econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 18,886
- 27,395
Kwa Sasa Tanzania ipo kwenye Hali ya state capture, baada ya serikali, vyombo vya Dola , mahakama na bunge kuwa kitu kimoja na kuondoa uwajibikaji. Leo bunge limeacha kazi yake ya kuisimamia serikali baadala yake limekuwa rubber stamp ya maamuzi ya serikali. Kwa mfano bunge la Tanzania limetumika kupokea wabunge wasiokuwa na chama au waliofukuzwa kwenye chama chao.
Ila kwa sababu ya state capture bunge linafanya maovu na hakuna wa kuligusa. Bunge kupitia Spika wake wameona suala la wananchi kutekwa sio la msingi kujadiliwa bungeni ila kumpongeza Rais Kwa hotuba yake ndio la muhimu zaidi.
Swali ni je, nani atasaidia tuondokkane na bunge la mchongo lililojaa machawa wa serikali wasiojua majukumu yao?.
Mahakama ndio imeoza kupindukia. Kuna kipindi Jaji Mkuu Ibrahim Juma alisema hadharani ya kwamba majaji watoe hukumu kwa kuangalia falsafa ya serikali.
Yani baadala ya mahakama kuwa huru na kufanya maamuzi stahiki, Jaji Mkuu anashauri majaji waangalie muelekeo wa serikali ni upi.
Jaji Mkuu mwenyewe alitakiwa kustaafu kwa mujibu wa Katiba ila kutokana na state capture aliongezewa muda kinyemela. Ndio maana Rostam Aziz alidai ya kwamba mahakama zetu zinapigiwa simu tu na kutoa maamuzi.
Swali ni nani atawasaidia wananchi waondokane na mahakama mbovu ya Tanzania?
Vyombo vya Dola navyo vinajiendesha under state capture.
Ndio maana mpaka Leo tunajikanyaga kuhusu nani anateka watu na kuwapoteza. Polisi hawajui, TISS hawajui na hata JWTZ hawajui. Sasa nani atawalinda wananchi dhidi ya utekaji . Leo Kuna wananchi jumla ya 89 wamepotezwa mpaka Leo ila kila mtu hajui wapi wapi. Yani raia anaondolewa kwenye basi na kuuawa na hakuna anayewajibika.
Inasikitisha sana. Kutokana na state capture wananchi watazidi kupotezwa na hata kuuawa bila ya msaada. Nani atawasaidia wananchi na huu ukatili?
Serikali imejaa dharau na kebehi. Waziri wa Fedha alifikia sehemu ya kusema asiyeridhika na tozo ya miamala ya simu ahamie Burundi. Kauli za dharau na kiburi maana hakuna wa kumwajibisha. Rais Samia akatoa Lugha ya dharau kwamba wanaotekwa wanajiteka wenyewe.
Na hakuishia hapo akaendelea kudai hata waliouawa kwenye matukio ya utekaji Vifo vyao ni vya kawaida. Yani kwake uhai wa raia ni kawaida tu. Anaongea hivyo maana state capture inamsaidia na hakuna uwajibikaji na hakuna atakalofanywa. Ni nani atatusaidia tuondokkane na Rais mwenye kiburi na dharau Kama huyu?
Leo Tanzania Tume ya Uchaguzi inaweza kuamua kuwapa CCM majimbo yote na hakuna atayeiwajibisha.
Leo watu wanaweza kuamka asubuhi na kwenda kuapishwa bungeni bila kuwa na chama na Wakaaapishwa.
Mimi nadhani Kuna njia nne za kuondokana na huu ufirauni wa state capture nchini Tanzania.
1. Katiba Mpya itakayoweka structures na uwajibikaji. Yani mtu akitekwa hadharani mchana akaenda kuuawa , RPC wa eneo lililotokea utekwaji anawajibika mwenyewe kwa kutochukua hatua. Juzi hapo Kenya IGP Msaidizi alihukumiwa miezi SITA jela kwa kudharau mahakama baada ya raia kupotea bila sababu. Pona yake wale raia wawili waliopotea walipatikana siku hiyo na yeye kuomba msamaha mahakama na kusamehewa.
2. Mass Uprising. Wananchi waanazishe maandamano nchi nzima kushinikiza kuoondka kwa state capture Tanzania. Hii kwa Tanzania itakuwa ngumu mpaka pale kila mmoja atakapoguswa .
3. Second Liberization movement. Hapa ni kuanzisha kikundi Cha uasi kuondoka state capture na kurudisha mamlaka kwa wananchi. Hii njia sio nzuri maana itapelekea vita na mauaji na mambo mengi kurudi nyuma.
4. Kumuomba Mungu afanye miujiza tuondokane na hii laana ya state capture.