Nani amelielewa tangazo hili la Bank of Tanzania (BoT), atufafanulie!

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
19,796
23,094
Tangazo ni hili
--
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUONDOA KWENYE MZUNGUKO NOTI ZA ZAMANI ZA SHILINGI YA TANZANΝΙΑ

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuufahamisha Umma kuhusu zoezi la kuondoa kwenye mzunguko noti za zamani za shilingi ishirini (20), mia mbili (200), mia tano (500), elfu moja (1000), elfu mbili (2000), elfu tano (5000) na elfu kumi (10000) kwa matoleo ya mwaka 1985 hadi mwaka 2003, na noti ya shilingi mia tano (500) iliyotolewa mwaka 2010 zenye sifa zilizoainishwa kwenye Tangazo la Serikali Na. 858 la tarehe 11 Oktoba 2024.

Zoezi la ubadilishwaji linatarajiwa kuanza tarehe 06 Januari 2025 hadi tarehe 05 Aprili 2025 kupitia Ofisi zote za Benki Kuu na benki zote za biashara kwa kupatiwa malipo yenye thamani sawasawa na kiasi kitakachowasilishwa. Aidha, matumizi ya noti hizo yatafikia ukomo wa kuwa fedha halali za Tanzania kuanzia tarehe 06 Aprili, 2025. Baada ya tarehe hiyo, mtu yeyote au taasisi yoyote inayomiliki fedha hizo haitaruhusiwa kuzitumia katika kufanya malipo popote duniani; na benki zote hazitaruhusiwa kulipa wala kupokea amana au maombi ya kubadilisha noti zilizoondolewa kwenye mzunguko.

Hivyo, Benki Kuu inatoa rai kwa wananchi wote wenye akiba ya noti hizo za zamani, kuzibadilisha au kuziweka amana kwenye benki yoyote ndani ya kipindi kilichotolewa.

Kwa taarifa/msaada zaidi tafadhali wasiliana na: Kurugenzi ya Usimamizi wa Sarafu, Benki Kuu ya Tanzania, 2 Mtaa wa Mirambo, S.L.P 2939 Dar es Salaam; au kwa Barua Pepe: info@bot.go.tz au botcommunications@bot.go.tz; au kwa simu +255745 802 007.

Emmanuel M. Tutuba.

GAVANA

FB_IMG_17299550031872392.jpg
 
Wanataka uziweke kwenye mfumo hakuna kubadilishana hela kwa hela,hii itakuwa ngumu sana kwa watz wengi maana wengine hatuna inshu za kutufanya tupeleke hela huko bank
wanazibadilisha wanakupa hela ya sasa watathaminisha sawa na thamani ya sasa. au la unaweza kuziweka kama amana kwenye mabenki kwa thamani zawa na ya sasa.
 
Back
Top Bottom