Namtafuta Godfrey Mliondoko, ni Mpare wa Kilimanjaro

New Nytemare

JF-Expert Member
Dec 15, 2011
3,332
2,484
Hbl za leo ndugu zanguni. Mimi naitwa SIPHAELY MGENI naishi Songea naomba msaada wenu wadau. Namtafu mtu mmoja anaitwa GODFREY MLINDOKO samahani Kama nitakwaza.

Huyu ndg alimpa ujauzito dadangu alikuwa anaitwa NIWA NDINGWI wakati huo dadangu alikuwa anafanya kazi ya uhouse girl DAR mtaa wa buguluni ilikuwa mwaka 1997 . Akaludi nyumbani NJOMBE,Lupembe.

Akajifungua mtoto wa like, bahatu mbaya akafariki mwaka 98 na kumuacha mtoto akiwa na umri wa miezi 7 tuu.yeye ndiye aliye alie tuelekeza jina la baba wa mtoto ambalo nimetaja hapo juu.

NA sasa hivi huyu mtoto yupo kidato cha 5 namsomesha Mimi. Pia huyo ndg Ni mpare wa huko kilimanjaro Kama sijakosea. Kwa anayemfahamu atusaidie hatuna jambo baya,lengo mtoto amfahamu baba yake.

Kwa ndugu zake,au yeye mwenyewe, au anaemfahamu anaweza kuwasiliana na Mimi kwa 0755212938,0717705614,0684812938.

Nisaidieni kutuma magroup mengine.

Asnte ndg zanguni MUNGU awabariki.
 
Poleni sana kwa mkasa huu mzito.

Na pia nakupa hongera/pongezi nyingi kwa kuwa bega kwa bega na mwanao (mtoto wa Marehemu wa dada ako).

Kwa kweli inahitaji moyo na upendo wa hali ya juu, kuweza kufanya ambacho unakifanya mpaka mtoto wa Marehemu Dada ako kuweza kufika kidato cha tano.

Ubarikiwe
 
Hongera kwa malezi naamin Mwenyezi Mungu atakulipa.
 
Nadhani ni Godfrey Mrindoko..........na Niwa (RIP).....alikuwa kikazi Buguruni ndio akarudi nyumbani Ludewa......
ngoja tu forward kwenye magroup mengine.........lazima ujumbe utamfikia.......
 
Moshi kuna mtu anaitwa mrindoko. Ana mabasi yameandikwa hilo jina. Uliza stand kuu ya mabasi moshi. Anaweza kukusaidia
 
Hongera kwa wema huo ni vyema umetumia busara hii...ngoja tuisambaze hii bila shaka utampata..Utufahamishe pia ukifanikiwa ili tuache kuulizia....pole na hongera Mungu awasaidie.
 
Hongera kwa malezi ya mtoto wa dada yako,pia hongera kwa huyo mtoto kuwa na roho ya imani ya kumtafuta baba yake ili amuone, Mleta mada labda nikuulize swali ambalo litasaidia kutoa mwanga wa kumtafuta huyo Mrindoko,

Mkuu toka mwaka 1997 ulikuwa unamtafuta huyo baba wa mtoto au ndio umeamua kumtafuta mwaka huu tu wa 2016 ?
 
Huyo binti ana ndugu zake wengi tu,mmoja wapo ni aliye kuwa katibu mkuu wa maji Bwana Bashiri Mrindoko,na mwingine ni ofisa wa manunuzi mamlaka ya maji Arusha nadhani ukiwapata watu hao utakuwa umewapata wakwe zako
 
Nadhani ni Godfrey Mrindoko..........na Niwa (RIP).....alikuwa kikazi Buguruni ndio akarudi nyumbani Ludewa......
ngoja tu forward kwenye magroup mengine.........lazima ujumbe utamfikia.......

Hongera, mmejitahidi aisee, nipo New Delhi, na mpaka sasa nimeshaipokea hii sms ktk magroup ma3 tofauti! safi sana
 
Tuifanye hii kipelelez said,turud dar mwaka 97 Dada alipokuwa akihudumu twende na picha ya Dada tuwaonyeshe wauza maduka picha ya dada lengo likiwa ni kuwarahisishia kuvuta kumbukumbu ya dada,tuwaulize kama wanamkumbuka kaka alokuwa akionana na dada hapo dukan kwao,kurahisisha kaz yetu tuwaambie dada alishakufa ili simanz iwajae watusaidie kuvuta pocha ya kitambo tuwamslizie na lengo mtoto anataka kumfahamu mshua wake.Zoezi ni rahisi nipm bugurun ni kubwa kama ujui dada ako alikuwa bugurun sehemu gan inabid tumwage vijana bugurun nzima kuzuru kila nyumba kumtafuta mwajir wa dada mwaka 97 kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…