Naomba msaada wa kupata kazi yoyote ile bila kujali vyeti vyangu

Okwaaa

JF-Expert Member
Dec 3, 2020
1,332
2,963
Habari za jioni ndugu zangu 🤝?(ninyi ni kama ndugu zangu)

Najua kuna wakubwa lakini pia vijana rika langu, itoshe tu kusema itifaki imezingatiwa🙏

Kama kichwa tajwa hapo juu, mm ni kijana miaka 25, mhitimu wa chuo 2019 kwa masomo ya sayansi ya jamii. Nimezaliwa Mbozi ila kwa sasa nipo Sumbawanga (nimefika huku siku tano zilizopita baada ya kukosa ajira za ualimu na nyumbani kukawa na maswali mengi si kwa mzazi tu ila toka kwa watu wengi waliokuwa wanajua nasoma na nimemaliza, hivyo nimedharaulika nyumbani na maza pia kachekwa kwa juhudi zake kutusomesha watoto wawili wote lakini hakuna aliyeajiriwa yani maza anapiga vibarua hana pakulima mashamba aliuza ili kulipa ada na ndo chanzo nikakimbia kwanza nyumbani mana nikimwona maza napata machungu mno).

NAJITOKEZA kwenu ndugu zanguni ili kuomba msaada wa kupata kazi ya aina yoyote ile iliyo halali na yenye kunipatia chochote. Sitajari ugumu wa kazi mana nimekulia maisha ya kufanya kazi ngumu. Sihusishi vyeti vyangu jaman labda ikibidi. Kwa sasa naishi kwa kaka yangu naye hana ajira kama mimi.

Jamani sisi sote ni ndugu, naombeni msada wenu. Mama yangu namhurumia zaidi na nahisi yeye ndo anyeumia zaidi yetu anajiambia mwenyewe eti anamkosi😪. Natamani nimwaminishe tofauti na mawazo yake lakini bado😭

Plz jamani. Samahani kwa maelezo merefu🙏

Sorry mmeniomba kozi niliyosomea ni Bachelor arts with education japo juu nilirahisha kwa kusema masomo ya sayansi ya jamii. Masomo ni Geography & Kiswahili. Najua hayaajiriki sasa. Sitaki kuwa mwongo ujuzi mwingine sina zaidi ya kompyuta kwenye Microsoft word na kidogo kwenye Microsoft exile.

LAKINI PIA NIPO NIPO TAYARI KUUZA SIMU YANGU SAMSUNG A10As kwa yeyote ambaye anahitaji kunisaidia kwa kununua cm, nauza 280,000/=, haina shida yoyote ile
 
Pole kwa changamoto ulizopitia, ila umesema ww ni mwalimu kwann pia usingeambatanisha qualification za masomi gan ambayo umesomea
Pia Mungu akutangulie katika hitaji lako mpendwa.
 
unaweza kutumia simu yako kujifunza online skills nyingine zinazolipa kwa sasa, soft na hard skills. Acha stress, jichuchunguze una nini ambacho unaweza kuanza nacho hapo ulipo, huwezi sema eneo lote ulipo hakuna kitu unachoweza kufanya kikakuingizia hata visent kidogo. Stress na kulalamika, huziba macho ya kuona fursa, hata ukiona fursa bado utakuwa na yale maswali...italipa, ikifa itakuweje na maswali mengine yanayozuia uthubutu. Pitia andiko za motivation speaker km joel nananauka na wengine...unahitaji kuwa motivated ndo utulie uanze kuona fursa. Mwisho, practice gratitude....kabla hujaanza kulalamika na kujionea huruma, pata dakika 5 za kutafakari kwa nini umshukuru Mungu mpka hapo ulipofikia, hiyo hali haiko kwako peke yako...wapo wengi.
 
Sure stress zinanitesa mnoo, labda mkuu unaweza nisaidia skills mojawapo inayoweza nisaidia mm kwa kutumia hii cm yngu! Ntakushukru kwa hili mkuu
 
Tatizo ni uaminifu kuwa zero kwa wengi wanaokuja kwa style hii,wakipewa nafasi wanaanza kujijenga kwa kuiba na kusahau walikotoka then wanatoroka.

Ni ngumu sana kupata kazi kwa style hii kwa sasa vijana uaminifu na uvumilivu ni zero kwa sasa wanataka mafanikio ya haraka.
 
Habari za jioni ndugu zangu 🤝?(ninyi ni kama ndugu zangu)

Najua kuna wakubwa lakini pia vijana rika langu, itoshe tu kusema itifaki imezingatiwa🙏

Kama kichwa tajwa hapo juu, mm ni kijana miaka 25, mhitimu wa chuo 2019 kwa masomo ya sayansi ya jamii. Nimezaliwa Mbozi ila kwa sasa nipo Sumbawanga (nimefika huku siku tano zilizopita baada ya kukosa ajira za ualimu na nyumbani kukawa na maswali mengi si kwa mzazi tu ila toka kwa watu wengi waliokuwa wanajua nasoma na nimemaliza, hivyo nimedharaulika nyumbani na maza pia kachekwa kwa juhudi zake kutusomesha watoto wawili wote lakini hakuna aliyeajiriwa yani maza anapiga vibarua hana pakulima mashamba aliuza ili kulipa ada na ndo chanzo nikakimbia kwanza nyumbani mana nikimwona maza napata machungu mno).

NAJITOKEZA kwenu ndugu zanguni ili kuomba msaada wa kupata kazi ya aina yoyote ile iliyo halali na yenye kunipatia chochote. Sitajari ugumu wa kazi mana nimekulia maisha ya kufanya kazi ngumu. Sihusishi vyeti vyangu jaman labda ikibidi. Kwa sasa naishi kwa kaka yangu naye hana ajira kama mimi.

Jamani sisi sote ni ndugu, naombeni msada wenu. Mama yangu namhurumia zaidi na nahisi yeye ndo anyeumia zaidi yetu anajiambia mwenyewe eti anamkosi😪. Natamani nimwaminishe tofauti na mawazo yake lakini bado😭

Plz jamani. Samahani kwa maelezo merefu🙏

Sorry mmeniomba kozi niliyosomea ni Bachelor arts with education japo juu nilirahisha kwa kusema masomo ya sayansi ya jamii. Masomo ni Geography & Kiswahili. Najua hayaajiriki sasa. Sitaki kuwa mwongo ujuzi mwingine sina zaidi ya kompyuta kwenye Microsoft word na kidogo kwenye Microsoft exile.

LAKINI PIA NIPO NIPO TAYARI KUUZA SIMU YANGU SAMSUNG A10As kwa yeyote ambaye anahitaji kunisaidia kwa kununua cm, nauza 280,000/=, haina shida yoyote ile
Nipe mawasiliano yako
 
Kuwa wakala wa kuuza laini za mitandao ya simu jiunge mitandao yote Tigo , Voda na airtel

Hiyo simu usiuze itakusaidia katika hiyo kazi ya kuuza laini za mitandao ya simu ukishaanza kupata pesa utajua mwenyewe jinsi ya kujiongeza
 
Aisee ina vunja moyo kwa kweli

Inawafanya watu walio na nia ya kusaidia kujiuliza mara mbili

Tatizo ni uaminifu kuwa zero kwa wengi wanaokuja kwa style hii,wakipewa nafasi wanaanza kujijenga kwa kuiba na kusahau walikotoka then wanatoroka.

Ni ngumu sana kupata kazi kwa style hii kwa sasa vijana uaminifu na uvumilivu ni zero kwa sasa wanataka mafanikio ya haraka.
 
anzia hapo hapo ulipo...sumbawanga nenda hapo nelson mandela kwenye haisi waombe ujiunge kupiga debe...komaa hata kila siku hadi upate chance...usiingie na digrii yako bebamizigo funga fresh kwenye magari ya vijijini...ukipata kama laki saba nenda ziwa rukwa kulekuna kambale wanauzwa bei poa wa kubanikwa inabidi ukomae ujifunze kubanika na kukesha kwenye moto ujaze mtaji..kiroba kimoja nikati ya laki moja na moja nanusu...unakula gari mpaka tunduma pale bei ya fasta jumla kambale mmoja ni elfu moja..kiroba kinaweza kuingia kambale miatatu...na garama zote kwa wiki unaweza kutengeneza laki tano mpaka saba au kwa wiki mbili kwa kuwa una ugeni itachukua mda kujazamzigo.....sitaki shukrani..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom