NGURI PORI
JF-Expert Member
- Oct 29, 2011
- 3,053
- 3,259
keyboard imecorrect vibaya ila inaeleweka ni tochi kama tulivyozoea kuziita not touchPitia tena kichwa cha habari Traffic camera aka......
Mkuu haukupigwa changa la macho. Teknolojia hiyo hapa Tanzania ipo kwa hizi tochi mpya. Hata mimi binafsi nilikuwa natoka Dar kwenda Dodoma, kuna eneo lipo kati ya Morogoro na Dodoma nadhani ni maeneno ya Mdaula nilipita kwa mwendo wa km 100 kwa saa lakini nikaja gundua mbele kuwa like eneo ni la kutembea 50km/h kwa kile kibao cha kunishukuru kwa kutembea mwendo unaoruhusiwa. Basi sikumaliza hata km 3 toka pale nikasimamishwa na trafiki na kuambiwa nilipita sehemu isiyoruhusu kutembea zaidi ya 50km/h nikabisha. Trafiki wakasema paki gari vizuri pembeni ushahidi unakuja,nikaweka gari pembeni. Basi baada ya kama dakika 10 akaja askari kavaa kiraia tu na akatoa kamera na kuonyeshwa tena picha nzuri kabisaaa za kisasa na mwendokasi niliokuwa natembea na hadi magari navyoyaovateki. Basi nikalipa fine lkn nia hasa ilikuwa ni kujiridhisha na kuthibitisha ukweli wa hizi tochi. Hivyo mkuu hukuibiwa
Hao traffic police wapo very curious katika kuangaika na dunia, utakuta polisi kajificha hadi pua haionekani na tochi, Serikali inabidi muwatafutie CAMOUFLAGED WEAR manake hizo nguo nyeupe wengine tuna macho makali kama Mimi huwa naziona km100 kabla.
Kweli ipo kwanza maeneo ya muleba tu bukoba na ushuhuda ipo iko advance ata kuliko za kenya juu iko na kumbukumbuKuna App iko playstore ina detect camera "Tochi " ya polisi...
Ukiwa una-drive ;
1.simu yako iwe fully charged..
2. Simu iwe na bundle muda wote...
3.Washa Gps ya simu yako.
4. Fungua ile application..
-Itakuwa inakuonyesha speed ya gari yako..
- then kuna display ingine Itakuwa inaonyesha Road map , mahali ulipo na mahali Tochi ilipo ( penye Tochi pataonyesha red)
App anaitwa Speedometer Gps
Install speedometers GPS to drive over 100km/hr anytime.
Hakuna kitu kama hicho, ila hilo eneo anakuepo askari anajificha au anavaa kiraia tu, kazi yake ni kupiga tochi tu ila hasimamishi anachofanya anawapigia simu wenzie mbele huko unakoelekea kwamba gari fulani imepita hapa spead kubwa isimamishwe ipigwe faini.Jana nilikia njiani Kutokea Singida .. Mbele ya Magugu kidogo kukawa kuna Kibao cha 50km/h Limit speed .
Kwa bahati mbaya kulikua na mazungumzo kwnye gari kitu ambacho kilinifanya nipite pale na speed ya 80 ..nimekuja kushtuka kua nilikua kwnye 50km/hr Zone baada ya kuona kile kibao kinachoashiria sasa umemaliza eneo la 50km/hr.
Tukacheka tukasema bahati yetu Hakuna TOCHI .
Tukatembea Umbali kama wa 2Km hivi . .. tukasimamishwa ... tukaambia Kuna Satelati Camera zimewapiga Picha Mahala Flani Mmepitiliza speed .
Duh kwanza nikacheka ...huku nikingoja ushahidi .,
Ushahidi wa kwanza ana namba ya gari yangu kwnye List yake ..nikasema kaandika sasa hivi au ?
Ushahidi wa pili akasema ,kaa dakika 10 ,tunangoja picha yako inatumwa (hapo ndipo nilichoka ) .. mm kwa vile nilikua na haraka sikuona haja ya kungoja mda wote huo ...nikalipa fine off nikaondoka coz kweli pale nilipitiliza ..
Je ni kweli kuna technology ya namna hiyo Tanzania hii kunasa picha pale unapooverspeed ,au niliingizwa mjini kwa kelele za Tarumbeta .