Nani zaidi: Mkuu wa Mkoa au Meya wa jiji?

Doto Dotto

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
3,803
2,775
Wana JF wooote heshima kwenu...

Uchaguzi wa meya wa jiji letu letu la Dar umeisha na Bwana Isaya Mwata ameibuka kidedea kuwa meya mpya wa hili jiji.

Sasa swali langu ni hili, kati ya mkuu wa mkoa na meya wa jiji nani mwenye Madaraka/ mamlaka au mwenye sauti juu ya mwenzie? Maana nahisi kutakuwa na mgongano hapa kati ya Makonda na Isaya.

So mwenye uelewa zaidi wa hili jambo plz anisaidie.
 
mwenye wananchi ambaye ni Meya ila mkoa wa Dar kawekwa yule aliyeacha busara juu ya mto atajifanya anataka kumkunja meya ha ha ndipo atakapotawala kwa taabbuuuuuuuuuuuuuuu,cheo cha zawadi ya kikabila kama cha mkuu wa mkoa wa Dar tofauti na kile cha kuchaguliwa na wananchi
 


Jibu ni rahisi tu, Mkuu wa Mkoa ndiyo Raisi wa Mkoa na vyombo vyote vya usalama vya Mkoa viko chini yake, Mkuu wa Mkoa anawasiliana na Raisi wa nchi moja kwa moja ambaye (raisi) nafikiri ana uwezo wa kuvunja Baraza la udiwani na hata kwenda mbali kubadilisha mfumo wa Utawala wa Mkoa, hivyo Mkuu wa Mkoa ndiyo kila kitu Mkoani, Mkuu wa Mkoa akigoma hakuna kitakachofanyika hata kama Meya akiamua lkn Meya akigoma Mkuu wa Mkoa ana uwezo wa kumzunguka na kukifanya nyuma ya mgongo wake!
 
Kwanza ingefaa wanadar es salaam au Watanzania kwa ujumla, viongozi wa vyama vyote mawazo kama haya tuweke pembeni, nani mkubwa nani mwenye mamlaka kwani tunahitaji maendeleo au Kuna kuleteana ubabe?? kwa mawazo haya ni ngumu kuwaletea wananchi maendeleo, wanasiasa wote wenye akili hizi. mawazo kama haya ndo yalosababisha mfarano kati ya kubenea na Mheshimwa Makonda., WANASIASA TAHADHARINI HATUTAKI HIZI FIGISUFIGISU UCHAGUZI UMEKWISHIWA TUJENGENI NCHI.
 
Ni sawa na kuuliza Raisi na Spika nani zaidi
Umeona eeh? Namnukuu "maana nahisi kutakuwa na mgongano hapa kati ya Makonda na Isaya..." Mgongano utatokea iwapo mmoja wao atashindwa kujua majukumu yake yanaishia wapi
 
Kiutendaji jiji linamtegemea sana meya kwa mantiki ya makusanyo ya kodi na utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo ya jiji. Mkuu wa mkoa ni oversear wa shughuli zote za mkoa na anamtegemea sana meya wa jiji. Kwa kifupi wote ni muhimu kwa nafasi zao na wanatakiwa washirikiane ile isije tokea "conflict of interests" za vyama vyao.
 
ha ha ha ataipata mkuu wa mkoa wa kuzunguka nyuma hapo Kinondoni alikalishwa na Boniface hata mifuko ya simenti hakuwa hata pakuiweka atumie busara maana hakuna kitu chochote cha maendeleo kinafanywa bila baraza la madiwani mkuu wa mkoa ni karani wa raisi tuu vyombo vya ulinzi na usalama vipo chini yake kweli na havijawahi kuwa jibu la mendeleo
 
Sasa swali langu ni hili. kati ya mkuu wa mkoa na meya wa jiji nana mwenye Madalaka/ mamlaka au mwenye sauti juu ya mwenzie? maana nahisi kutakuwa na mgongano hapa kati ya Makonda na Isaya

Meya ndie mzoa takataka na mzibua mifereji ya maji machafu mkuu wa jiji.Mkuu wa mkoa ni msimamizi wa shughuli zote za serikali mkoani.Yeye ni Raisi wa mkoa akisimamia shughui zote za kiserikali mkoani.
 
Yesu alipowasikia wanafunzi wake wakirumbana kuhusu nani mkubwa akawaambia, "aliye mkubwa ni yuke anayewatumikia wenzake"
Tatizo hapa kila mtu atataka aonekane yeye ndo zaidi. si unajua watu wanavotaka sifa?
 
Mkuu wa mkoa hana nguvu kwa meya kwasababu, cheo chake ni cha kisiasa na anateuliwa na hana mamlaka yoyote kiutendaji, majukumu yake ni ya jumla jumla tuu na uteuzi wake unaweza kutenguliwa wakati wowote tofauti na meya ambaye anapatikana kwa kupigiwa kura na nafasi yake ni ya kiutendaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…