Naomba ushauri wa Kisheria

Crimea Bridge

Member
Oct 8, 2022
51
152
Habarini ndugu, naomba kupewa ushauri wa kisheria.. nilikopa kwenye bank fulani ya kigeni hela nyingi nikashindwa kurejesha. Bank hiyo walinifungulia mashtaka na sasa hukumu imetoka natakiwa kulipa deni hilo na hukumu imewapa wanaonidai interest ya 9% kwa mwaka mpaka nitakapomaliza kulipa mkopo..

Swali langu; Je, nini kitatokea nisipolipa deni hilo? Nitakamatwa kwenda jela au? Na je nikikamatwa nini itakuwa hatima yangu. Kwa sasa hvi mimi sina uwezo kabisa wa kulipa hata kidogo kidogo, deni lenyewe ni kubwa sana ..

NB: Mkopo huo ulikuwa na dhamana lakini dhamana yake ilipata changamoto kutokana na ugomvi wa kifamilia hvyo kwa sasa mkopo huo hauna dhamana. Maana mahakama iliiondoa dhamana hiyo kwenye mali zinazotakiwa kuuzwa ili kurejesha deni.

Ila hukumu imetoka kwamba mimi niliyekopa ndio nilipe deni hilo..

Naomba ushauri wenu wa kitaalamu.

Asanteni
 
Pole Mkuu
Itakubidi ulipe deni lao lakini ikitokea umeshindwa kulipa kwa wakati utafungwa then ukitoka itakupasa ulipe deni
 
Pole Mkuu
Itakubidi ulipe deni lao lakini ikitokea umeshindwa kulipa kwa wakati utafungwa then ukitoka itakupasa ulipe deni

Huwa kuna muda maalumu wa kulipa? Kwenye hukumu haijaelezwa muda maalum.. wao wameweka interest tu ya 9% kwa mwaka mpaka deni likiisha
 
Pole Mkuu
Itakubidi ulipe deni lao lakini ikitokea umeshindwa kulipa kwa wakati utafungwa then ukitoka itakupasa ulipe deni
Ukifungwa, gharama zote za kule jela atagharamia yeye aliyekufunga kumbuka kule utakula tofaut na wafungwa wengine utakunywa tofaut na wafungwa wengine,
Ila hizo gharama za kukuhudumia wewe zinaenda kuongezeka kwenye lile deni unalodaiwa..na kama atashindwa kulipa gharama za kukuhudumia ukiwa gerezani, alishindwa kupeleka hiyo pesa hata kwa siku 1, unaachiwa Toka gerezani.

Mimi sio mwanasheria, ila nilifatilia ITV kipind cha mahakama, ndo walikuwa wanaelezea case za madai zinavyoenda.
 
Asante kwa mchango wako..
 
Pole Mkuu
Itakubidi ulipe deni lao lakini ikitokea umeshindwa kulipa kwa wakati utafungwa then ukitoka itakupasa ulipe deni
Huyu si wakupewa pole alijua anafanya utapeli mfano amesema aliweka mali ya familia kama dhamana. Hivi alikuwa hajui kama ile mali ya familia haiwezi kuwekwa dhamana?.
Nikijibu kwa mkopaji(mtaka ushauri) kisheria mahakama inatakiwa itowe hukumu ya wewe kulipa deni lako. Pia kama kuna mali zako zipigwe mnada kama una kazi utakatwa asilimia hakimu atakayo isema. Ikishindikana yote hayo utakwenda keko ukale Kifir….o.🤣
 
Huwa kuna muda maalumu wa kulipa? Kwenye hukumu haijaelezwa muda maalum.. wao wameweka interest tu ya 9% kwa mwaka mpaka deni likiisha
Mmmh inawezekana ujasikiliza au ujasoma vizuri maana uwezi kuwa na interest kama muda aupo maana interest inatokana na muda husika Mkuu iyo rate ya 9 ukija kuchunguza utakuta kunamuda wake waliuweka
Pia ukifungwa baada ya kutoka aitachukuwa week inabid ulipe pesa Yao tena mbeye ya hakimu mkazi Yani mahakamani kwaiyo baada ya ww kufungwa hao jamaa awawez kukufwata ww direct inabid watumie mahakama kukudai apo ndio moto upo maana unaweza kupewa kesi Zaid ya Moja ambazo zitakughalimu maisha yako
Pole sana Mkuu
 
Back
Top Bottom