Nani anamlipia Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Matangazo Mubashara Clouds TV?

Fortilo

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
5,026
15,656
Sote tunakumbuka ya Clouds na report ya CAG kuhusu malipo zaidi ya milioni 600, kwa kisingizio cha kutangaza utalii wa ndani.

Leo, kati kati ya huduma mbovu za miundo mbinu ya bara bara, shule, na mahitaji lukuki ya hospitali za umma, kwenye mkoa wa Dar es salaam, mkuu wa mkoa yupo mubashara kwa zaidi ya saa 5 ( 5hrs Live on popular countries TV station) kila siku kwa takribani wiki mbili sasa.

Swali la kujiuliza;
1. Clouds kama TV binafsi, ina maslahi gani na office ya Mkuu wa mkoa wa Dar ambayo vyombo vingine vya habari havistahili?
2. Nani analipa gharama
3. Clouds walishiriki tenda wapi na wakashinda?

Kuna haja gani ya mkuu wa mkoa kuwa mubashara akitatua "kero" za wananchi.

Amos Makalla ni mtu anaeheshimika kama ni fair na Muungwana, lakini hili linafanya watu wajiulize credibility yake.

Kwa wale wasio jua gharama ya kwenda Mubashara kwa sec 30 kwa chombo maarufu kama clouds si chini ya TZS 500,000, sasa piga =500,000x2x 5x60
Kila siku nani analipa? kwa maslahi ya nani?
 
Ni vizuri viongozi wachape kazi kuliko kuwaa kwenye media hadi wanatoa maboko. Hao clouds Sabaya alikuwa anatumia na hakujua kumbe kuongea kwake ndo anajiexpose,Makalla tumpe mda tu atakuja kujifunga
 
Ni vizuri viongozi wachape kazi kuliko kuwaa kwenye media hadi wanatoa maboko. Hao clouds Sabaya alikuwa anatumia na hakujua kumbe kuongea kwake ndo anajiexpose,Makalla tumpe mda tu atakuja kujifunga

Mkuu ahsante,

Ila kwenda live 5 hrs kutoa "boko" ni suala lisilo kwepeka.
 
Tuanzie hapa kwanza, kwani Paul Makonda pesa za kuwalipa alikuwa anazitoa wapi Clouds wazee wa fursa wale, wanaweza kujitoa huku, ili wapate kulee!! Na shughuli hata iwe ndogo vipi ukiwakabidhi lazima iwe bonge la shughuli!!!
 
Tuanzie hapa kwanza, kwani Paul makonda pesa za kuwalipa alikuwa anazitoa wapi?clouds wazee wa fulsa wale, wanaweza kujitoa huku, ili wapate kulee!!na shughuri hata iwe ndogo vipi ukiwakabidhi lazima iwe bonge la shughuri!!!
Ila unadhani ni sawa mkuu? Fursa kwenye mali za Umma ni sawa?
 
Kwa miaka hii ya kariburini,Kunenge ndio RC bora kabisa. Anafanya kazi kwa vitendo na sio kutafuta kiki kwenye Media.
Nakubali 100%, Mkuu nadhani kama taifa tunalipia kwa gharama kubwa sana baadhi ya mapungufu binafsi ya viongozi wetu, so sad... weak leaders ndio wanapenda show offs za kijinga hivi, ila nani analipa?
 
Marehemu Ruge Mutahaba wakati wa uhai wake mbona alishatamka kwamba kwenye mambo ya maendeleo Clouds FM wapo tayari kutoa airtime bure kwa wadau ikiwemo wanasiasa

Aliyasema hayo katika lile sakata la Makonda kuvamia radio yao kwa bunduki. Tulichukulie hili suala positively
 
Hao clouds watu wakujiongeza mkuu.

Watu wakujisogeza kwa watawala ili kusogeza baadhi ya agenda zao na ku i win system,
Huyo makala hapo halipi sent tano.

Wanafanya ivo vitu miaka mingi sana kama ni mfuatiliaji mzuri.

Na hii ndo imekua silaha yao kubwa sana miaka yote.

Ni watu wajanja wajanja sana.
 
Marehemu Ruge Mutahaba wakti wa uhai wake mbona alishatamka kwamba kwenye mambo ya maendeleo Clouds FM wapo tayari kutoa airtime bure kwa wadau ikiwemo wanasiasa

Aliaema hayo katika lile sakata la Mqkonda kuvamia radio yao kwa bunduki. Tulichukulie hili suala positively
Ni kweli kwani kabla kabisa ya kuanza kampeni yake ya kusikiliza kero jimbo kwa jimbo nilimsikia RC akiwa clouds kueleza kampeni yake hiyo,na kuwaomba clouds kumuunga mkono katika kutangaza na kuhamasisha, na clouds kama redio ya watu walimkubalia kwani wao hujitoa kwa mambo yenye maslahi mapana,hata kama kutajitokeza wadhamini kugharamia baadhi ya gharama lakini clouds walijitoa kwa moyo mmoja.jambo analolifanya RC ni jema sana,na ndio dhana ya kiongozi bora ya kutokukaa ofisini na kufuata wananchi maana kero zipo huko
 
Kama Clouds TV /Radio Wana Sera ya kurudisha fadhila kwa jamii (Corporate Social Responsiblity) kwa mapokezi wanayopata.kutoka kwa wadau wao na Mkuu wa Mkoa ameomba mikutano yake irushwe ili kufikisha ujumbe kwa wananchi walio wengi (na amepewe).
Ninadhani ni wazo zuri,lakini kama huduma hii itahusisha malipo,ni mzigo mkubwa kwa walipa Kodi,Mkuu wa Mkoa angetumia utaratibu mwingine kufikisha ujumbe wake.
 
Back
Top Bottom