Miye navyojuwa haya hybrid kwanza yanatumia batteries na mafuta kwahiyo. Ukiwa unatumia nguvu kidogo unakula battery na ukitaka nguvu sana mwendo ndo mafuta yanatumika. Hizi batteries huwa zina mda wake wakutumika kama 5-10 years then needs to be replaced. Kuzipata bongo ndo tatizo na unaweza ukanunuwa gari nalikawa na defective batteries ikala kwako kuagiza mpya.
Kwenye electric cars hizi nazo zinatumia batteries full time unachaji kama simu. Magari haya kwa kuchaji nyumbani mpaka lijaye mengi yanachukuwa zaidi ya 8hrs na yanakuwa na range ya kuanzia km 200-500 hapo ukilichaji mpaka litakapo isha chaji. Lakini pia mwendo wako na mazingira inategemea yanaweza kumalizia chaji. Kimsingi pia haya yanakuja na batteries tuu kwahiyo batteries zake zikibuma lazima ureplace ndo ifanye tena kazi. Kwahapa bongo magari haya nichangamoto sana inabidi umpige shule fundi wako na YouTube kila wakati ukiwa na tatizo na parts lazima uagize toka huko kwawenzetu.