Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel: Viongozi wa Sekta ya Afya simamieni ubora wa Huduma za Afya Nchini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,718
13,467
Naibu Waziri wa Afya Dk. Godwin Mollel, amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanasimamia ubora wa huduma katika Hospitali na Vituo vya kutolea Huduma za afya na kuhakikisha wanawajengea uwezo watumishi ili kuepuka changamoto na uzembe unaofanywa na baadhi ya wataalamu wa afya nchini.
F_XxI8oXcAAgoMS.jpeg
Dkt. Mollel ametoa agizo hilo leo Jijini Dar Es Salaam wakati akizungumza na watumishii wa afya katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke.

Dk. Mollel amesema yanapotokea matatizo katika vituo vya afya alafu Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya hawana taarifa au hawajachukua hatua hadi viongozi wa taifa wanafika watu hao wanatakiwa wajitafakari.

Amesema yanapotokea matatizo katika sekta ya afya pamoja na daktari aliyefanya uzembe watu wengine watakao kuwa watuhumiwa ni waganga wakuu wa wilaya na mikoa kwa kutoona na kutatua changamoto kabla hazijatokea.

“Tukija kwenye mkoa wako tukakuta uzembe umetokea mama mjamzito amefariki na Mganga Mkuu wa Wilaya na Mkoa ni mtuhumiwa mpaka vyombo vitakapo chunguza, tukikuta mama, mtoto au mtu yoyote amepata shida alafu mganga mkuu wa mkoa, wilaya na wewe unashangaa inabidi ujitafakari," ameeleza Dkt. Mollel.

Aidha, amewataka watoa huduma na watalaamu wa afya kutunza vizuri vifaa tiba vinavyotolewa na Serikali kwani Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya nchini.

Hata hivyo amesema kuwa Rais Dk. Samia ameshafanya kazi yake ya kuwekeza katika sekta ya afya kwa kununua vitendea kazi vingi, ikiwemo kuwekwa mashine za CT Scan ili mtanzania apate huduma bora.
 
Back
Top Bottom