y
Mkuu
Eiyer kesho imefika tunakusubiria au hakujawa majaliwa?
Well...
Nilikuwa nimebanwa kiaina wakuu...
Iko namna hii,kwa namna nijuavyo na kwa mujibu wa utafiti ambao nimeufanya na ninaoendelea kuufanya kuhusu chapa ya mnyama na hii microchip ni kwamba mambo haya yanaweza kuhusiana lakini hayafanani au kwa lugha nyingine microchip siyo ile chapa iliyoandikwa kwenye ufunuo 13 ambayo ni 666 kwasababu zifuatazo...
1;Huwezi kuwa na chapa hii bila ya kuwa na mhusika ambaye ni mnyama [ufalme/mfalme] hivyo dhana kuwa microchip iliyopo ambayo watu wanawekewa kuwa ni hiyo chapa siyo sahihi maana maandiko yanazungumza vizuri tu namna itakavyokuwa....
2;Chapa iliyoandiokwa kwenye Ufunuo 13 siyo kifaa bali ni hesabu ya jina,tunachopaswa kujua ni kwamba hapo inazungumzwa habari ya jina na hesabu ya jina lake siyo kifaa chochote.Watu,kwa maana ya maandiko matakatifu ya Ufunuo 13:16-18 watapigwa chapa kwenye mapaji ya uso na kwenye mikono yao ya kuume na kuwatambulisha kuwa wao wamekubaliana na kile ambacho mnyama wa pili [Ufunuo 13:11-15] anakifanya kwa niaba ya mnyama wa kwanza [Ufunuo 13:1] kwa maana hiyo hapa tutakuwa na wanyama wawili lakini jina ambalo chapa yake ni 666 ni la mnyama wa kwanza,huyu wa pili atakuja kufanikisha upigwaji wa chapa hii.....
Kwa maana hii hutaweza kuona chapa hii yenye hesabu ya jina la mnyama kabla hujamjua mnyama mwenyewe.Mnyama anayezungumzwa hapo kwenye Ufuno 13:1-3 sijamuona na kwa maoni yangu bado hajakuwepo duniani,sasa utakuwaje na chapa kabla ya mhusika kuwepo?
Maandiko yanasema kuwa mnyama huyo atakuja kwanza kisha atakuja mwingine ambaye atafanikisha hilo zoezi,sasa yote haya yametokea wapi?
Inawezekana hii microchip ni aina ya maandalizi ya chapa hiyo kwa namna moja au nyingine lakini bado hatuwezi kusema hiyo ndiyo chapa yenyewe.Pia,inawezekana kifaa hiki kikaja kusaidia upigwaji wa chapa hii lakini kwa sasa hatuwezi kusema chenyewe ndiyo 666....
ONYO: Usikurupuke kukubali kitu usichojua malengo yake hasa kwa dunia hii ya sasa,tumia muda wako kufanya utafiti kabla hujakubali maana unaweza kujikuta kwenye wakati mbaya sana hapo baadaye....
Ahsanteni....