Naomba msaada ya tafsiri ya hili jambo kwa wataalamu wa mambo ya kiroho

vanus

JF-Expert Member
May 27, 2017
1,151
2,886
Wakuu kwema?

Kuna kijana mmoja alinisimulia kitu cha ajabu ambacho kwangu mm imekuwa ni ngumu kutafsiri kwa haraka nini maana ya hilo jambo/tukio.

Naomba kuwasilisha jambo hili kwenu wakuu mnitafsirie jili jambo kwa weledi wa juu.

Kijana anasema mama yake mzazi aliwahi kumueleza jambo la kustaajabisha ambalo lilitokea kipindi mama mzazi ana mimba ya huyu kijana.

Anasema ilikuwa ni jumapili majira ya jioni na mvua kwa mbali, mama mzazi alkuwa amekaa kwenye kochi huku akijiliwaza, katika kupepesa macho juu aliona nyoka mkubwa sana mwenye rangi nyekundu juu ya paa la nyumba.

Mama mzazi alishtuka sana, akaamua kutoka nje kutafuta msaada kwa majirani ili wamuue yule nyoka.

Alifanikiwa kupata jirani wa karibu ambae alikuja kwa ajili ya kutoa msaada kwa maana nyoka alikuwa mkubwa sana na wakutisha.

Baada ya kurudi ndani na kuangalia juu ya paa la nyumba hawakumuona tena yule nyoka, yule jirani akashauri watoboe ukuta kwa nje ili kama huyo nyoka amejificha ndani apate sehemu ya kutokea.

Walifanikiwa kutoboa ukuta kwa nje, na kwa bahati nzuri mpaka hiyo jioni mume wa huyo mama alikuwa amerudi, hivyo mama akawa na tumaini japokuwa hawajajua hatima ya huyo kiumbe maana hakuonekana tena kwa siku hiyo.

Siku inayofuata ya jumatatu, familia iliendelea na shughuli za kawaida wakapika chakula cha mchana na kuendelea kula, ghafla tena yule nyoka akaonekana anatembea kwenye ukuta ndo hapo yule mume mtu akamuona live na kuchanganyikiwa kwa ukubwa wa yule nyoka.

Wakachukua kitu kama fimbo kubwa na kutaka kumshambulia, ghafla akapotea na hakuonekana tena siku nzima.

Kwa ufupi huyo nyoka aliwasumbua sana kwa kipindi kama cha siku 3-4 bila ya kuwa na mafanikio ya kumuua au kumfukuza ndani ya nyumba, cha kushangaza hakuwahi kujaribu kumdhuru mtu yoyote hapo ndani na ukitaka kumpiga anapotea ghafla.

Sasa baada ya hizo siku 3–4 yule mama akashikwa na uchungu, mume akamuwaisha hospitali kwa ajili ya taratibu za kujifungua.

Baada ya kujifungua na kurudi nyumbani, walikaa siku nzima bila ya kumuona yule nyoka, wakafikiri labda watamuona kesho yake maana ilishakuwa tayari kama kitu cha kawaida kwao kwa hizo siku chache.

Lakini yule nyoka hakuwahi kuonekana tena mpaka leo hii.

Ombi langu ni kwa wataalamu wa haya mambo na maswala ya kiroho zaidi, naombeni msaada wenu nini maana ya hili jambo kwa huyo mtoto?

Maana nyoka alionekana siku chache kabla mama hajapata uchungu, ila baada ya kujifungua tu huyu mtoto, yule nyoka hakuwahi kuonekana tena ndani ya nyumba, na hakuwahi kuonesha ishara ya kutaka kumdhuru mtu yoyote ndani ya familia.

Msaada tafadhali kwa wenye uelewa pia unaweza kum-tag mtu mwenye ufahamu na mnisamehe kama mada haipo kwenye jukwaa sahihi.
 
Tukio kama hilo liiiwahi kumtokea Mke wa Jamaa yangu, lakini yeye ilikuwa ni Paka.

Kila siku usiku Paka anaonekana Nyumba yenyewe iko Gorofa ya nne na full grill.

Mara nyingi yule Kiumbe alikuwa analala kitanda kimoja yule Dada akishtuka yule kiumbe anaondoka

Siku ya kujifungua kile kiumbe kikapotea.

Mpaka leo halijajulikana lengo lla yule Mnyama.
 
Kitu kimoja Bina dam tunatakiwa kujua nikwamba hatuko peke yetu duniani

tuna ishi na viumbe wengi wenye uwezo kuliko sisi japo vitabu vitaka tifu vina tu aminisha kwamba sisi niwa tawara wa dunia

Ila ukweli ni kwamba tuna tawaliwa kwa Siri

hebu jarbu kuchunguza mienendo ya viongozi wakubwa wakubwa wa dunia uta gundua sio Bina damu wa kawaida hasa ukichunguza maamzi yao,hakiri zao.vitu wanavyo fanya

Vita kuambia kitu kuhusu Hawa

KWAHIYO NDUGU YANGU WE ARE NOT ALONE ON THIS PLANET
 
kama maisha yanaenda normal wasichukulie serious kabisa , muhimu wajitahidi kutenda matendo mema maana mema yanaua mabaya mengi.
matendo mema hayana tafsiri ya moja kwa moja kwamba ni hivi au ni vile,bali dhamiri na amani itawaonyesha yaliyo mema katika matendo.

Mungu awape hekima na maarifa.
 
Piga goti mbele za Mungu! Fanya ibada
Nijuavyo mm nyoka ni ishara ya ubaya .Swali ni kwamba kwa nn alikuwa anatoweka wanapojaribu kumdhuru?Maanake ni kuwa si nyoka wa kawaida,maana angekuwa wa kawaida wangemuona anavyoondoka pindi wanapotaka kumpiga.Kwa ufupi huyo nyoka anaweza kuwa na connection na mizimu au uchawi na ujio wake pia una neno na mtoto aliyetarajiwa kuzaliwa na may be ni ishara ya hatma ya mtoto huyo.Hivyo yote kwa yote huyo mtoto inabidi ajitahidi kusali na kuomba Sana ili kama kuna lolote baya linaloashiriwa na huyo nyoka lisimfike maana hakuna haja ya kuogopa lolote Mungu anapokuwa tegemeo lako.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Nijuavyo mm nyoka ni ishara ya ubaya .Swali ni kwamba kwa nn alikuwa anatoweka wanapojaribu kumdhuru?Maanake ni kuwa si nyoka wa kawaida,maana angekuwa wa kawaida wangemuona anavyoondoka pindi wanapotaka kumpiga.Kwa ufupi huyo nyoka anaweza kuwa na connection na mizimu au uchawi na ujio wake pia una neno na mtoto aliyetarajiwa kuzaliwa na may be ni ishara ya hatma ya mtoto huyo.Hivyo yote kwa yote huyo mtoto inabidi ajitahidi kusali na kuomba Sana ili kama kuna lolote baya linaloashiriwa na huyo nyoka lisimfike maana hakuna haja ya kuogopa lolote Mungu anapokuwa tegemeo lako.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
Ahsante kwa machango wako, pia kuna baadhi ya watu walimuambia kuwa hiyo inaweza kuwa ni mizimu ya ukoo wao ambayo haina shida kabisa,

Maana kama ingekuwa ni tatizo ishara zingeonekana maafa na majanga ndani ya familia au magonjwa kwa watoto, lakini amekuwa vizuri tu mpaka leo hii

So nikaona nije huku kwa wataalamu kupata nyongeza zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom