Namna ya kujitetea katika makosa ya jinai kulingana na mazingira ya kesi

Mr George Francis

JF-Expert Member
Jun 27, 2022
234
366
UTETEZI WA KIJINAI
DEFENSES IN CRIMINAL CASES.

Karibu tujifunze namna ya kujitetea katika makosa ya jinai kulingana na mazingira ya kesi husika kwa kusoma makala hii.

Imeadaliwa na
Mr. George Francis.

Email: mr.georgefrancis21@gmail.com

Zifuatazo ni baadhi ya aina za utetezi wa makosa ya jinai.
1. UMRI MDOGO (Immature age)
Mtuhumiwa aliye chini ya umri wa miaka kumi hawezikuwajibika kijinai na iwapo ana miaka 12Mahakama haitamhukumu kuwa ametenda kosa hadiitakapohakikisha kuwa wakati wa kutenda au kuacha kutenda kitendo hicho alikuwa anajua kuwa hapaswi kutenda au kuacha kutenda, hivyo ametenda kosa hilo kwa kukusudia au alikuwa na nia ovu.

Mtoto wa kiume wa
miaka chini ya 12 anahesabika kutokuwa na uwezo wakutenda kosa la kujamiiana au kufanya tendo la ndoa kama vile kosa la ubakaji.
rejea kusoma kifungu cha 15 cha sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai Sura ya 16.

2. ULEVI WA KUPINDUKIA. (Intoxication)
Ulevi sio utetezi katika makosa ya jinai lakinimtuhumiwa akiweza kuthibitisha kwamba wakati anatenda kosa la kijinai alikuwa amelewa kiasi cha kutofahamunini alikuwa anatenda, inaweza ikawa sababu yautetezi.

Mtuhumiwa anatakiwa kuthibitisha mambo tafuatayo ili utetezi wake uweze kukubalika.

(a) Hali ya kulewa huko kulisababishwa bila ya hiari yake kwa makusudi au kwa kitendo cha uzembe wa mtu mwingine.

(b) Ulevi huo ulimpelekea kuwa matatizo ya akili kwa muda au vinginevyo wakati anatenda au kuacha kutenda kosa hilo. Kwa kifupi ni kwamba hakuwa anafahamu anachokifanya kwa wakati huo.

Mtuhumiwa akiweza kuthibitisha utetezi huu na kama kesi itaangukia chini ya aya (a) hapo juu basi anaweza kufutiwa kesi au kama kesi ikiangukia kwenye aya (b) hapo juu basi masharti ya Sheria ya Makosa ya jinai pamoja na Sheria ya Mienendo ya Makosa ya Jinai kuhusu wendawazimu yatatumika.
rejea kusoma kifungu cha 14 cha sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai Sura ya 16.

Telegram: TANZANIA LAWYERS FORUM 🎓

3. UPUNGUANI AU UKICHAA. ( Insanity)
Mtuhumiwa anaweza kutumia utetezi huu pale ambapo atakuwa ametenda kosa la jinai lakini hakuwa anafahamu alichokuwa anakifanya kwa wakati huo kwasababu ya ukichaa auupunguani. Hivyo, alitenda kosahilo bila ya kukusudia.

Mtuhumiwa anatakiwa kuthibitisha kwamba wakati anatenda kosa hilo alikuwa katika hali ya ugonjwa wowote ambao uliathiri akili yake kiasi kwamba

(a) Hakuweza kujua kitu anachokitenda.
(b) Hakuweza kutambua kwamba hapaswi kutenda au kufanya
jambo alilolitenda au
(c) hakuwa na uwezo wa kujizuia kitenda kosa hilo.

Lakini, elewa kwamba kama ungonjwa huo ulioathiri akili yake haukumletea mojawapo ya madhara haya tajwa hapo juu basi mtuhumiwa atachukuliwa kuwa ametenda kosa la jinai na hivyo atawajibika kwa mujibu wa sheria.

Kwahiyo ni lazima mtuhumiwa aweze kuthibitisha utetezi huu kwasababu sheria inamchukulia kila mtu kuwa na akili timamu wakati wote mpaka pale itakapothibitishwa vinginevyo.
rejea kusoma kifungu 13 & 12 vya sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai Sura ya 16.

4. KUDAI HAKI KWA NIA NJEMA (Bona fide claim of rights)
Mtuhumiwa anaweza kujitetea kuwa alitenda kosa lajinai lakini alikuwa na nia njema.

Utetezi huu unatumika hasa pale mtuhumiwa anapokuwa ametenda kosa linalohusiana na mali.

Hii ni pale ambapo kitendo kilichofanywa au kilichoachwa kufanywa na mtuhumiwa huyo kinahusiana na mali hiyo na alifanya hivyo kwa nia njema ya kudai haki na hakuwa na nia ya kuiba.
rejea kifungu cha 9 cha sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai, Sura ya 16.

5. SHURUTISHO (Compulsion)

Katika utetezi wa kijinai, Mtuhumiwa anaweza kujitetea kuwa alishurutishwa kutenda kosa hilo la kijinai na mkosaji mwenzake kwa kutishiwa kuuawa papohapo au kumdhuru kimwili endapo atakataa kutenda kosa hilo aliloamriwa kulitenda.

Hivyo, mtuhumiwa anatakiwa kuthibitisha kwamba
(a) Haikuwa hiari yake yeye kutenda kosa hilo bali ameshurutishwa na mtu mwingine kutenda kosa hilo.

(b) Ametenda kosa hilo kwasababu katika kipindi chote ambacho kosa hilo limekuwa likitendeka alikuwa chini ya kitisho au hatari.

(c) Hatari hiyo ni lazima iwe ya kuawa au kudhuriwa mwili endapo angekataa kutenda kosa hilo.
Mfano: "mtuhumiwa aliambiwa ni lazima uibe na kama hutaki kuiba tutakuua"

Katika mazingira kama haya, mtuhumiwa anaweza kujitetea kwamba alishurutishwa kutenda kosa.

LAKINI, Vitisho vya kuumizwa hapo baadae hautachukuliwa kuwa ni utetezi wa kosa lolote, isipokuwa endapo mtuhumiwa huyo ni mtoto hivyo kushindwa kujinasua katika vitisho au hatari hiyo.

Lakini, unapaswa kutambua kwamba utetezi huu haukubaliki katika mambo yafuatayo.
(a) Haukubaliki katika kesi za mauaji. Hivyo, mtuhumiwa hawezi kujitetea kwamba alimuua mtu fulani kwasababu yeye alitishiwa kuuawa au kuumizwa mwili.

(b) Utetezi hautakubalika endapo mtuhumiwa alikuwa na uwezo au nafasi ya kujinusuru.

(c) Utetezi haukubaliki endapo mtuhumiwa alijiunga katika kikundi cha kufanya uhalifu au ugaidi na hivyo kulazimishwa kutenda kosa.

(d) Utetezi hautakubalika endapo kitisho au hatari hiyo haikuelekezwa kwake bali imeelekezwa kwa mtu mwingine.

[rejea kusoma Kifungu cha 17 cha sheria ya Kanuni za Makosa ya jinai sura ya 16.]

6. SHURUTISHO KUTOKA KWA MUME.

Mwanamke aliyeolewa anaweza kutumia utetezi huu katika kosa la jinai alilotenda kutokana na kushurutishwa na mumewe kutenda kosa hilo.

Mwanamke huyo anatakiwa kuthibitisha mambo yafuatayo.
(a) Ametenda kosa hilo kwa kushurutishwa lakini, hakutenda kwa hiari yake mwenyewe.

(b) Ameshurutishwa kwa kutishiwa kuuawa au kuumizwa.

(c) Ametenda kosa hilo mbele ya mumewe.

(d) Ameshurutishwa na mumewe kutenda kosa.

Mwanamke akiweza kuthibisha utetezi huu, hatawajibika kwa kosa lolote isipokuwa kwenye shtaka la;
(i) Uhaini au
(ii) Mauaji

Hivyo kama mwanamke amehusika katika kosa la kutaka kuipindua serikali au kosa la kuua, utetezi huu hautakubalika.

Lakini pia unapaswa kutambua kwamba Mahakama haitakubali utetezi huu iwapo tishio la kuuawa au kuumizwa ni la wakati ujao.

Utetezi huu unatumika kwa wanawake tu, hasa walioolewa. Hivyo haukubaliki kwa wapenzi, yaani boyfriend na girlfriend.

Sheria imempa mwanamke utetezi huu kwasababu inaaminika kwamba wanaume wana nafasi kubwa ya kuwa watawala dhidi wake zao na kuwapa amri ya kipi wafanye na kipi wasifanye.

Hivyo, kuna umuhimu mkubwa wa kuwalinda wanawake katika makosa ya kijinai wanayofanya kwa kushurutishwa na waume zao.

[rejea kusoma kifungu cha 20 cha Sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai Sura ya 16]

7. UTETEZI WA KIMAHITAJI (Necessity)
Mtuhumiwa anaweza kutumia utetezi huu endapo anakabiliwa na shtaka la kufanya kosa la jinai pale ambapo mazingira yalimlazimisha kufanya kosa hilo.

Mazingira yamemlazimisha kutenda kosa hilo ili kuepuka kusababisha madhara makubwa zaidi au kosa kubwa zaidi ya alilotenda.

Kimsingi utetezi huu haupo katika sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai au sheria za Tanzania kwa ujumla lakini ni utetezi unaotambulika na kukubalika nchini kwa kufuata sheria za Uingereza ( common law) kupitia kifungu cha 2 cha Sheria za Mahakama ( Judicature and Application of Laws Act) ambacho kimeruhusu kutumika kwa sheria hizo nchini mnamo tarehe 22 July, 1920.

Utetezi huu unakubalika hasa pale mtu anapokuwa katika hatari. Ili mtuhumiwa aweze kufanikiwa katika utetezi huu anatakiwa kuzingatia mambo yafuayayo.
(a) Lazima pawepo na hatari ambayo ingesababisha madhara makubwa kuliko madhara ya kosa alilotenda.
(b) Hakuwa na mbadala au namna ya kuweza kuepuka kutenda kosa hilo.
(c) Kitendo au kosa alilotenda halina madhara makubwa zaidi ya lile ambalo lingetokea kama angeacha litokee.

Katika utetezi huu, inaaminika kwamba mtuhumiwa ametenda kosa ambalo mtu yoyote mwenye ufahamu wa kawaida angetenda kama angekuwa katika mazingira yaliyomkuta mtuhumiwa.

Asili ya utetezi huu ni Uingereza hasa katika shauri la JAMHURI dhidi ya DUDLEY na STEPHENS (1884).
Katika kesi hii watuhumiwa hao wawili na kijana mdogo wa miaka 17 walikuwa safarini katika meli ambako walikwama baharini kwa siku 18 na walikosa chakula na maji kwa siku 7 baada ha kuishiwa.

Wawili hao Dudley na Stephens walishauriana na waliamua kumuua na kumla yule kijana mdogo ambaye alionekana kudhoofu sana kiasi cha kukaribia kupoteza uhai. Hii iliwasidia kuokoa maisha yao kwa siku kadhaa walizokuwa huko majini kabla ya kuokolewa na kufikishwa Mahakamani.

Walifikishwa Mahakamani kwa kosa la mauaji ya yule kijana aliyejulikana kwa jina la Richard Parker. Katika utetezi wao wakasema kwamba ilikuwa ni lazima kwa wao kumuua yule kijana ili kuokoa maisha yao.

Lakini, Mahakama ilikataa utetezi huu na kuwahukumu kunyongwa kabla baadae kupunguziwa hukumu na kufungwa miezi sita (6) gerezani.

Utetezi huu wa kimahitaji haupaswi kutumika kwa mtu aliyepoteza uhai wa mtu mwingine kwaajili ya kuokoa maisha yake. Thamani ya mtu haipimwi kwa kuondoa uhai wa mtu mwingine.

Jambo la msingi katika utetezi huu ni kuangalia kama mazingira yamemlazimisha mtuhumiwa kutenda kosa ambalo madhara yake ni madogo ukilinganisha na madhara ambayo yangetokea endapo hasingetenda kosa hilo, hivyo hakuwa na namna nyingine.

Mfano. Binti ametolewa ujauzito na daktari ili kuokoa maisha yake ambayo yalikuwa hatarini kupotea endapo angekuja kujifungua, kutokana hali yake kiafya kufuatia vipimo vya kitabibu. Japo kutoa mimba ni kosa, lakini katika mazingira kama haya utetezi huu unaweza ukakubalika na mtuhumiwa kuachiwa huru.

8. DHANIA ISIYO KWELI ( Mistake of facts )

Utetezi huu unatumika kwa Mtuhimiwa ambaye ametenda kosa la jinai kwa kukosea uweli.
Mtuhumiwa anatakiwa kuthibisha mambo yafuatayo:
(a) Ametenda kosa hilo pasipo kudhamilia.
(b) Amekosea ukweli, kwa kuamini kuwepo kwa kitu fulani tofauti na jinsi uhalisia ulivyo.
(c) Alikuwa na dhamira njema na sio kutenda kosa la jinai kama ilivyokuwa hatimaye.

Mfano; kesi ya JAMHURI dhidi ya SULTAN MAGINGA (1969) HCD,
Katika kesi hii Sultan Maginga alishtakiwa kwa kosa la mauaji.
-Tunaambiwa kuwa siku moja wakati wa usiku Maginga alienda shambani kulinda shamba lake dhidi ya nguruwe poli waliokuwa wakiharibu mazao hapo shambani.

-Alipofika shambani aliona majani ya mpunga yanatikisika kiashiria cha kuwepo hao nguruwe pori maeneo yale lakini hakuwa na uhakika ni nini kilikuwa maeneo yale.
-Akajaribu kuita kujua kama ni binadamu basi ajitokeze lakini ikawa kimya.
-Ghafla aliona kama vimvuli vinakimbia uelekeo tofauti, aliwasha tochi yake lakini haikuwa na mwanga wa kutosha kumwezesha kuona mbali ndipo aliamua kurusha mkuki na kumchoma mmoja kati ya wale waliokuwa wanakimbia.

-Alipofika karibu ndipo akagundua kuwa alichokirushia mkuki hakuwa nguruwe pori bali ni binadamu ambao inasemekana walikuwa ni watu waliouwa wakifanya mapenzi nyakati zile za usiku katika shamba hilo la mpunga.

-Hatimaye Maginga alikamatwa na kufikishwa mahamani kwa kosa la mauaji na ndipo aliopotumia utetezi huu wa dhania isiyo kweli ( mistake of facts) na utetezi wake ulikubalika.

Hivyo, ukiweza kujitetea kwa kutumia utetezi huu na ukaweza kuthibitisha vigezo vinavyotakiwa, Mahakama inaweza kukuachia huru au kuamua vinginevyo kwa mujibu wa sheria.

rejea kusoma kifungu cha 11 cha sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Makosa ya Jinai

9. KINGA YA KISHERIA (Judicial Immunity)

Huu ni utetezi unaotumika kwa maafisa wa Mahakama kama vile Jaji, Hakimu au afisa msajili wa Mahakama, kwa makosa wanayoweza kufanya katika kutekeleza majukumu yao ya kazi.

Lengo la utetezi huu ni kuhakikisha uhuru wa mahakama katika utoaji wa haki au maamuzi. Hii inawasaidia kutekeleza majukumu yao kwa uhuru na bila hofu ya kuingia hatia ya kosa la kijinai.

Hivyo, afisa wa mahakama anaweza kutumia utetezi huu kwa makosa aliyofanya pindi anatekeleza majukumu yake. Hivyo ametenda kosa hilo kwa nia njema ili kutekeleza majukumu ya kazi yake ya Kimahakama.
(rejea kusoma kifungu cha 16 cha sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Makosa ya Jinai sura ya 16)

10. KUTOADHIBIWA MARA MBILI (Double Jeopardy) Mtuhumiwa anaweza kutumia utetezi huu kwa kosa ambalo tiari Mahakama imelitolea maamuzi.

Maamuzi hayo yanaweza kuwa mtuhumiwa amekwisha adhibiwa au aliachiwa huru.

Hivyo, sheria inasema kwamba, mtu hawezi kuadhibiwa mara mbili kwa kosa lile lile. Hii ina lengo la kufanya kesi ziweze kufikia mwisho na kuepusha usumbufu kwa watuhumiwa au Mahakama kwa ujumla.

(rejea kusoma kifungu cha 21 cha sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Makosa ya Jinai sura ya 16)

11. KULINDA MTU AU MALI
(Self Defense/ Defense of Person or Property)

Mtuhumiwa anaweza kutumia utetezi huu kwa kosa la jinai la kuua au kujeruhi alilofanya wakati anatimiza haki yake ya
(a)Kujilinda au kujitetea katika shambulio au uovu wowote.

(b)Kumlinda mtu mwingine dhidi ya shambulio au uovu wowote.

(c)Kulinda mali yake au mali ya mtu mwingine isiibiwe au kuharibiwa.

Utetezi huu unakubaliwa nw Mahakama inaweza kumwondolea hatia ya kosa hilo la jinai.

Katika kujilinda, kumlinda mtu mwingine au mali, mtuhumiwa anatakiwa awe ametumia nguvu kiasi zinazostahili. Matumizi ya nguvu kupita kiasi yatamfanya mtuhumiwa huyo kuwajibika kwa mujibu wa sheria.

Mfano, Mtu akikushambulia kwa kukupiga ngumi, sio sahihi kujibu mashambulizi kwa kutumia panga kwani kufanya hivyo ni matumizi ya nguvu kupita kiasi.

Hivyo, ni vyema kuwa makini katika nguvu unazozitumia katika kujitetea. Lakini, sheria inasema, kama ukisababisha kifo kutokana na matumizi ya nguvu kupita kupita kiasi utahukumiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia.

Katika utetezi huu, Mtuhumiwa anatakiwa kuthibisha mambo kadhaa kama matumizi yake ya nguvu yamesababisha kifo au madhara makubwa kwa mtu mwingine. Hivyo, ilikuwa ni lazima kutumia nguvu ili kulinda maisha yake, maisha ya mtu mwingine au mali. Mfano ni katika mambo yafuatayo.
-Hatari ya kupoteza maisha yake kama hasingetumia nguvu kujitetea

-Hatari ya kupata madhara makubwa/kuumizwa

-Hatari ya kubakwa au kufanyiwa tendo la ndoa kinyume na maumbile

-Kulikuwa na nia ya kutekwa nyara au kutoroshwa

-Kuvunja au kuingia ndani au unyang'anyi au kosa lolote la kijinai lenye kuhatarisha maisha au mali.

(_rejea kusoma kifungu cha 18, 18A, 18B na 18C cha Kanuni ya Adhabu ya Makosa ya Jinai, sura ya 16)

12. KUKASILISHWA KUPITA KIASI (Provocation)

Huu ni utetezi ambao mtuhumiwa wa kosa la jinai kwa kitendo kama vile kuua au kujeruhi anaweza kuutumia.

Ili Mtuhumiwa aweze kukubaliwa utetezi wake kuwa alikuwa amechukizwa kupita kiasi lazima athibitishe mambo yafuatayo.
(a) Alitendewa tendo ovu na la kumdhalilisha.

(b) Kitendo alichofanyiwa kililenga kumdhalilisha yeye binafsi au mtu yoyote mwenye uhusiano nae wa karibu.

(c) Kitendo cha kumdhalilisha kilikuwa ni cha hali ya juu kiasi cha kumfanya hashindwe kutuliza hasira zake au ashindwe kujitawala.

(d) Ametenda kosa hilo la kijinai papohapo na ni ghafla kiasi cha kukosa muda wa kutuliza hasira zake.

Mtuhumiwa atakayethibisha kuwa ametenda kosa la mauaji kutokana na kukasirishwa kupita kiasi atahukumiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia.

(rejea kusoma kifungu cha 201 na 202 cha Kanuni ya Adhabu ya Makosa ya Jinai ili kuelewa zaidi maana ya utetezi huu.)

13. KUTOKUWEPO ENEO LA TUKIO (Defense of alibi)

Huu ni utetezi unaotumika pale ambapo Mtuhumiwa hakuwepo eneo la tukio au eneo ambalo kosa hilo la kijinai limetendeka.
Yaani Mtuhumiwa alikuwa sehemu nyingine hivyo isingewezekana kwa muda huo kuwepo eneo ambalo kosa hilo limetendeka.

Mfano, umeshitakiwa kwa kosa la wizi lililofanyika Dodoma majira ya saa moja asubuhi, Mtuhumiwa anaweza kutumia utetezi huu kuonesha kuwa alikuwa Morogoro pindi tukio hilo limetendeka, hivyo sio rahisi mtu uwe Morogoro arafu wakati huohuo uibe mali ya mtu iliyopo Dodoma.

Lakini, kauli ya kusema tu "sikuwepo" haitoshi bali ni lazima Mtuhumiwa alete ushahidi au mashahidi wa kuweza kuthibitisha kwama walimuona au alikuwa nao huko anaposema kwamba alikuwepo siku hiyo ambayo kosa limetendeka.

Kwa kuhitimisha mada hii ya utetezi wa kijinai, mtuhumiwa anayo haki ta kusikilizwa na kujitetea Mahakamani kwa kosa lolote la kijinai.

Kukubalika au kukataliwa kwa utetezi wake inategemea na namna mtuhukiwa atakavyoweza kuthibitisha utetezi husika kulingana na kosa husika.
(ongeza maalifa kwa kusoma kifungu cha 194 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai)

Ahsante wa kuwa pamoja nami tangu tulipoanza mada hii ya UTETEZI WA KESI ZA KIJINAI hadi hapa tulipoishia. Nawakaribisha kufuatilia mada zijazo.

Mwisho

Ahsante na hongera kwa kusoma hii ndefu kuhusu utetezi wa makosa ya jinai. Ubarikiwe sana msomaji wangu.

It's prepared by
A Lawyer and LifeCoach
Mr. George Francis
Contacts: 0713736006
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com
 
Umeniongezea madin
Mistake of facts
Upunguani
Kukasirshwa
Kutend kosa dogo zd ya mazngr
Kujilind na kulind Mali

HV KAMA NIMETENDA KOSA NDANI YA KAZI (MAKOSA YA KIUTENDAJI ambayo yamepelekea hasara kwa kampuny au ofis yake.... wakat nauguz mtu wa karbu sana hii haiwez kuw utetez kam mwajir amekushtak mahakam
 
UTETEZI WA KIJINAI
DEFENSES IN CRIMINAL CASES.

Karibu tujifunze namna ya kujitetea katika makosa ya jinai kulingana na mazingira ya kesi husika kwa kusoma makala hii.

Imeadaliwa na
Mr. George Francis.

Email: mr.georgefrancis21@gmail.com

Zifuatazo ni baadhi ya aina za utetezi wa makosa ya jinai.
1. UMRI MDOGO (Immature age)
Mtuhumiwa aliye chini ya umri wa miaka kumi hawezikuwajibika kijinai na iwapo ana miaka 12Mahakama haitamhukumu kuwa ametenda kosa hadiitakapohakikisha kuwa wakati wa kutenda au kuacha kutenda kitendo hicho alikuwa anajua kuwa hapaswi kutenda au kuacha kutenda, hivyo ametenda kosa hilo kwa kukusudia au alikuwa na nia ovu.

Mtoto wa kiume wa
miaka chini ya 12 anahesabika kutokuwa na uwezo wakutenda kosa la kujamiiana au kufanya tendo la ndoa kama vile kosa la ubakaji.
rejea kusoma kifungu cha 15 cha sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai Sura ya 16.

2. ULEVI WA KUPINDUKIA. (Intoxication)
Ulevi sio utetezi katika makosa ya jinai lakinimtuhumiwa akiweza kuthibitisha kwamba wakati anatenda kosa la kijinai alikuwa amelewa kiasi cha kutofahamunini alikuwa anatenda, inaweza ikawa sababu yautetezi.

Mtuhumiwa anatakiwa kuthibitisha mambo tafuatayo ili utetezi wake uweze kukubalika.

(a) Hali ya kulewa huko kulisababishwa bila ya hiari yake kwa makusudi au kwa kitendo cha uzembe wa mtu mwingine.

(b) Ulevi huo ulimpelekea kuwa matatizo ya akili kwa muda au vinginevyo wakati anatenda au kuacha kutenda kosa hilo. Kwa kifupi ni kwamba hakuwa anafahamu anachokifanya kwa wakati huo.

Mtuhumiwa akiweza kuthibitisha utetezi huu na kama kesi itaangukia chini ya aya (a) hapo juu basi anaweza kufutiwa kesi au kama kesi ikiangukia kwenye aya (b) hapo juu basi masharti ya Sheria ya Makosa ya jinai pamoja na Sheria ya Mienendo ya Makosa ya Jinai kuhusu wendawazimu yatatumika.
rejea kusoma kifungu cha 14 cha sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai Sura ya 16.

Telegram: TANZANIA LAWYERS FORUM

3. UPUNGUANI AU UKICHAA. ( Insanity)
Mtuhumiwa anaweza kutumia utetezi huu pale ambapo atakuwa ametenda kosa la jinai lakini hakuwa anafahamu alichokuwa anakifanya kwa wakati huo kwasababu ya ukichaa auupunguani. Hivyo, alitenda kosahilo bila ya kukusudia.

Mtuhumiwa anatakiwa kuthibitisha kwamba wakati anatenda kosa hilo alikuwa katika hali ya ugonjwa wowote ambao uliathiri akili yake kiasi kwamba

(a) Hakuweza kujua kitu anachokitenda.
(b) Hakuweza kutambua kwamba hapaswi kutenda au kufanya
jambo alilolitenda au
(c) hakuwa na uwezo wa kujizuia kitenda kosa hilo.

Lakini, elewa kwamba kama ungonjwa huo ulioathiri akili yake haukumletea mojawapo ya madhara haya tajwa hapo juu basi mtuhumiwa atachukuliwa kuwa ametenda kosa la jinai na hivyo atawajibika kwa mujibu wa sheria.

Kwahiyo ni lazima mtuhumiwa aweze kuthibitisha utetezi huu kwasababu sheria inamchukulia kila mtu kuwa na akili timamu wakati wote mpaka pale itakapothibitishwa vinginevyo.
rejea kusoma kifungu 13 & 12 vya sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai Sura ya 16.

4. KUDAI HAKI KWA NIA NJEMA (Bona fide claim of rights)
Mtuhumiwa anaweza kujitetea kuwa alitenda kosa lajinai lakini alikuwa na nia njema.

Utetezi huu unatumika hasa pale mtuhumiwa anapokuwa ametenda kosa linalohusiana na mali.

Hii ni pale ambapo kitendo kilichofanywa au kilichoachwa kufanywa na mtuhumiwa huyo kinahusiana na mali hiyo na alifanya hivyo kwa nia njema ya kudai haki na hakuwa na nia ya kuiba.
rejea kifungu cha 9 cha sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai, Sura ya 16.

5. SHURUTISHO (Compulsion)

Katika utetezi wa kijinai, Mtuhumiwa anaweza kujitetea kuwa alishurutishwa kutenda kosa hilo la kijinai na mkosaji mwenzake kwa kutishiwa kuuawa papohapo au kumdhuru kimwili endapo atakataa kutenda kosa hilo aliloamriwa kulitenda.

Hivyo, mtuhumiwa anatakiwa kuthibitisha kwamba
(a) Haikuwa hiari yake yeye kutenda kosa hilo bali ameshurutishwa na mtu mwingine kutenda kosa hilo.

(b) Ametenda kosa hilo kwasababu katika kipindi chote ambacho kosa hilo limekuwa likitendeka alikuwa chini ya kitisho au hatari.

(c) Hatari hiyo ni lazima iwe ya kuawa au kudhuriwa mwili endapo angekataa kutenda kosa hilo.
Mfano: "mtuhumiwa aliambiwa ni lazima uibe na kama hutaki kuiba tutakuua"

Katika mazingira kama haya, mtuhumiwa anaweza kujitetea kwamba alishurutishwa kutenda kosa.

LAKINI, Vitisho vya kuumizwa hapo baadae hautachukuliwa kuwa ni utetezi wa kosa lolote, isipokuwa endapo mtuhumiwa huyo ni mtoto hivyo kushindwa kujinasua katika vitisho au hatari hiyo.

Lakini, unapaswa kutambua kwamba utetezi huu haukubaliki katika mambo yafuatayo.
(a) Haukubaliki katika kesi za mauaji. Hivyo, mtuhumiwa hawezi kujitetea kwamba alimuua mtu fulani kwasababu yeye alitishiwa kuuawa au kuumizwa mwili.

(b) Utetezi hautakubalika endapo mtuhumiwa alikuwa na uwezo au nafasi ya kujinusuru.

(c) Utetezi haukubaliki endapo mtuhumiwa alijiunga katika kikundi cha kufanya uhalifu au ugaidi na hivyo kulazimishwa kutenda kosa.

(d) Utetezi hautakubalika endapo kitisho au hatari hiyo haikuelekezwa kwake bali imeelekezwa kwa mtu mwingine.

[rejea kusoma Kifungu cha 17 cha sheria ya Kanuni za Makosa ya jinai sura ya 16.]

6. SHURUTISHO KUTOKA KWA MUME.

Mwanamke aliyeolewa anaweza kutumia utetezi huu katika kosa la jinai alilotenda kutokana na kushurutishwa na mumewe kutenda kosa hilo.

Mwanamke huyo anatakiwa kuthibitisha mambo yafuatayo.
(a) Ametenda kosa hilo kwa kushurutishwa lakini, hakutenda kwa hiari yake mwenyewe.

(b) Ameshurutishwa kwa kutishiwa kuuawa au kuumizwa.

(c) Ametenda kosa hilo mbele ya mumewe.

(d) Ameshurutishwa na mumewe kutenda kosa.

Mwanamke akiweza kuthibisha utetezi huu, hatawajibika kwa kosa lolote isipokuwa kwenye shtaka la;
(i) Uhaini au
(ii) Mauaji

Hivyo kama mwanamke amehusika katika kosa la kutaka kuipindua serikali au kosa la kuua, utetezi huu hautakubalika.

Lakini pia unapaswa kutambua kwamba Mahakama haitakubali utetezi huu iwapo tishio la kuuawa au kuumizwa ni la wakati ujao.

Utetezi huu unatumika kwa wanawake tu, hasa walioolewa. Hivyo haukubaliki kwa wapenzi, yaani boyfriend na girlfriend.

Sheria imempa mwanamke utetezi huu kwasababu inaaminika kwamba wanaume wana nafasi kubwa ya kuwa watawala dhidi wake zao na kuwapa amri ya kipi wafanye na kipi wasifanye.

Hivyo, kuna umuhimu mkubwa wa kuwalinda wanawake katika makosa ya kijinai wanayofanya kwa kushurutishwa na waume zao.

[rejea kusoma kifungu cha 20 cha Sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai Sura ya 16]

7. UTETEZI WA KIMAHITAJI (Necessity)
Mtuhumiwa anaweza kutumia utetezi huu endapo anakabiliwa na shtaka la kufanya kosa la jinai pale ambapo mazingira yalimlazimisha kufanya kosa hilo.

Mazingira yamemlazimisha kutenda kosa hilo ili kuepuka kusababisha madhara makubwa zaidi au kosa kubwa zaidi ya alilotenda.

Kimsingi utetezi huu haupo katika sheria ya Kanuni za Makosa ya Jinai au sheria za Tanzania kwa ujumla lakini ni utetezi unaotambulika na kukubalika nchini kwa kufuata sheria za Uingereza ( common law) kupitia kifungu cha 2 cha Sheria za Mahakama ( Judicature and Application of Laws Act) ambacho kimeruhusu kutumika kwa sheria hizo nchini mnamo tarehe 22 July, 1920.

Utetezi huu unakubalika hasa pale mtu anapokuwa katika hatari. Ili mtuhumiwa aweze kufanikiwa katika utetezi huu anatakiwa kuzingatia mambo yafuayayo.
(a) Lazima pawepo na hatari ambayo ingesababisha madhara makubwa kuliko madhara ya kosa alilotenda.
(b) Hakuwa na mbadala au namna ya kuweza kuepuka kutenda kosa hilo.
(c) Kitendo au kosa alilotenda halina madhara makubwa zaidi ya lile ambalo lingetokea kama angeacha litokee.

Katika utetezi huu, inaaminika kwamba mtuhumiwa ametenda kosa ambalo mtu yoyote mwenye ufahamu wa kawaida angetenda kama angekuwa katika mazingira yaliyomkuta mtuhumiwa.

Asili ya utetezi huu ni Uingereza hasa katika shauri la JAMHURI dhidi ya DUDLEY na STEPHENS (1884).
Katika kesi hii watuhumiwa hao wawili na kijana mdogo wa miaka 17 walikuwa safarini katika meli ambako walikwama baharini kwa siku 18 na walikosa chakula na maji kwa siku 7 baada ha kuishiwa.

Wawili hao Dudley na Stephens walishauriana na waliamua kumuua na kumla yule kijana mdogo ambaye alionekana kudhoofu sana kiasi cha kukaribia kupoteza uhai. Hii iliwasidia kuokoa maisha yao kwa siku kadhaa walizokuwa huko majini kabla ya kuokolewa na kufikishwa Mahakamani.

Walifikishwa Mahakamani kwa kosa la mauaji ya yule kijana aliyejulikana kwa jina la Richard Parker. Katika utetezi wao wakasema kwamba ilikuwa ni lazima kwa wao kumuua yule kijana ili kuokoa maisha yao.

Lakini, Mahakama ilikataa utetezi huu na kuwahukumu kunyongwa kabla baadae kupunguziwa hukumu na kufungwa miezi sita (6) gerezani.

Utetezi huu wa kimahitaji haupaswi kutumika kwa mtu aliyepoteza uhai wa mtu mwingine kwaajili ya kuokoa maisha yake. Thamani ya mtu haipimwi kwa kuondoa uhai wa mtu mwingine.

Jambo la msingi katika utetezi huu ni kuangalia kama mazingira yamemlazimisha mtuhumiwa kutenda kosa ambalo madhara yake ni madogo ukilinganisha na madhara ambayo yangetokea endapo hasingetenda kosa hilo, hivyo hakuwa na namna nyingine.

Mfano. Binti ametolewa ujauzito na daktari ili kuokoa maisha yake ambayo yalikuwa hatarini kupotea endapo angekuja kujifungua, kutokana hali yake kiafya kufuatia vipimo vya kitabibu. Japo kutoa mimba ni kosa, lakini katika mazingira kama haya utetezi huu unaweza ukakubalika na mtuhumiwa kuachiwa huru.

8. DHANIA ISIYO KWELI ( Mistake of facts )

Utetezi huu unatumika kwa Mtuhimiwa ambaye ametenda kosa la jinai kwa kukosea uweli.
Mtuhumiwa anatakiwa kuthibisha mambo yafuatayo:
(a) Ametenda kosa hilo pasipo kudhamilia.
(b) Amekosea ukweli, kwa kuamini kuwepo kwa kitu fulani tofauti na jinsi uhalisia ulivyo.
(c) Alikuwa na dhamira njema na sio kutenda kosa la jinai kama ilivyokuwa hatimaye.

Mfano; kesi ya JAMHURI dhidi ya SULTAN MAGINGA (1969) HCD,
Katika kesi hii Sultan Maginga alishtakiwa kwa kosa la mauaji.
-Tunaambiwa kuwa siku moja wakati wa usiku Maginga alienda shambani kulinda shamba lake dhidi ya nguruwe poli waliokuwa wakiharibu mazao hapo shambani.

-Alipofika shambani aliona majani ya mpunga yanatikisika kiashiria cha kuwepo hao nguruwe pori maeneo yale lakini hakuwa na uhakika ni nini kilikuwa maeneo yale.
-Akajaribu kuita kujua kama ni binadamu basi ajitokeze lakini ikawa kimya.
-Ghafla aliona kama vimvuli vinakimbia uelekeo tofauti, aliwasha tochi yake lakini haikuwa na mwanga wa kutosha kumwezesha kuona mbali ndipo aliamua kurusha mkuki na kumchoma mmoja kati ya wale waliokuwa wanakimbia.

-Alipofika karibu ndipo akagundua kuwa alichokirushia mkuki hakuwa nguruwe pori bali ni binadamu ambao inasemekana walikuwa ni watu waliouwa wakifanya mapenzi nyakati zile za usiku katika shamba hilo la mpunga.

-Hatimaye Maginga alikamatwa na kufikishwa mahamani kwa kosa la mauaji na ndipo aliopotumia utetezi huu wa dhania isiyo kweli ( mistake of facts) na utetezi wake ulikubalika.

Hivyo, ukiweza kujitetea kwa kutumia utetezi huu na ukaweza kuthibitisha vigezo vinavyotakiwa, Mahakama inaweza kukuachia huru au kuamua vinginevyo kwa mujibu wa sheria.

rejea kusoma kifungu cha 11 cha sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Makosa ya Jinai

9. KINGA YA KISHERIA (Judicial Immunity)

Huu ni utetezi unaotumika kwa maafisa wa Mahakama kama vile Jaji, Hakimu au afisa msajili wa Mahakama, kwa makosa wanayoweza kufanya katika kutekeleza majukumu yao ya kazi.

Lengo la utetezi huu ni kuhakikisha uhuru wa mahakama katika utoaji wa haki au maamuzi. Hii inawasaidia kutekeleza majukumu yao kwa uhuru na bila hofu ya kuingia hatia ya kosa la kijinai.

Hivyo, afisa wa mahakama anaweza kutumia utetezi huu kwa makosa aliyofanya pindi anatekeleza majukumu yake. Hivyo ametenda kosa hilo kwa nia njema ili kutekeleza majukumu ya kazi yake ya Kimahakama.
(rejea kusoma kifungu cha 16 cha sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Makosa ya Jinai sura ya 16)

10. KUTOADHIBIWA MARA MBILI (Double Jeopardy) Mtuhumiwa anaweza kutumia utetezi huu kwa kosa ambalo tiari Mahakama imelitolea maamuzi.

Maamuzi hayo yanaweza kuwa mtuhumiwa amekwisha adhibiwa au aliachiwa huru.

Hivyo, sheria inasema kwamba, mtu hawezi kuadhibiwa mara mbili kwa kosa lile lile. Hii ina lengo la kufanya kesi ziweze kufikia mwisho na kuepusha usumbufu kwa watuhumiwa au Mahakama kwa ujumla.

(rejea kusoma kifungu cha 21 cha sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Makosa ya Jinai sura ya 16)

11. KULINDA MTU AU MALI
(Self Defense/ Defense of Person or Property)

Mtuhumiwa anaweza kutumia utetezi huu kwa kosa la jinai la kuua au kujeruhi alilofanya wakati anatimiza haki yake ya
(a)Kujilinda au kujitetea katika shambulio au uovu wowote.

(b)Kumlinda mtu mwingine dhidi ya shambulio au uovu wowote.

(c)Kulinda mali yake au mali ya mtu mwingine isiibiwe au kuharibiwa.

Utetezi huu unakubaliwa nw Mahakama inaweza kumwondolea hatia ya kosa hilo la jinai.

Katika kujilinda, kumlinda mtu mwingine au mali, mtuhumiwa anatakiwa awe ametumia nguvu kiasi zinazostahili. Matumizi ya nguvu kupita kiasi yatamfanya mtuhumiwa huyo kuwajibika kwa mujibu wa sheria.

Mfano, Mtu akikushambulia kwa kukupiga ngumi, sio sahihi kujibu mashambulizi kwa kutumia panga kwani kufanya hivyo ni matumizi ya nguvu kupita kiasi.

Hivyo, ni vyema kuwa makini katika nguvu unazozitumia katika kujitetea. Lakini, sheria inasema, kama ukisababisha kifo kutokana na matumizi ya nguvu kupita kupita kiasi utahukumiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia.

Katika utetezi huu, Mtuhumiwa anatakiwa kuthibisha mambo kadhaa kama matumizi yake ya nguvu yamesababisha kifo au madhara makubwa kwa mtu mwingine. Hivyo, ilikuwa ni lazima kutumia nguvu ili kulinda maisha yake, maisha ya mtu mwingine au mali. Mfano ni katika mambo yafuatayo.
-Hatari ya kupoteza maisha yake kama hasingetumia nguvu kujitetea

-Hatari ya kupata madhara makubwa/kuumizwa

-Hatari ya kubakwa au kufanyiwa tendo la ndoa kinyume na maumbile

-Kulikuwa na nia ya kutekwa nyara au kutoroshwa

-Kuvunja au kuingia ndani au unyang'anyi au kosa lolote la kijinai lenye kuhatarisha maisha au mali.

(_rejea kusoma kifungu cha 18, 18A, 18B na 18C cha Kanuni ya Adhabu ya Makosa ya Jinai, sura ya 16)

12. KUKASILISHWA KUPITA KIASI (Provocation)

Huu ni utetezi ambao mtuhumiwa wa kosa la jinai kwa kitendo kama vile kuua au kujeruhi anaweza kuutumia.

Ili Mtuhumiwa aweze kukubaliwa utetezi wake kuwa alikuwa amechukizwa kupita kiasi lazima athibitishe mambo yafuatayo.
(a) Alitendewa tendo ovu na la kumdhalilisha.

(b) Kitendo alichofanyiwa kililenga kumdhalilisha yeye binafsi au mtu yoyote mwenye uhusiano nae wa karibu.

(c) Kitendo cha kumdhalilisha kilikuwa ni cha hali ya juu kiasi cha kumfanya hashindwe kutuliza hasira zake au ashindwe kujitawala.

(d) Ametenda kosa hilo la kijinai papohapo na ni ghafla kiasi cha kukosa muda wa kutuliza hasira zake.

Mtuhumiwa atakayethibisha kuwa ametenda kosa la mauaji kutokana na kukasirishwa kupita kiasi atahukumiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia.

(rejea kusoma kifungu cha 201 na 202 cha Kanuni ya Adhabu ya Makosa ya Jinai ili kuelewa zaidi maana ya utetezi huu.)

13. KUTOKUWEPO ENEO LA TUKIO (Defense of alibi)

Huu ni utetezi unaotumika pale ambapo Mtuhumiwa hakuwepo eneo la tukio au eneo ambalo kosa hilo la kijinai limetendeka.
Yaani Mtuhumiwa alikuwa sehemu nyingine hivyo isingewezekana kwa muda huo kuwepo eneo ambalo kosa hilo limetendeka.

Mfano, umeshitakiwa kwa kosa la wizi lililofanyika Dodoma majira ya saa moja asubuhi, Mtuhumiwa anaweza kutumia utetezi huu kuonesha kuwa alikuwa Morogoro pindi tukio hilo limetendeka, hivyo sio rahisi mtu uwe Morogoro arafu wakati huohuo uibe mali ya mtu iliyopo Dodoma.

Lakini, kauli ya kusema tu "sikuwepo" haitoshi bali ni lazima Mtuhumiwa alete ushahidi au mashahidi wa kuweza kuthibitisha kwama walimuona au alikuwa nao huko anaposema kwamba alikuwepo siku hiyo ambayo kosa limetendeka.

Kwa kuhitimisha mada hii ya utetezi wa kijinai, mtuhumiwa anayo haki ta kusikilizwa na kujitetea Mahakamani kwa kosa lolote la kijinai.

Kukubalika au kukataliwa kwa utetezi wake inategemea na namna mtuhukiwa atakavyoweza kuthibitisha utetezi husika kulingana na kosa husika.
(ongeza maalifa kwa kusoma kifungu cha 194 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai)

Ahsante wa kuwa pamoja nami tangu tulipoanza mada hii ya UTETEZI WA KESI ZA KIJINAI hadi hapa tulipoishia. Nawakaribisha kufuatilia mada zijazo.

Mwisho

Ahsante na hongera kwa kusoma hii ndefu kuhusu utetezi wa makosa ya jinai. Ubarikiwe sana msomaji wangu.

It's prepared by
A Lawyer and LifeCoach
Mr. George Francis
Contacts: 0713736006
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com
Ndg Wakili naomba kuuliza! Kama niligushi na kujimilikisha Mali isiyo yangu, natakiwa nujiteteeaje hapo!!??
 
Kuunganishwa katika jinai labda lwa kukamatwa ukiwa na mtuhumiwa pasipo kujuwa kama alitenda kosa ila ukajumuishwa mfano wizi n.k hii imekaaje
 
Back
Top Bottom