GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 6,837
- 9,669
Jana, katika pita pita yangu mitandaoni, nimekutana na clip yenye tafsiri ya neno Tanganyika.
Tanganyika ni neno la Kichapu likimaanisha nchi yenye rutuba.
Kwa uelewa wangu, rutuba inaashiria ustawi.
Unajua maneno yanaumba? Ni kipindi gani nchi ilikuwa na ustawi, ilipokuwa ikiitwa Tanganyika au baada ya jina jipya, Tanzania?
Linganisha ujenzi wa reli ya Kati miaka hiyo na ya SGR miaka ya sasa! Unajua, ingawa miaka hiyo teknolojia haikuwa juu kama ilivyo sasa lakini ujenzi wa reli haukuchukua muda mrefu kama wa SGR?
Yumkini kulikuwa na agenda ya siri iliyopelekea maadui wa Tanganyika kutaka kuitokemeza kwa jina mbadala, Tanzania.
Japo nilijiita Mtanzania muda mrefu, lakini nimegundua mimi ni Mtanganyika. Na ninapojiita Mtanganyika, ninajisikia huru zaidi.
Msiniite Mtanzania, hilo ni jina bandia. Mimi ni Mtanganyika. Tanganyika ndilo jina halisi la nchi yangu.
Hata wasiponiita Mtanganyika, mimi nitaendelea kujitambua kuwa ni Mtanganyika.
Mimi ni Mtanganyika, raia wa nchi ya ustawi.