LGE2024 Naibu Waziri Pinda ajiandikisha kijijini kwake kibaoni

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
May 14, 2024
80
63
MLELE

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda ameshiriki zoezi la kujiandikisha kwenye orodha ya mpiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Mhe. Pinda amejiandikisha Jumamosi katika mtaa wa Ndemanilwa katika kata ya kibaoni halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi.

Kwa mujibu wa mwandikishaji wa kituo hicho Bw. Dikson Fabian zoezi la uandikishaji katika kituo chake limeenda vizuri na kwa mafanikio makubwa ambapo takriban watu 1,090 wamejitokeza.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye ni Mbunge wa jimbo la Kavuu katika halmashauri ya Mpimbwe Mhe. Geophrey Pinda amesema, kwa kumbukumbu za jimbo lake zinaonesha watu wengi wamejitokeza kujiandikisha.

‘’Nitoe wito kwa watu wote ambao hawajajitokeza kujiandikisha wajitikeze kwa ajili ya kushiriki kuchagua viongozi ambao ni uhitaji wao’’ alisema Mhe. Pinda
 
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda ameshiriki zoezi la kujiandikisha kwenye orodha ya mpiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.
Huyu ni mtoto wa Mzee Piga Tuu!!?
 
Back
Top Bottom