Naomba tufahamishane bei za mpunga maeneo mbalimbali.

Ramea

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,146
4,083
Kwa wale wafanyabiashara wa mazao hasa mpunga, naomba tujuzane bei ya mpunga ili tunaopenda kusteki nafaka tujipange kisaikolojia.

Huku niliko, pwani ya kusini Lindi, Mtwra na Tunduru(Ruvuma) bei ni kati ya 8,500/- hadi 12,000/- kwa debe.

Vipi Kilombero, Kyela na kwingineko bei zikoje?
 
Huko kilombero gunia elfu 70
Gunia la debe sita au saba?
Mana huku kwetu twatumia kipimo cha debe then tunahifadhi kwenye maroba ya debe 6-10 hatutumii sana kipimo cha magunia.
Asante Mkuu kwa mchango.
 
Kwa bei hizi tunazoziona hapo juu kwa debe zaweza kupanda au kushuka maana nasikia morogoro mavuno bado vizuri
 
Kwa bei hizi tunazoziona hapo juu kwa debe zaweza kupanda au kushuka maana nasikia morogoro mavuno bado vizuri
Tuwasubiri wa Morogoro watujuze. Maana Morogoro ndo inaathiri bei ya mpunga kwa asilimia kubwa nchini.
 
Madibila Iringa gunia la debe 10 bado bei juu.. 100,000 - 120,000
 
Debe ndio kipimo gani, na debe ni la aina gani na kutoka wapi, ni vizuri tutumie Vipimo ambavyo ni std tuambiane gunia la kilo mia ni bei gani, huku Rukwa ni kati ya 60,000 na 70,000/= gunia la kilo 90
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…