Tetesi: Naiona Mahakama ya mafisadi ikianza kazi

MSHAURI_WA_NCHI

Senior Member
Nov 10, 2015
139
73
Je unafikiri ni akina nani watuhumiwa Wa kwanza? Usisahau kuwa mramba na yona walifikishwa mahakani na hatimaye kufungwa ikiwa ni zaidi ya miaka 6 tangu watoke madarakani.

Tegemea baadhi ya vigogo ambao kwa sasa tumeanza kuwasahau kwenye orodha ya mafisadi papa kufikishwa na hatimaye kufungwa na Mahakama hii maalumu ya kusafisha nchi.

Msaidie. Rais kwa kuwataja mafisadi hapa JF ili upelelezi uanze....
 
Lazima wa screen watu wote watako husika na hiyo mahakama kama wanataka kufanikiwa. Kwani Twakukuru, upelelezi na kwingine kote kumejaa uozo ndio sababu hakuna fisadi hata mmoja anayetumikia kifungo.
 
Lazima wa screen watu wote watako husika na hiyo mahakama kama wanataka kufanikiwa. Kwani Twakukuru, upelelezi na kwingine kote kumejaa uozo ndio sababu hakuna fisadi hata mmoja anayetumikia kifungo.
Hiyo Mahakama ianze na kesi ya Zile billion 251 zilizopotea wizara ya Ujenzi kwa kulipwa makandarasi hewa, kisha ije kwa yule aliyenunua kivuko kibovu cha Dsm Bagamoyo kwa billion 8 na kwa Mwakyembe aliyenunua mabehewa chakavu, kabla ya kuendelea na escrow, mikataba ya Gesi, madini, uuzaji mali za umma nyumba za Serikali nk
 
Mahakama ianze na wizara ya zamani ya Magufuli huko kuna Ufisadi mwingi kuanzia kivuko na ulipaji madeni wa kijanja janja ( kandarasi hewa) kisha uendelee kwenye pesa za chenji ya Rada, bunge la Katiba, Buzwagi, zipo pesa nyingi zimetafunwa kimya kimya Mahakama ikianza kesi zitajaa mpaka mahakimu washindwe kupumua.
 
Kaka bila shaka na wewe ni fisadi au ndugu zako?
Mbona unaongea yasiyowezekana?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…