Nakumbuka Mwaka 2012

Magical power

JF-Expert Member
Sep 27, 2022
1,990
5,249
Nakumbuka Mwaka 2012
1737528131498.jpg

Kipindi Ujana Maji Ya Moto πŸ˜‚, Nilianzaga Mazoezi Ya Ngumi Kwa Ajili Ya Self Defense (Deep Down Ni Ukorofi Tu Ndo Ulikuwa Unanisumbua)

Basi Bana Nikapiga Tizi Usiku Na Mchana Kwa Kipindi Cha Miezi 3. Kidume Nikajiona Nimekwiva Teyari Kwa Mapambano
- Kukabiliana Na Yeyote Yule Atakayezingua. (Unajua Ukianza Mazoezi Ya Ngumi Mikono Uwa Inawasha Unajiona Mohamed Alli)

One Day Baada Kula Ugali Wangu Tembele Kwa Bi Mkubwa πŸ˜‚ Nikaenda Zangu Road ( Road Ni Sehemu Kama Town Sehemu Mnayokaa, Biashara Zote Zipo Huko - - Kwa Kifupi Mishemishe Zote Zipo Huku, Stendi Za Daladala, Biashara Nk.)
Tuendelee, Si Unajua Tena Nina Miezi Kama Mi3 Nafanya Mazoezi Ya Ngumi Tu Lakini Bado Sijapigana Na Mtu Yoyote Kiukweli Ukweli, Siku Hiyo Nikaona Isiwe Tabu, Ngoja Nijipime Kama Nimekwiva. Nilipofika Road -
Nikawa Namuangalia Yoyote Yule Mnyonge Nimuanzishie, Finally Nikamuona Muuza Machungwa Na Baiskeli Yake, Nikamsimamisha Then Nikamwambia Animenyee Chungwa Nile, Kweli Bana Jamaa Akamenya Akanipa, Tf Nikamwabia Bro Ili Chungwa Chachu Sana Kwahiyo Silipi (Hapo Natafuta Shari Tu πŸ˜‚)

Jamaa Akaja Juu " inakuaje Umekula Chungwa Alafu Utaki Kulipa Na Machungwa Yangu Yote Ni Mazuri,
Nipe Hela Yangu Bro Nimetoka Kigoma Kuja Kutafuta Sio Kuchekea Watu"" Dah Mimi Sasa Nikaona Eenh Kajaa ***** 🀣, Huyu Huyu Ndo Wakujipima.

Nikamwambia Chungwa Nimekula Na Sikulipi
- Nikajifanya Kama Nataka Niondoke Ili Ajaribu Kunishika Nicheze Na Kidevu

🀣. Dah Mipango Aikufanya Kazi Kwani Jamaa Alinirukia Sijui Taikwando Au Mieleka, Nikajikuta Nipo Chini Gafulaa Alafu Mdomoni Natoka Damu πŸƒπŸΎβ€β™‚οΈπŸ˜‚.🀣🀣🀣🀣🀣

Bwege Mimi Nikainuka Ili Nizipange Sasa, Mweh Kila Nikirusha
Ngumi Jamaa Anakwepa Alafu Napewa (Acha Kabisa Mtu Na Mali Yake πŸƒπŸΎβ€β™‚οΈπŸ˜‚) Nomaa Watu Wamejaa Wametuachia Uwanja Paringi Mtu Mbili ,

Dah Kila Nikirusha Ngumi ***** Jamaa Gadi Ukuta Akirusha Kwangu Lazima Niyumbe Kidogo Kama Sio Kwenda Deki, Kila Nikiangalia Ule Umati Wa Watu Atokee

- Hata Mtu Agombelezee Akuna, Watu Wanapiga Viluzi Tu Mpambano Uendelee, Ah Nikaona Isiwe Tabu Hapa Nikutoka NDUKI Tu πŸƒπŸΎβ€β™‚οΈπŸ˜‚, Hata Tyson Alishawahi Pigwa Adi Akang'ata Mimi Ni Nani Mpaka Nivumilie Kutoka Manundu πŸƒπŸΎβ€β™‚οΈπŸ€£πŸ˜‚. Nikatoka Tokaa Nduki Bana Watu Nyuma Wakaniungia Kamata Huyo

- Kamata Huyoooooo πŸƒπŸΎβ€β™‚οΈπŸƒπŸΎβ€β™‚οΈπŸƒπŸΎβ€β™‚οΈπŸƒπŸΎβ€β™‚οΈ. Dah Na Ndio Ukawa Mwanzo Na Mwisho Kucheza Ngumi Na Pia Kupigana Na Mtu Ngumi Tupu Bila Kutegemea Silaha.

kama Nikizinguanaa Na Mtu Naenda Home Kuchukua Chapa Jogoo Then Namfanya Bucha πŸ˜‚πŸƒπŸΎβ€β™‚οΈπŸƒπŸΎβ€β™‚οΈπŸƒπŸΎβ€β™‚οΈπŸƒπŸΎβ€β™‚οΈ, Mpaka Wakanipa Jina La Eguchi πŸ™ŒπŸΎπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.

Nb:
By The Way : Picha Na Matukio Ni Tofauti, Nimeweka Picha Kuelezea Tukio Halisi.
 
Back
Top Bottom