Naijutia kura yangu niliyowapa UKAWA kwa jiji la DSM

fdizzle

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,902
2,396
Nawasalimia wakuu!!
Mpaka kufikia kuanzisha hii mada naomba nikiri wazi kuwa nimefuatilia kwa kina mijadala unayo endelea kwa sasa hapa nchini.
Nisingependa kuwatoa katika mijadala hiyo lakini pia naomba tuchukue muda kutafakari baadhi ya mambo.
Ikumbukwe kuwa mwaka 2015 ulikuwa na changamoto kubwa ya watu kutaka mabadiliko. Naomba nikiri wazi kuwa mimi ni mmojawapo wa waliotaka mabadiliko na kura zangu zote niliwapa UKAWA, na bahati mbaya kura ya rais ndio ilishindwa.
Baadhi ya vitu nilivyotegemea baada ya UKAWA kuchukua jiji ni kufuatilia kwa kina suala la UDA na zile sarakasi za kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani.
Badala yake UDA imewashinda na wamekaa kimya, na cha ajabu zaidi tozo kwa wanaosindikiza wanaosafiri pale ubungo imepanda na cha kusikitisha hakuna uboreshwaji wa miundombinu ndani ya stendi (ukitaka kuijua vizuri kadhia hii nenda wakati wa mvua halafu ukute basi linataka kutoka nawe umechelewa utakanyaga matope bila ya kupenda).
Aliyewahi kuwa waziri mkuu enzi za awamu ya nne ndg. Lowassa alipata kusema bungeni kuwa "anashangaa wananchi wanalalamika na viongozi wanalalamika badala ya kuchukua hatua kutatua kero za wananchi"
Hii kauli naiona inatumika kwa hawa madiwani tuliowapa jiji kwani badala ya kuchukua hatua nao wanalalamika kuhujumiwa sasa sisi wananchi wa kawaida tufanye nini?
Nahuzunika kuona meya akitolea matamko suala la vyeti feki na mbaya zaidi anatoa matamko katika mtindo wa mipasho na tuliowengi wetu tunashangilia na kumsifia.
Nashauri ndugu zangu tujifikirie vizuri haya mambo tunayoshabikia na sio bendera kufuata upepo tu.
Kwa upande wangu najutia kura yangu niliyowapa UKAWA.
Nawasalisha.
 
Kwakuwa umetambua madhaifu haya basi usiichague UKAWA na kwakuwa nchi inaendeshwa na ILANI ya chama Tawala imewafanya UKAWA kushindwa kutekeleza majukumu yao hivyo kujiKuta ikiburuzwa na kulazimishwa kufuata ILANI ya chama Tawala.

Hivyo basi kwakuwa kumekuwa na mvutano wa kimaslahi kati ya chama Tawala na UKAWA nakushauri tena usivichague.
Ila ukichagua kimoja wapo kati ya hivyo atakuwa sio mzalendo wakweli bali utakuwa unanjaa inayokusumbua.
 
Ungemshauri kabisa afanye yale maamuzi ya Kihehe ili aondokane na hizi kadhia.
 
Hivi huyu jamaa mwenye vyeti feki hapa dar nae ni UKAWA?
 
Me ntaichagua tu coz juhud zao naziona kwenye issue ya uda wanafanyiwa mizengwe kibao mubashara, kuna hela walizigomea rais akatishia kuzichukua
Walizigomea halafu Raid akatishia kuzichukua baadae walizikubali siyo???

Na ishu ya mgao kwa madiwanini wanaounda jiji wa m3 ilifikia wapi vile???
 
Walizigomea halafu Raid akatishia kuzichukua baadae walizikubali siyo???

Na ishu ya mgao kwa madiwanini wanaounda jiji wa m3 ilifikia wapi vile???
Mpaka sasa wameigome.Serikali si kweli kwamba wamekubaliana na JPM.

Ila sababu jambazi wa UDA ni home boy Yale ya wizi wa raslimali za umma yamerasimishwa rasmi!
 
Waambie manake watu wamejikita zaidi kupambana na mtu/watu binafsi badala ya kupambana na kurekebisha changamoto za wapiga kura wao ili waonyeshe tofauti na watungulizi wao.Sasa utasikia Bashite,mtukufu,dikteta uchwara, malaika yaani hawapambani na issue za wapiga kura wao wanapambana watu binafsi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…