Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Ndg. Masauni hatoshi, amfuate Kitwanga akapumzike

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Nimemfuatilia kwa karibu utendaji wake na jinsi anavyojibu maswali bungeni,hajiamini,akitamka maneno hayasikiki,hatoi kauli kuhusu mauaji yanayoendelea,ni kama mtu anayependa mizaha.

Ni rai kwa Rais ampumzishe au la ampangie wizara Nyepesi.

Katika wizara ambazo Rais alikosea,moja wapo ni hii.
 
Huyo amepewa Wizara hiyo ili kusaidia mambo ya polisi na kuilinda zanzibar
 
Jana akiongozana na IGP na CDF katika kijiji cha Mikocheni huko Tanga (eneo la tukio), Naibu Waziri alitoa tamko, au huwa kuna idadi fulani ya matamko yanatakiwa kutolewa na yeye katoa machache.?

Mbona mimi nimesikia vizuri na ameeleka kabisa wakati wa kipindi cha maswali na majibu, au redio/ tv yako haina sauti? Lakini pia humo ndani aliyehitaji jibu amejibiwa na karidhika, la sivyo angesema hajaridhika na majibu.

Tusipende kukosoa bila sababu, au ni maswali gani ambayo unadhani hayajajibiwa?
 
jana nilisubiri nisikie wanakijiji walivyolalamika kuwa polisi wanawachoma wananchi wanaofichua wahalifu lakini kimya
 
You're right! Hii wizara ilitakiwa waziri awe jenerali mkorofi ila mwenye kuzijua na kuzijali haki za kikatiba za wananchi. Naibu wake alitakiwa awe komandoo aliyekubuhu katika idara zote na mwenye utumishi uliotukuka na medani za kutosha katika tasnia ya ulinzi na forensic. Hawa akina Masauni na Kitwanga sina hakika hata kama kufyatua risasi walishawahi kufanya hivyo.
 
Mhhh,,,,,,,!!!!!,??????
 
Wala haitaji hayo mambo,Hekima na Busara ndio ngao ya uongozi.Kama unampa mtu uongozi wakati hana uwezo wa kuongoza unategemea nini?
 
Watu mna maneno!!!nimecheka sana
 
Reactions: Wun
Mkuu wa mkoa alivyoshindwa kutoa majina ya watumishi hewa alifukuzwa mara moja, lakini viongozi walioshindwa kulinda usalama wa raia hadi watu zaidi ya 25 wanachinjwa nchi nzima mwezi May pekee wanadunda tu. Hii inaonekana maslahi ya mkuu wa nchi sio kulinda usalama wa raia kwa vile hawana thamani
 
jana nilisubiri nisikie wanakijiji walivyolalamika kuwa polisi wanawachoma wananchi wanaofichua wahalifu lakini kimya
Haya matukio yana mambo mengi, na sisi wananchi tuna maneno mengi pia.
 
Waziri amfyatulie risasi Nani? Tunachotaka ni waziri Mwenye mikakat
 
Waziri amfyatulie risasi Nani? Tunachotaka ni waziri Mwenye mikakat
Hiyo ni fasihi mzee. Wanajua kutumia silaha na mikikimikiki ya kipolisi/kijeshi? Anatakiwa mtu mwenye weledi katika eneo hilo ndicho nilichomaanisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…