Najituma kuliko unavyoweza kufikiri, kila hatua ninayopiga ni ya moto, sioni hata walau mwanga wa mafanikio. Nahisi kuukatia tamaa ujana wangu

FORTUNE JR

Member
Mar 20, 2021
82
495
Wasaalamu Mabibi na Mabwana . Poleni na Majukumu.

Mimi ni (Me), nina Umri wa miaka 24 sasa, Nimechoshwa, najihisi kukataa tamaa kabsa ya Maisha kutokana na mapambano ya usiku na Mchana pasina Mafanikio.

Labda nianze na Utangulizi(Background). Nimezaliwa mkoani Iringa. Elimu yangu ya Msingi nimesoma kati ya Mwaka 2005 hadi 2011, katika shule niliyosoma katika kusoma kwangu kote nilikua nikiongoza darasani, Darasa lenye takribani wanafunzi 50+. Kwenye mashindano baina ya shule yetu na shule jilani ambapo sometimes tulikua tunaungana hata shule 6 Kufanya mitihani kwa pamoja sikuwahi kutoka nje ya top 4..

Baada ya kumaliza Elimu yangu ya Msingi nkachaguliwa moja ya shule maarufu ya vipaji Mkoani Morogoro, Competition ilikua ni kubwa sikuwahi kunusa top 5 lakini pia hali haikuwa mbaya Mara nyingi niliangukia 6-15. Nikamaliza Form 4 2015 kwa ufaulu mzuri tu wa dision 1, na ni darasa zima tulifaulu kwa division 1 na 2.

MLANGO WA MFULULIZO WA MIKOSI NA BAHATI MBAYA UNAFUNGUKA .
"Nikiwa katika Maandalizi ya kwenda kidato cha 5 kuna binti mmoja nlikuwa na mahusiano naye, nilimpenda sana, siku chache kabla ya kwenda shule binti alinitunuku tunda, sikuwahi Kulala na Mwanamke kabla kwaio yeye ndiye aliyeniharibia Uvulana Wangu" naomba ikumbukwe hii itasaida kuunganisha matukio mbele ya safari

Safari Yangu ya masomo Ya kidato cha 5 ikaendelea Mkoani Mbeya kwa Mchepuo wa CBG Moto uliwaka mapema kabsa na nilijiwekea malengo makubwa, nilala mda mchache sana, mda mwingi nilitumia kusoma iwe mchana au usiku. Mwisho wa term tulifanya mtihani nilipata "D" moja tu na masomo yaliyosalia ni "F"(Miswaki) Nilikua top 5 ya mwisho Darasa la watu 80+, Hii ilikua Anguko langu kubwa zaidi kuwahi kutokea katika masomo Ilinifanya kuwa Mnyonge na kutoelewa hasa nini kimetokea maana nilisoma sana kabla ya mtihani. Nikachukulia ajari kazini ingawa iliniogopesha kwakua ilitokea kwenye mazingira ambayo hata ckutambua yan hadi rafik zang ambao mm ndio nlikua nawafundisha na pindi ya kumaliza mtihani walikiri kua Mtihani ulikua mwepesi maana vingi walivielewa kutokana na nilivowafundisha.

Kwenye maandalizi ya Mtihani uliofwata hapo ndipo niliposahau kabsa kama hata nilienda na Godoro shule nilisoma bila kuchoka huku nikiwa nakumbukumbu ya kufeli mwanzo. tukafanya mtihani tena matokea yakawa ni "D" moja na miswaki"F" masomo mengine nafasi ya 3 kutoka mwisho. Hii hali ilinifanya kua mpole, Mnyonge, Mwenye kujitenga Mda wote. Nikaamua kubadili Combination kwakuhisi huenda masomo nayosoma Si Fani yangu, lakini ikumbukwe hayo masomo ndiyo niliyoyafanya vizuri kipindi cha nyuma. Safari hii nikajiunga na Darasa la HGL ambao walikuwepo 60+ darasani, pindi likaendelea lakin bado maswali ni Mengi kwenye ufaham wangu wa akili hasa nkikumbuka mbona Darasani naelewa vizuri sana kipi kinanikuta pindi nikiingia kwenye mtihani?. HGL Haikuwa kozi ngumu hivyo nilishakua nimeelewa vitu vingi kwa mda mfupi, Tukaingia kwenye mitihani tena Safari hii nikitaka kujitathimini tena lakin nina Woga haswa, Matokeo yakaja Language II "D" Language I "D" yaliyobaki ni miswaki, mtu wa 5 toka mwishoni.

Nikaenda bwenini nikachukua Vitabu vyangu vyote nikampa rafik ang mmoja, Then nikachukua Daftari zangu na Uniform nikaenda kuchoma moto saa hio machozi yananitoka nashindwa kuyazuia nikabeba begi langu mgongoni tayari kwakuludi Iringa kifupi nilijifuta shule. Nikaludi nyumbani kwa wazazi ambao ni wakulima wa kipato cha chini sana walitumia nguvu kubwa sana hata kwenye kunisomesha nikaungana nao kwenye kilimo, kwa Takribani mwaka Mmoja hivi

Naomba ku Summarize , Baada ya huo mwaka 1, Wazazi matumaini yao yote ni mm nisome ivyo wakauza mazao na mikopo juu wakanitafutia Private fulan nisome mwaka mmoja , Of course nilienda HGL once again, niliwakuta wenzangu 9 katika mitihani ya ndani na Test zote mimi niliwafungia mahesabu/walinizi mda wote ilihali nilisoma sana nilijitesa zaidi yao lakin wap. Tukafanya Necta form 6 tulifaulu wote ila Mm kwa kuchechemea sana.

Nko chuo Sasa ni Mwendo wa Supplementary kila Semister, Sometimes sup 3, Nilikua mcheshi sana zamani, lakini sasa ni mpole, Mnyonge najitenga mda wote, Mwenye Misongo ya Mawazo mbaka kupelekea sasa nina matatizo ya presha na vidonda vya tumbo.
Kuna siku nilienda kwenye mkutano mmoja wa Injili kuna Mtumishi nilimfwata nilimwomba aniombee, nilimwambia tu kuna changamoto za maisha napitia ingawa sikusema Exactly kinachonisibu, alichoniambia yule mtumishi wakati ananiombea alisema anaona kuna Agano/mkataba nimeingia na binti ambapo uyo binti yeye Koo yake na mizimu yao ilishakataa wao kujihusisha na Elimu. Ukumbuke sikumweleza huyu mtumishi hata kama ni issue za Ki Elimu, Hili lilinshtua sana Lilinifanya nitulize akili yangu na kutathimini, nikaja kugundua kweli toka nizini nayule binti ndipo mikosi na bahati mbaya Zilipoanza, pia nikaenda mbali zaidi nikaja ku prove kweli ile koo ya yule binti hakuna aliyewahisoma zaidi ya darasa la 7 yan wote wakifika hapo ni full stop.

Yule mtumishi aliniombea na kuniambia nkazane kujiombea mwenyewe, Mbaka sasa Najitahidi kuomba sana sometimes hadi kwa mifungo lakini bado hali tete Naelewa masomo vizuri ila nikiingia kwenye mitihani shughuli ni tete ni Sup nje nje. Nakosa raha sana hasa nkiwatazama wazazi wangu ambao wanazidi kuchoka matumaini yao kwangu, Hadi sasa GPA kisoda.
Siendi starehe na marafiki, Situmii vilevi, Sio mtu wa Wanawake natumia mda mwingi mpweke Kujisomea, kufunga na Kuomba lakini bado sioni Mwanga, nahisi kukata tamaa, na nje ya msingi ya Elimu kutoboa nayo ni kipengele, wazazi nao wananitazama. NIMECHOSHWA SANA, NIMECHOKA .nakula maombi sana nakula kitabu sana lakini wapi

Asanteni kwa time yenu! Na Mungu awabariki
 
Wasaalamu Mabibi na Mabwana . Poleni na Majukumu.

Mimi ni (Me), nina Umri wa miaka 24 sasa, Nimechoshwa, najihisi kukataa tamaa kabsa ya Maisha kutokana na mapambano ya usiku na Mchana pasina Mafanikio.
Mwampo umemcheki tumaji twake na mafuta vina save sana vile..

Ingawa na mm km umenipiga alarm hivi mmh humu tunamopita tuwe makini sana tunabeba visivyobebeka kabisa..
 
0787 315 762 mtumishi vumilia huyo mtafute akuombee

Kisa changu
mi mwenyewe nilikuwa na hali kama yako o level nilikuwa best student wa 2 nilipiga 1.13 2019 hapo wengi walipiga 2 na 3 shuleni kwetu.

A level nikaaingia kwa mbwembwe nyingi term ya 1 f5 nilikuwa top 5 PCM hapo

Likizo nililala na malaya aseeee kurudi shule 2021 nilifeli vibaya mno nusu nifukuzwe shule nilikuwa napiga division 0 F zote mitihani yote mkuu daaah nimerudi likizo nikaunganishwa na mtumishi nikaombewa fresh

Mungu alivyo wa ajabu kwanzia nimeingia term 2 f6 2022 nilikuwa nakula 3 na 2 necta nikaosha 2.11 safi

Saivi nipo chuo nagonga mabanda tu A nguvu kidogo gpa inasoma na Mungu akipenda ntakuwa best student kwa mwaka huu wa 1 aseee navyoona

Semester ya 1 nina gpa ya 4.x x = siisemi 😆😜😜

Ila nipo serious huo ni ushuhuda wangu n.b kaa mbali na uzinzi
 
Nikaenda bwenini nikachukua Vitabu vyangu vyote nikampa rafik ang mmoja, Then nikachukua Daftari zangu na Uniform nikaenda kuchoma moto saa hio machozi yananitoka nashindwa kuyazuia nikabeba begi langu mgongoni tayari kwakuludi Iringa kifupi nilijifuta shule.
Babu yenu Mkwawa kawarithisha urithi mbaya sana nyie wanyalu. Angalia usijinyonge, rehema za Mungu ni kama bahari.
 
nina Umri wa miaka 24 sasa, Nimechoshwa, najihisi kukataa tamaa kabsa ya Maisha kutokana na mapambano ya usiku na Mchana pasina Mafanikio.
24 unakata tamaa bado kinda kabisa, wenye 35+ na bado wanauza Samaki na mafungu ya nyanya kwa pesa za mkopo na kila siku wanafuatwa kulipa madeni, kila siku wanahama machimbo ya mikopo wanakopa huku wanalipa huku ili maisha yasonge nao wasemeje ?
 
So sad 😢😔
 
So sad 😢😔
Yes ndio maisha ya kitaa mtu ana vicoba zaidi ya 8 anashirikiana na mkewe ili maisha yasonge watoto wanataka kula na kuvaa kupishana chooni, wewe ndio baba shughuli yako kuchoma Samaki mama mpika sambusa na chapati umekopa laki 5 mtaji wa Samaki umekula hasara wenye mkopo wao wanakufuata hadi nyumbani ukapata mkopo mwingine wa laki 8 ili ulipe laki 5 ubaki na laki 3 uongezee kwenye mtaji siku 3 nyingi biashara haujaenda ukakopa Tena kwingine laki 4 uongezee mtaji hujakaa sawa wamekufuata watu wanataka kukopesha laki 6 ukachukua ili biashara ya nyanya iende, sasa huyu ndio kwanza 24 jua ndio kwanza linachomoza kakata tamaa au amerogwa ?
 
Duuuh aseee life kwa ground ni tabu mnooo 😓😓 mi mwenye 20 inabidi nitembee kifua mbele

Ila kinachosikitisha ni unakuta kijana mdogo wa 26 years yupo kwenye v8 na bonge la jumba, ajira na biashara nzuri unajiuliza daaah huyu jamaa kawezaje

Hii kitu inachoma sana moyo mkuuu
Japo wenye shida ni wengi
 
Ila kinachosikitisha ni unakuta kijana mdogo wa 26 years yupo kwenye v8 na bonge la jumba, ajira na biashara nzuri unajiuliza daaah huyu jamaa kawezaje
Kila mtu atakula kwenye sahani yake mkuu, kuna wanaopewa maji kwenye vikombe vya plastic na wanaopewa kwenye kibombe Cha bati (birauli) na wanaopewa kikombe Cha glass, kwa hio kuna tofauti huyu wa kwenye glass ikidondoka ikivunjika haiwezi kurudi tena km awali Ila mwenye kikombe Cha plastic na huyu mwenye kikombe Cha bati kikidondoka haviwezi kuvunjika hata kidogo, fumbo lifumbue
 
Nice one ila nimeelieelewa asee
 
Wasaalamu Mabibi na Mabwana . Poleni na Majukumu.

Mimi ni (Me), nina Umri wa miaka 24 sasa, Nimechoshwa, najihisi kukataa tamaa kabsa ya Maisha kutokana na mapambano ya usiku na Mchana pasina Mafanikio.

Labda nianze na Utangulizi(Background). Nimezaliwa mkoani Iringa. Elimu yangu ya Msingi nimesoma kati ya Mwaka 2005 hadi 2011, katika shule niliyosoma katika kusoma kwangu kote nilikua nikiongoza darasani, Darasa lenye takribani wanafunzi

Asanteni kwa time yenu! Na Mungu awabariki
Sasa c umeambiwa tatizo ni huyo Binti c umuache ? Ili wewe uendeleee na mengine
 
Ni Kweli ngono ni hatari lakini unabidi kuamini katika Mungu wa Majira Kama unasoma Sana na unafeli hapo tatizo lipo maana sisi wengine ili tupate Sup maana yake hatujasoma kabisa.
 
Mi mwenzenu navyochepuka nasali kabla ya kugegeda. Nakua honest tu kua mungu najua natenda dhambi ila naomba nilinde hapa napogegeda nisibebe malaana toka kwa huyu manzi.Kama amenuia kunichawia kupitia papuchi yake naomba minu zake zikwame malaika zako wanisimamie nitoke salama bila mikosi wala majanga.

Hii nimeona inanisaidia.
 
Back
Top Bottom