungu anisaidie na aingilie kati, pia amsaidie wife aweze kukubaliana na hili, naelewa sana jinsi ambavyo inam frustrate pengine kila anapofikiri kuanza safar ndefu ya miezi 9 yenye kila aina ya vikwazo kiafya na kihisia.
Naelewa ni namna gani huwa inatu consume kusubiri mtoto kuzaliwa na majibu ya maombi yetu kuwa mtoto azaliwe salama mwenye afya njema bila kasoro. Haya yote tunayajua kwa watoto hawa wa 4 tuliojaaliwa.
Sasa sisi tukawa tunahesabu mambo haya tumekwisha yamaliza na hatuta rudi tena huko zaid ya kukaa na kulea watoto na kuwaandalia future yao.
Wakuu nachanganyikiwa japo nimeanza kukubaliana na hili.
Naomba ushauri wenu na kutiwa moyo.
Nafikiri baada ya hili kupita kama Mungu akitujaalia kumaliza mwendo salama, mmoja wetu atapaswa kufunga uzazi, hakuna namna.
Ahsanten na karibun kwa ushauri.
Siku njema