Nani yuko nyuma ya hili Tamasha la Matokeo ya Sensa?

Engager

JF-Expert Member
Jan 12, 2011
1,489
3,174
Ifike pahala labda itoshe tuu kuwajua wanao tuhujua hata kama hamna kitu tunaweza kuwafanya. Nafsi zetu ziwanung'unikie tuu watalipwa mbele kwa mbele.

Najiuliza ni pesa ngapi zimetumika kuandaa hili tamasha la kuambiwa tuko mil.61? Hivi kweli hawa watawala hawajaona hata shida tu ya maji dar wakaelekeza hizo pesa kukabili changamoto walau hiyo moja ya dharura?

Nchi inanuka shida, maisha yanakuwa magumu kila kukicha, mfumuko wa bei haukamatiki, halafu inapatikana wapi bajeti ya kufanya tamasha useless kama lile?!

Social media za kumwaga, radio, television etc etc... hadi muandae shughuli na helkopter juu kuonesha idadi ya watanzania kweli?!

Ni nani huyu yuko nyuma ya hii idea? Huyu mtu amefanya hivi kwa manufaa ya nani? Kwa umhimu gani?. Na ukija kusomewa bajeti iliyotumika hapo unaweza uzimie.

Tumuombe CAG aliangazie hili zoezi la sensa tangu limeanza hadi hili tamasha la leo tuone madudu humo.

Kama kunamtu kashindwa kupata point katika maandishi haya anisamehe bure. Nimeandika kwa jazba😠
 
Punguza jazba, huo ni mzunguko wa pesa unaboostiwa, hata matokeo ya sensa yangetangazwa kimya kimya hizo pesa usingepewa wewe wala Mimi.

Punguza makasiriko pambana ukae kwenye line ulambe asali.
 
Ukiziangalia sana fedha zinavyopigwa unaweza kuugua if yo can't defeat them join them
 
Wanatafuta kuhalalisha ufisadi wa B600 zilizotajwa kutumika katika zoezi zima la sensa hiyo.
 
Back
Top Bottom