Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,385
- 121,017
Wanabodi
Merry Chritmas
Mjadala wa tuhuma za rushwa unaovurumishwa na Tundu Lissu, umezidi kushika kasi, tuhuma zilianzia majukwaani, zikahamia mitandaoni sasa zinaendelea kule Club House, spaces na X- tweeter.
Hivyo najitolea kumtetea Mbowe, Chadema, wengine wote wanaotuhumiwa kwa tuhuma za uongo na uzushi wa rushwa ya mtu na mama mtu.
Declaration of interest, mimi ni mpinzani mkubwa wa usultani wa uongozi kwenye vyama vya siasa, niliwahi kumuuliza Mfalme Cheyo wa UDP, Kayafa Lipumba wa CUF na hivyo siungi mkono Sultan Mbowe kugombea tena uenyekiti wa Chadema.
Hakuna ubaya wowote kwa mtu yoyote, chama chochote au taasisi yoyote kupokea fedha zozote kutoka kwa mtu yoyote au taasisi yoyote, sio kila fedha ni rushwa!.
Ili fedha zozote, kitu chochote au hata huduma yoyote, ili iwe ni rushwa, inategemea na madhumuni ya fedha hizo, kitu hicho au huduma hiyo, ndio itaamua kama ni rushwa, au ni charty tuu au ni takrima.
Chedema imewahi kupokea mamilioni ya mfanyabiashara Jaffary Sabodo, kwa madhumuni ya kujenga ofisi za makao makuu, fedha ilipokelewa yote, hakuna hata tofali au mfuko wa sementi ulinunuliwa, fedha yote na yote ilitafunwa, na hakuna tuhuma zozote za fedha hizo kuitwa rushwa kwasababu hizo ni fedha za charity.
Mbowe akiwa gerezani Segerea kwenye ile kesi, Chadema ilikuwa na hali mbaya sana kiuchumi, ilikuwa hoi bin taaban!, haikiweza hata kulipa watumishi wala kuendesha kikao cha Baraza Kuu.
Mbowe baada tuu ya kuachiwa, breki ya kwanza ni kwenda Ikulu kumshukuru Rais Samia kumsamehe na kumuachia, ila pia alilia shida, japo haikusemwa popote, lakini mara ghafla Chadema ikafufuka, mara ghafla wakapata pesa kuitisha Baraza Kuu, mara ghafla wakafanya ziara za nje ya nchi, ndipo yakaja maridhiano. Mbowe na Chadema walipokea fedha, hazikusemwa ila sio rushwa. Hakuna ubaya wowote Mbowe na Chadema kupokea fedha zozote kutoka popote. Hata CCM inapokea mafedha kibao kutoka kwa wafadhili mbali mbali, hadi nchi inapokea fedha kibao za wafadhili na sio rushwa!, sasa nongwa ya nini Mbowe au Chadema kupokea fedha za mtu na mama mtu?.
Kitu muhimu ni kufuatwa kwa sheria, taratibu na kanuni za fedha ikiwemo ku declare any monies received.
Siipendi kabisa hii Tabia ya Lissu kutaka kujihalalisha kwa kutumia uongo na uzushi wa rushwa, Lissu ajihalalishe kwa kuonyesha mapungufu ya Mbowe kuonyesha kuwa hana uwezo wa kufanya a,b na c na yeye anao uwwzo huo, ili kuwapa wajumbe sababu ya kutomchagua Mbowe kwa kupungukiwa uwezo na sio kumjengea chuki kwa kumzushia tuhuma za uongo za rushwa.
Lissu achaguliwe kwa kuonyesha uwezo sio kwa kuwazushia tuhuma wengine!.
Merry Christmas
Paskali