ILI kuweza kutatua matatizo na kujiletea maendeleo endelevu watu wote wanapaswa kujifunza mambo mengi kila siku. Tangu tumezaliwa bado tunaendelea kujifunza kwa maana haiwezekani kujua kila kitu. Anayejua hiki hajui kile. Kujifunza ni kuongezeka kwa uwezo wa mtoto wa kupambana na kupambanua mazingira yake kwa kutenda, kuona, kuonja, kusikia na kunusa.
Uwezo huu ndio unaomwezesha mtoto kuelewa, kufahamu na kupata uzoefu wa kutenda. Badiliko hili la kujifunza mambo mbalimbali na tabia linatokea wakati mtoto anapopambana na mazingira yake nyumbani, katika jamii, kundi rika shuleni na anapojihusisha na vitu mbalimbali. ZAIDI...