Naomba maana ya hii ndoto

Ndondwa

Member
Jan 7, 2016
46
12
Nimeota kama nimechaguliwa kujiunga na chuo fulani hivi (kwa mazingira yake ni cha ufundi). Hcho chuo kina hosteli ambazo wanawake na wanaume hulala pamoja.

Siku tuliyofika kuripoti tulikuwa wanafunzi wengi wa kike na wakiume (siimfaham hata mmoja), tulipo ingia ifisini hatukumwona mwenyeji yeyote pale ndznie (hakuwepo mtu).

Baada ya hapo watu wakaanza kutembea tembea mule ndani ili kuyajua mazingira, mimi na baadhi ya watu tulizunguka kwa nyuma tukakuta kuna matunda mengi na nyani weusi wengi sana wakiwa na vitoto vyao(lakin hao nyani wala hawakutuogopa, wala kututisha, waliendelea kucheza juu ya miti na kula matunda.

Kwenye mlango uliofungwa kuna baadhi ya wanafunzi walikuwa wanataka kuufungua, baada ya kushindwa wakauvunja (walipo uvunja wala hawakuingia ndani, walicho kifanya wakaondoka maeneo yale).

Wakati huo mimi nlikuwa nimepanda juu ya mti (sikumbuki kuwa nlikuwa nakula matunda au la).

Chini ya mti niliokuwa nimepanda alikuwepo mdada ambaye kazi yake ilikuwa ni kuchuma matunda na kuwapiga nyani watoto (nyani hawakufanya chochote bali waliendelea kucheza na kula matunda), lakini baadae yule mdada alimpiga tawi moja jembamba ambalo mtoto mmoja wa nyani alikuwa amekaa, yule nyani alianguka chini.

Baada ya hapo, nyani wote wakanizonga mimi juu ya mti nlioupanda (hawakunishambulia wala kupiga kelele) walikuwa wakiniangalia tu huku wakisogea karibu yangu zaidi, mimi nlikuwa nikijitetea kwa kupiga kelele ya kwamba si mimi, huku ninyoosha kidole kuwaonesha yule dada alipiga mtoto wao.

Dada aliyekuwa chini ya mti alikuwa ametulia kimya kabisa (na hakufuatwa na nyani hata mmoja).

NDUGU WATALAAMU WA NDOTO NISAIDIENI TAFSIRI YA NDOTO HII. Nimeiiota ALFAJIRI.

Natanguliza shukurani
 
Ndoto ya maruhani iliyochanganyika na mizimu.matunda huwakilisha neema nyani ni mizimu.ndoto za shule huwakilisha huduma,yani kuhudumia jamii.ni ndoto za kiugangauganga.unaandamwa na mizimu ya kiganga
 
Ndoto nyingine hutokea kupitia mawazo uliyoyawaza sana wakati wa mchana ama kitu ulichokiona ama kufanya mchana unaweza pia kukiota mfano kama ulitembelea mbugani ama ulikuwa barabarani ukaona hao manyani unaweza kuja kuota kitu kile kile usiku.....Mimi huwa naota magumashi siku nikilala bila kusali ila nikisali usiku nalala usingizi kama mtoto mdogo yaani kama vile sidaiwi ada ya watoto wala sinamajukumu yeyote....Nikishaamka tu asubuhi majukumu yote nayo yanaingia kichwani hadi najuta kwanini nimelalala mpaka saa hizi.
 
Ndoto ya maruhani iliyochanganyika na mizimu.matunda huwakilisha neema nyani ni mizimu.ndoto za shule huwakilisha huduma,yani kuhudumia jamii.ni ndoto za kiugangauganga.unaandamwa na mizimu ya kiganga
Ahsante kwa mawazo yako
 
Ahsante kwa mawazo
 
Tena kitu kingine, mimi huwa sioti ndoto mara kwa mara, naweza kukaa hata miezi miwili bila kuota
 
Nna tafsiri mbili, ya kwanza kabla sijatafsiri naomba nikuulize swali. Una mtu wako wa karibu ambae ameokoka na anaomba sana juu ya familia yenu au juu yako?
 
Nna tafsiri mbili, ya kwanza kabla sijatafsiri naomba nikuulize swali. Una mtu wako wa karibu ambae ameokoka na anaomba sana juu ya familia yenu au juu yako?
Ndyo, mama yangu mzazi ameokoka
 
Ndyo, mama yangu mzazi ameokoka
-Good, sasa apo Mkuu inaonesha mama yako ana vita vikali sana vya kupambana na roho chafu, ninaposema roho chafu ina maana mapepo ambayo yanakamata maisha ya watu kama uzinzi, magonjwa, shida, laana n.k.

-Kitendo cha wewe kupanda juu ya mti na bila kugombana na hao wadudu inaonesha kuwa hizo roho chafu umeambatana nazo na ndo maana ulivyopanda tu wala hao wanyama hawakushtuka, hii inatokana kwamba wanakuona wewe ni mwenzao.

-Huyo mwanamke uliyemuona chini ya mti akiwapiga nyani ina maana ni mtu ambaye anazipiga hizo roho na imeonekana kuna kipindi alikuwa hajui ni namna gani ya kuzipiga ila alipotuma fimbo ndo ukaona kuwa imeleta mtafaruku kwa hao nyani(roho chafu) zimekugeukia wewe kwa ajili malipizi ya kisasi. Mama yako anapaswa kukemea malipizi ya kisasi baada ya kupambana ktk hiyo vita. Ila kikubwa zaidi ni wewe Kuokoka na kuanza kukemea hizo roho kwako.

-Kuhusiana na hii ndoto uliyoota mwambie mama yako na ikiwezekana mwambie hata ni namna gani ulivyotafsiriwa, yeye atajua namna gani ya kupambana.
 
Sawa mkuu, nitaongea na mama
 
Sawa mkuu, nitaongea na mama
Ndoto zina maana sana Mkuu ila wanadamu tunapenda kuzipuuza ila Mshkuru Mungu kwa kupata Neema ya kuikumbuka hiyo ndoto.
Na mara nyingi mambo kama haya inakuwaga ni mizimu na mambo ya kichawichawi, ila yote hayo ni madogo sana mbele ya Yesu. We si umeona imeguswa tu kidogo, yenyewe ikatetemeka.
Mimi ntakuwa pamoja na wewe ktk ushauri kwenye mambo haya, jibu atakalokupa mama unaweza ukanitarifu PM. Kuwa na amani, Yesu alikuja ili kutuweka wanadamu huru.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…