star health talks
Member
- Apr 28, 2017
- 26
- 58
Vipimo vinavyotumika mara nyingi sana kupima HIV/VVU ni aina ya HIV antibody tests, changamoto ya vipimo hivi ni kuwa kinahitaji mtu awe amepata maambukizi angalau miezi mitatu nyuma kabla ya kupima ili kipimo hiki kiweze kumgundua mtu kuwa ana maambukizi ya HIV/VVU.
Ndo maana ukipima katika vituo vya kutolea huduma za afya na majibu yakawa negative unashauriwa kupima tena baada ya miezi mitatu, wale wanaopima hapo hapo na mtu wake majibu yakawa negative na kuamua kwemda kavu kavu kuna risk kubwa tu.
Kipindi hiki ambacho kipimo hakijaweza kugundua kuwa mtu ana maambukizi ya HIV/VVU ndo kipindi mtu mwenye maambukizi mapya ya HIV/VVU anakuwa na uwezo wa kuambukiza HIV/VVU kwa kiasi kikubwa sana highly infectious period. Take home message ni kuwa ukimpima mtu kwa mara ya kwanza akawa negative pima tena baada ya miezi mitatu kuhakiki hali yake ya maambukizi ya HIV/VVU, pili tuendelee kutumia kinga mara zote na kuwa waaminifu kwa wenza wetu.