Naibu Waziri TAMISEMI: Serikali inaendelea kupunguza uhaba wa walimu kwa kuajiri kila mwaka kulingana na upatikanaji wa fedha

The Watchman

JF-Expert Member
Nov 7, 2023
633
1,082
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Zainab Katimba, amesema serikali inaendelea kuchukua hatua za kukabiliana na upungufu wa walimu kwa kuajiri kila mwaka kulingana na upatikanaji wa fedha, huku kwa sasa ikiwa katika majaribio ya matumizi ya teknolojia ya madarasa janja.

Katimba ameyasema, Februari 22, 2025, alipokuwa akizungumza na maofisa elimu kata waliokuwa wakipatiwa mafunzo ya matumizi ya Madarasa Janja katika Taasisi ya Elimu Kibaha, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutembelea taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuajiri walimu kila mwaka kwa kutoa vibali vya ajira, huku ikiimarisha utaratibu wa kuwatumia walimu wa kujitolea.

Pia, Katimba amebainisha kuwa pamoja na jitihada hizo, serikali inaendelea kupandisha madaraja ya walimu kama sehemu ya motisha ya kiutendaji.

Chanzo: TBC
 
Back
Top Bottom