GEBA2013
JF-Expert Member
- Feb 22, 2014
- 4,982
- 6,310
Imefika muda serikali iwe na huruma na wananchi wake. Vijana wanaotoka katika familia maskini ndiyo wamekuwa waathirika wakubwa wa haya makampuni ya kitapeli, na serikali imeshindwa kuwalinda dhidi ya hawa matapeli.
Kuna mtoto wa rafiki yangu ameitwa Tabora kufanya kazi na hiyo kampuni kwa ahadi ya kwamba watamlipa shilingi laki 3 na 75 elfu. Cha kushangaza, alipofika wakamwambia atoe 40,000 ya usajili. Akawa hana, ikambidi ampigie baba yake simu ampe hiyo kiasi. Babake akamtumia. Baadaye wakampigia, wakamwambia atoe 25,000 ya chumba na kiasi cha fedha kwa ajili ya uniform. Haikutosha, wakadai awatafute watu wawili au zaidi kwa ajili ya kujiunga na kampuni ili alipwe mshahara mzuri.
Tukamwuliza kama amelipwa mshahara na ana zaidi ya mwezi na nusu, anadai hajalipwa. Cha kushangaza, jana amepiga simu anadai apewe laki 6 aipe kampuni ili aajiriwe. Mzazi akapigiwa na boss wa hiyo kampuni, anadai apewe laki 6 ili kijana aajiriwe na kupanda daraja. Mzazi akasema hana, akawa anambembeleza apewe hata laki 3 awali na nyingine baadaye.
NANI YUKO NYUMA YA HAYA MAKAMPUNI?