Namna ya kutoa nta masikioni

BILGERT

JF-Expert Member
Feb 27, 2015
6,534
11,001
Habarini za jioni wanajukwaa,jana asubuh baada ya kuamka nilihisi sikio langu la kulia haliko sawa,yaani lilikuwa na mawimbi makali halaf likiwa zito,na hvo kunifanya nisisikie vizur,lakin lilikuwa halina maumivu yoyote.Hali hyo imedumu mpaka hivi leo asubuh nilipochukua uamuzi wa kwenda hospitali.Daktari kanieleza kuwa sikio langu liko vizur ila napaswa kununua Boric Acid,ambapo inabid niweke matone mawili sikioni kila baada ya masaa nane,,hvo ilinibidi nianze kuweka ile saa nane mchana.lakini cjaona unafuu wowote.Daktar aliniambia kuwa kama hyo nta haitayeyuka zaid ya ck mbili itabid nirud kwake.

naombeni ushauri wenu wadau,naamini humu kuna madaktar na wtu wa kada za afya pia.nifanyeje? maana kiukweli nimekosa aman na hii hali ilonipata.natanguliza shukrani
 

Dr wako keshakushauri tayari..kakwambia tiba aliyokupa isipofaa baada ya siku mbili urudi kwake..nafikiri rudi kwanza uone dawa atakayokubadilishia kama itakusaidia ama vp...kumbuka ndio kwanza umeanza tiba na huo ugonjwa sidhani kama umekua sugu kiasi cha kukukatisha tamaa..vuta subira umalize tiba ya dr wako
 
Mimi sio Dr ila nilishapatwa na tatizo hilo.

Nilikuwa sisikii vizuri, nikaenda kwa Dr pale Kinondoni hospital nikapewa hiyo boric acid haikusaidia, nikarudi Dr akanambia niende kwa specialist wa masikio akanielekeza kwenda ekenywa iko magomeni mwembechai, nikaenda Dr akaniingiza kichuma, katoa kibonge cha uchafu mara mbili sikio likazibuka, nilishangaa sana!!

Zamani nilikuwa na mtindo wa kujichokoa sikio kila siku, kwa kipindi hicho niliacha. Nilivotolewa uchafu ule nikaanza tena kupitisha vile vistiki vya masikio kila siku.

Nadhani ni muhimu sana kutoa nta kila mara, usipofanya hivyo unajaa na kufanya kuziba sikio.

Nenda ekenywa, militia 40, 000 nikarudi mzima.
 
Pia nina tatizo kama
Habari zenu wana jukwaa. Mimi pia nmepatwa na tatizo kama hili. Ninaomba alie post hii aniambie al .
..
Haa.

Habari zenu jamani. Mimi pia nimepatwa na tatizo k

.

Habarini zenu jamani. Mimi pia nimepatwa na tatizo kama hili. Ninaomba ali .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…