Naomba Msaada wa kisheria kuhusu hili la ndoa ya mkeka

JAMBONIA LTD

JF-Expert Member
Jan 22, 2014
584
273
Habari wakuu, kuna binti anadai kijana wetu amempa mimba. Hivyo wamekuja wazazi wa binti kudai ndoa ya mkeka, kinyume na hapo wanatishia kumfunga kijana wetu kwani binti kamaliza form four mwaka jana. Mimba ina miezi 4/5 hivo iliingia wakati akiwa mwanafunzi ingawa kwa sasa amemaliza.

Kijana anakataa sio yake kwani ana muda mrefu hajawasiliana naye na binti mtaani ana mabwana wengi.

Sasa sisi tumesema mpaka ajifungue tupime DNA tutahudumi. Wao wanaendelea kutishia kumfunga.

Je, kisheria wana kipengele cha kumfunga hapo?

Asante
 
Hao wazazi wa bint ni wagwana sanaa na wewe una bahati sanaa
 
Kijana bado anakula kwa baba hivo mzigo utakuwa wa mzee na binti anajulikana ni kicheche mtaani. Hofu ni kifungo naomba msaada wa kisheria kutoka mwanasheria
 
Mambo ya kipumbavu sana.
Waambie wamfunge.
Mahakama zetu dhaifu ila haziwezi kumfunga kwa kosa hilo.
Swali ni moja tu: Huyo ni mwanafunzi wa shule gani?, WIZARA YA ELIMU inaweza kuthibitiaha kuwa ni mwanafunzi?
 

Mambo ya kipumbavu sana.
Waambie wamfunge.
Mahakama zetu dhaifu ila haziwezi kumfunga kwa kosa hilo.
Swali ni moja tu: Huyo ni mwanafunzi wa shule gani?, WIZARA YA ELIMU inaweza kuthibitiaha kuwa ni mwanafunzi?
Kwa sasa si mwanafunzi amemaliza kidato cha nne. Wanadai mimba imeingia akiwa ni mwanafunzi.
 
Hizo kesi za kumpa mimba mwanafunzi zimekaaga kimtego sana. Watakachoangalia ni mimba bint anayo, bint ni mwanafunzi au kipindi anapewa mimba alikua mwanafunzi, bint akimtambua aliyempa mimba tu kesi inakua imeisha saa 12 asubuhi. Ubakaji miaka 30.
 
Hizo kesi za kumpa mimba mwanafunzi zimekaaga kimtego sana. Watakachoangalia ni mimba bint anayo, bint ni mwanafunzi au kipindi anapewa mimba alikua mwanafunzi, bint akimtambua aliyempa mimba tu kesi inakua imeisha saa 12 asubuhi. Ubakaji miaka 30.
Huwa hazihitaji ushahidi? Kama mimba ni yake au laa? Maana binti ni mtu mzima 18yrs ana uwezo wa kumsingizia mimba.
 
Ushauri: Kama unaona usumbufu kupambana na hiyo kesi kubali ndoa then baada ya wiki tu unampa talaka tatu mchezo umeisha ila jiandae kurogwa
Tumeona twende nayo mbele kuoa hapana kwa kweli binti ni kicheche. Aliwekwa ndani tumemtoa walioshtaki wameomba kesi itoke kituo kidogo ieleekee kituo kikubwa cha polisi. Jumatatu nafikiri kutakua na kikao dawati la jinsia pande mbili hakuna muafaka basi itakwenda mahakamani.

Mashtaka yao yanasomeka: kosa la kumzorotesha mwanafunzi masomo kwa kumpa mimba. Wanadai imempelekea kufeli na kuramba zero.
 
Kama kuna mwanasheria bado tunahitaji mwongozo wako
Wamekupa suluhisho jepesi wadau kwamba jifanye mjinga maisha yaendelee kwa kukubali ndoa kisha dogo hata anasafiri anamtelekeza hapo anaenda kusaka maisha, siku zikisonga anajifungua mtoto anatoka sio copy (kama kweli hajampa hiyo mimba) anamlima talaka mchezo umeisha dogo anaoa yule amtakaye.
Ila ww inaonekana unaleta kaubabe ka kutaka kesi, wakikaa vizuri hao unaowadharau dogo anakula mvua 30 kiulani tu na nyie mliokuwa mnataka kesi mnaanza kulaumiana na kurudi kuomba upande mwingine msamaha muyamalize na inakuwa too late.


Umekaa unasema tu huyo binti kicheche kicheche,


Shauri yako,
Kuna dogo alizingua ka issue za kiujana kiutani utani hivi tukachukulia masihara na dharau kama zako hivi,

Gues what?

Alikula mvua 30 na baada ya hapo zikatakiwa hela mingi sana kila mtu akaona ni mzigo basi watu full kuzimiana simu.

Anaendelea na mvua yke
 
Dah aisee acha niitishe kikao cha dharula kabla ya j3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…