Naomba kujua ni biashara gani inayofaa katika eneo lenye vilabu vya pombe vingi maarufu kama ubanda

thadayo

Senior Member
Jan 28, 2023
183
175
Mimi ni mjasiriamali mdogo nipo kijiji ambacho Kuna shughuli za uuzaji pombe jina maarufu ubanda, naomba kupata mawazo ya biashara ambayo itaendana na mazingira hayo.

Nipo tayari kupokea mawazo yenu wakuu.
 
Weka sufuria kubwa uuze mapupu, kongoro, supu ya utumbo, choma mishkaki ile ya bei ndogo, hapo uwe na pilipili ya kutosha wapikie na ndizi kidogo kwenye supu hiyo hapo umemaliza
 
Uza ugolo, tumbaku, sigara anzia nyota, master, winston na kadhalika
Mara nyingi vitu hivyo ulivyo taja vinapatikana mule mule ndani katika maubanda Kwa nilivyo kuelewa wewe mradi wako uwe unajitegemea wenyewe nje ya Hizo ubanda..
 
Gozo, supu ya washiwashi na bandama,vichwa,utumbo na miguu ya kuku ya kukaanga
 
Mara nyingi vitu hivyo ulivyo taja vinapatikana mule mule ndani katika maubanda Kwa nilivyo kuelewa wewe mradi wako uwe unajitegemea wenyewe nje ya Hizo ubanda..
Hiyo anaweka kameza nje ya mlango wa kuingia hapo masankuroni
 
Hapo Biashara nzuri tengeza Supu,iwe ya mapupu,kichwa Cha Ng'ombe au miguu ya mbuzi.

Unauza cheaper kuliko uliowakuta, maana naamini wapo. Unaweka ya 1000 na ya 500.

Unauza pia hapo Ndizi za mchemsho za bei rahisi.

Biashara nyingine inategemea na Imani yako, kama ni mkristo nenda machinjio ya 🐖 asubuhi, Kuna nyama nyingi za bei rahisi. Ulimi, masikio, mkia, maini, maziwa na nyama nyingine za ndani. Vinauzwa hapo Bei rahisi.

Unakata vipande vya 1000 na 2000.Unakaanga na Ndizi,usisahau Kachumbari na chachandu yenye pilipili nyingi.Utawakamata.

Kama ni lifeist na unataka Hela ya maana,na hapo ni kwako na una kauwanja kidogo.Pia kama huo mtaa wa ubanda umechangamka na Kuna movement,Tengeneza vyumba vya kupangisha visiwe vikubwa sana.

Weka kitanda 4×6, Nenda mtaa mrefu Mtafute dada Mkubwa wa hapo mwambie una vyumba unahitaji watu wa kazi. Atakuletea, maana supply ni kubwa kuliko demand.

Minimum utakunja 15000 daily Kila chumba.Kula vizuri na watu tu.
Nimemaliza..👊🏾.
 
Weka Lodge bubu ya kienyeji.
Weka banda la kitimoto.
Chajisha simu, makava, memory card na kuweka nyimbo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom