Naomba kujua sheria ya leseni ya udereva kama imebadilishwa ama La!

Brice85

JF-Expert Member
Oct 18, 2015
873
1,758
Naomba msaada kujua sheria inayosimamia leseni hususani leseni ya udereva kama imebadilishwa au La.
Ndugu wana jamvi siku za nyuma kabla hatujaletewa leseni mpya kwa kipindi kile tulikuwa tunatumia leseni kama vitabu, madaraja ya leseni yalikuwa haya haya isipokuwa daraja B ndilo halikuwa maarufu. Nasema hivyo kwa sababu sikuwahi kukutana nalo popote pale na daraja C1 na C2.

Hivyo kama ilivyofahamika kwa kipindi kile:-
Daraja A ilikuwa kwa pikipiki na daraja D kwa magari binafsi yenye uzito usiozidi tani tatu na nusu na yasiozidi abiria 7.
Daraja C ni kwa magari yote ya abiria.
Daraja E ni kwa magari ya mizigo kuanzia tani tatu na kuendelea.
Daraja G ni Trecta na
DarajaF ni kwa mitambo.

Sasa baada ya kuja hizi leseni mpya, kwanza madaraja yaliongezeka kuwa A, A1, A2, B, D, C, C1, C2, C3, E, F na G na haikuishia hapo yakachorewa na michoro ya mfano wa vyombo husika vinavyotakiwa kwa kila daraja.. sasa hapa ndipo penye shida kubwa kwangu na watu wengine pamoja na watu wa usalama barabarani katika kutafsiri hii kitu.

Michoro inaonyesha :-
daraja A zote ni pikipiki na makundi yake,
daraja B ni gari aina ya SALOON,
daraja C ni BUS huku daraja C1 ni Bus na tera na daraja C2 ni Bus dogo na tera huku daraja C3 ni Tax.
Wakati daraja D ni mfano wa pickup
daraja E ni Marori
daraja F ni mitambo na
daraja G ni trecta.

Swali langu hii sheria imebadilishwa kutokana na matumizi ya madaraja ya leseni? Maana huku barabarani kila mtu anazungumza lake.

Juu ya daraja B, D imekuwa ikiwachanganya wengi wa watu wakiwemo madereva na askari wa usalama barabarani.
 
Nimeambatanisha na picha
0b58e1812696050ebd7e10ee9ee92e66.jpg
 
Jamani naombeni msaada wenu: kipindi nikiwa na miaka 23, nilipata leseni ya daraja E, ila nimekaa nayo mpaka imekua expired ni nikaogopa kwenyenda ku renew na kushusha daraja ili nibakiwe na daraja D maana sina vyeti vya kuonyesha kuwa nilisoma ilo daraja E, ni muda sasa umepita nimekuwa muoga sana kwenda kubadili reseni yangu kwa kuogapa kuuliza maswali na kuchukuliwa hatua kali za kisheria juu yangu. Msaada tafadhali
 
Ku renew leseni ikiwa kama ilivyo mwanzo. hakuna shida huto ulizwa chochote wala hakiitajiki cha ziada zaidi ya leseni yako iliyo expire.. ikiwa labda utaitaji kuongeza daraja ndio itaitajika chet kwa ajili ya daraja usika
 
Daah mkuu nilishapata kisanga kama chako. Lakini kuna mtu wa Mungu humu JF alinisaidia free of charge. Mungu amtimizie haja ya moyo wake
 
Dah! Sijaelewa kabisa hayo madaraja!
Kama una gari yako ndogo binafsi ya kutembelea mf.IST na Boxer ni daraja lipi hapo linahusika kwa mtu mmoja mwenye kumiliki hivyo vyote 2 !?
 
Back
Top Bottom