Namna Jenerali Qasem Soleiman alivyotumiwa na Wamarekani

hamis77

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
13,809
21,427
Tunajitahidi kuwaelimisha watu wengi mipango ya kimkakati inayo tumiwa na Wazungu hususani Wamarekani katika muendelezo wa kuitawala dunia.

Watu wengi wanafikiri kwamba mtu kutumika ni lazima achangamane na mshirika wake, lah! siasa haipo hivyo,"bali wakati mwingine unaweza kuwaona Trump na Mfalme Salman,wakigongeana grasi na kufurahi,"Kumbe nyuma ya pazia wanapigana vita vya kiakili,vilevile unaweza kuwaona wanasiasa wakipayuka kwa kujiakti ni maadui,"kumbe nyuma ya pazia hushirikiana,Na hivyo ndivyo zilivyo Irani na Marekani.

MASHIA WALIVYOGEUZWA CHAMBO TOKA WAKATI WA VITA VYA KUMNG'OA SADDAM HUSSEIN
Hapa Wazungu waliamua kuzitumia chuki za Mashia dhidi ya utawala wa Saddam ambaye alikuwa Msuni,na Jenerali Qasem Soleiman pia alishiriki kisiri katika vita hivi ambavyo mwishowe tutaona Wamarekani walimweka Waziri mkuu Mshia anayeungwa mkono na Irani Nour al Maliki.

PICHA NA MAELEZO
Picha namba moja na mbili tutamwona aliyekuwa raisi wa Marekani George Bush,na Waziri mkuu Mshia Nour al Maliki,wakipata chakula pamoja na wanajeshi wa Marekani katika sherehe za kupongezana baada ya kuushinda utawala wa Msuni Saddam Hussein.

Picha namba tatu tutamwona aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza wa Iraki na ambaye ni kibaraka wa Marekani Nour al Maliki, akiwa pamoja na kiongozi wa kidini wa Irani Ayatollah Khamenei.

Picha Namba nne tutamwona Jenerali Qasem Soleiman akiwa na Nour al Maliki ambaye ni kibaraka wa Marekani huko nyumbani kwake nchini Iraki.

SWALI WANALOJIULIZA WATU NI HILI, IKIWA NI MTU WAO SASA KWA NINI WAMUUWE?
Marekani na Wamagharibi walicheza na akili za Wairani, walizitambua chuki zao za kihistoria dhidi ya Waarabu, kwani ni Waarabu ndio walio isambaratisha dola ya Uajemi ya Sassanidian Empire, hivyo mpaka sasa Wairani walikuwa na ndoto za alinacha za kuirejesha himaya yao ya Majusi ikiwa chini ya Mfalme wao Ayatollah Khamenei, Jenerali huyu ameuawa baada ya kuvuka mstari wake aliochorewa wa kupambana na Mataifa ya Kiarabu, badala yake akaanza kujiandaa akitishia maslahi ya waliompatia nguvu yeye pamoja na vikosi vyake vyote vya Wapiganaji wa Kishia katika ardhi za Mashariki ya kati.

Jenerali Qasem Soleiman kujishughulisha zaidi na vikosi vya Wapiganaji wa Kishia nje ya mipaka ya Irani ili kuyadhibiti tena maeneo ambayo yalikuwa chini ya utawala wao ya Yemen, Iraq, Syria na Jerusalemu inayokaliwa na Israeli.

Hivyo walichokifanya Wazungu ni kuwatumia dhidi ya Waarabu kisha kuwa na taadhali nao, kwani Irani hana ubavu wa kuzidhibiti ardhi za Syria na Iraki bila ya msaada wa Marekani na Russia, hivyo ndoto yake hii ya kutafuta dola mgongoni mwa Wazungu ilikuwa ni ujinga tu ulio wanufaisha Wazungu na kuuacha Ulimwengu wa Kiarabu na Kiislaamu ukishindwa.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…