Naomba uelewa wa hili juu ya kadi nyekundu kwa Makocha

ikiumasema

JF-Expert Member
Oct 9, 2015
923
1,299
Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa Ligi kuu ya Tanzania na pia Ligi pendwa duniani yaan Epl....Ila Kuna utofauti wa sheria za pale England na hapa Tanzania hasa pale makocha wanapopewa kadi nyekundu....

Mwanzoni kabisa mwa msimu wa Ligi kuu nilishuhudia Antonio Conte na Thomas Tuchel wakipewa red card baada ya mchezo kumalizika pale Stamford bridge lakini walirejea Tena kwenye touchline match zilizofuata.

Juzi hapa J.Klop alipewa red card.....na FA ya wamemcharge kwa makosa yake leo ktk taarifa yao rasmi na pia wamemruhusu aendelee kukaa benchi mechi inayofuata.


Hapa Tanzania ipoje?

Makocha wanapopewa red card wao hikosa michezo mitatu Kama wachezaji mifano ipo ya Naserdine Nabi alipewa kadi nyekundu akafungiwa michezo mitatu na faini.

Je hii imekaaje?

Sheria Ina tija?
Au ibadilishwe ifuatwe ya Uingereza?
 
Eleza hapo ' wamemcharge' Kwa makosa yake
Wamepmpa adhabu ya kulipa faini pamoja na kumpa onyo Kali.....pia klop ktk conference yake alikiri kosa pamoja na kuomba radhi kwa namna ambavyo alikosea.....Ila makocha kupewa adhabu sawa na wachezaji ni sahihi?....na klop atakaa benchi kwenye mchezo unaofuata
 
Namna ya kutumikia adhabu ya Red card ni kanuni inayowekwa na FA husika. Wengine wanaweza kuchagua mechi za kutumikia, wengine una simamishwa mechi zote zinazo fuatia.
 
Huwa wanakata rufaa, ya conte ilikubaliwa lakini tuchel mechi 1 alifuatilia akiwa jukwaani
 
Kwanza HAKUNA anapewa kadi Bali ni kuoneshwa. Kiongozi yeyote wa benchi la ufundi anaeoneshwa Kadi nyekundu hutumikia adhabu ya mechi moja tu unless unless kosa Liwe kubwa sana...
 
Klop atakosa mechi moja.... kwahiyo hata Kama ukimuona yupo mechi inayo fata na West ham basi baada ya hiyo hutamuona mechi na Notingam forest.... utaratibu ni mechi moja Kwa makocha
 
Back
Top Bottom