Naomba mwenye link ya kitabu cha Rosa mistika anisaidie

Rosa Mistika

Sura ya kwanza.

Huko kisiwa cha Ukerewe kulikuwa na mwanamke mmoja aliyeitwa Regina. Regina na jamaa yake waliishi pamoja katika kijiji cha Namagondo. Regina alikuwa mzuri sana lakini alikuwa na mume aliyemtesa. Regina alikuwa na binti watano; Rosa Mistika, Flora, Honorata, Stella, na Sperantia. Mume wa Regina aliitwa Zakaria na alitaka sana kupata mtoto wa kiume. Regina alikuwa na mimba sasa na alimwomba Mungu ampe mtoto wa kiume.

Usiku mmoja, Regina alikuwa akila chakula cha jioni pamoja na watoto wake. Alizungumza nao juu ya mambo ya malezi. Baadaye walikwenda kulala. Wakati huo huo, Zakaria alikuwa akirudi kutoka mahali pa kunywa pombe. Alilewa sana na alimwambia Regina kwamba alitaka kuwaona watoto wake. Watoto waliitwa isipokuwa Rosa kwa sababu Rosa alikuwa ameanza kuwa mtu mzima. Zakaria aliwaambia waimbe na kufanya mazoezi ya kijeshi. Mara Stella alimwambia baba yake kwamba Rosa alipokea barua pamoja na pesa. Zakaria alikasirika. Hakutaka binti zake watembee na mvulana ye yote. Rosa aliitwa na Zakaria na aliulizwa juu ya barua hiyo.

Rosa hakumtaka babake asome barua yake. Alijaribu kuila, lakini Zakaria alimshika Rosa shingo. Zakaria aliipata barua, akaisoma. Barua ilizungumzia mapenzi na Zakaria alikasirika zaidi. Alikwenda pamoja na Rosa nyumbani kwa mvulana aliyemwandikia Rosa barua. Mvulana huyo, aliitwa Charles. Zakaria alimtupia Charles shilingi, akamwambia kwamba hakutaka kumwona tena pamoja na binti yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…