VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Rais ni mkuu wa Serikali na nchi. Rais ni nembo yetu; fahari yetu; kiongozi wetu na kiungo chetu. Lakini, Rais ni 'mwajiriwa wetu' nambari moja nchini. Ndiyo maana, akifanya vizuri tunamsifu na akifanya vibaya tunamkosoa na kumsema.
Tunapaswa kujua anakoenda na anachoenda kufanya. Labda kama anakwenda likizoni. Usirisiri kwenye mambo yamhusuyo Rais wetu unatutisha na hatuupendi. Ukomemeshwe hadi ukome. Huu ni ujumbe wangu kwa wahusika wote wa ulinzi na protokali za Rais wetu.
Ilianza kule Kenya. Raila Odinga, kinara wa upinzani nchini Kenya, alidai kuwa Rais Samia alikwenda nchini Kenya kwa ajili ya kujaribu kuwapatanisha Raila na Rais William Ruto. Habari hii ilishtua wengi. Iliwezekanaje Rais Samia, aliyekuwa na nia ya amani ya Kenya, kwenda sirini na kisirisiri?
Ikafuata kuonekana ndege ya Rais kule Uarabuni hivi majuzi. Kama watanzania, hatukutangaziwa wala kufahamishwa kama Rais wetu ana ziara Uarabuni. Iliwezekanaje ndege ya Rais wetu (iliyoashiria kuwa Rais alikuwa huko pia) iende kisirisiri Uarabuni?
Ratiba za Rais wetu ziwe wazi. Mambo yake kama Rais yawe wazi. Kufichaficha na kumsafirisha Rais wetu sirini hakuna faida. Tutaambiwa nini ikiwa jambo lisilovutia likimtokea Rais wetu huko anakokwenda kwa siri...hukohuko sirini? Nani anaratibu mambo haya hatarishi kwa Rais wetu?
Rais ni public figure. Tunapaswa kujua yote anayoyatenda kama Rais.
Mzee Tupatupa wa Lumumba (Kilosa, Morogoro)