Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,588
- 1,190
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Daniel Sillo amesema Serikali iko mbioni kufunga mitambo ya camera za uchunguzi takribani 6500 kwa kuanzia na Majiji makuu manne ili kupunguza uhalifu na kuimarisha ulinzi na usalama kwa Wananchi.
Amesema hayo akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Kagera alipokutana na Taasisi ambazo ziko chini ya Wizara hiyo ikiwemo Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jeshi la Magereza, Idara ya Uhamiaji pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA na kufanya nao mkutano sambamba na kusikiliza changamoto zinazowakabili.
Naibu Waziri Sillo, amesema camera hizo zitasaidia kufichua wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu pamoja na kuimarisha suala la ulinzi na usalama kwa Wananchi na mali zao.
Amesema camera hizo zitafungwa katika maeneo ya mikusanyiko ya Watu wengi kama masoko, viwandani na kwenye makampuni ikiwemo kwenye Majiji makuu manne ambayo ni Arusha, Mwanza, Dodoma na Dar es salaam.
”Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kipindi cha uongozi wake tunajivunia mengi kwani ameimarisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama kwasababu Jeshi la Polisi linaenda kwenye mradi mpya unaoitwa Majiji salama utakaowezesha kufunga mitambo ya camera za kisasa 6500 kama ilivyoelezwa kwenye bajeti ya fedha ya Jeshi la Polisi 2024/25 ya kuhakikisha haya Majiji manne yako salama ikiwa ni awamu ya kwanza”