Naibu Waziri Nishati, Judith Kapinga: Vijiji vyote Newala vimefikiwa na umeme

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,826
13,584
WhatsApp Image 2024-10-29 at 13.31.41_c3b47d23.jpg
Naibu Waziri Nishati, Judith Kapinga amesema Vijiji vyote 76 vya Jimbo la ya Newala Vijijini Mkoa wa Mtwara vimefikiwa na huduma ya umeme kwa umbali wa Kilometa 1.

Kapinga ameyasema hayo leo Oktoba 29, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mhe. Maimuna Mtanda Mbunge wa Newala Vijijini aliyetaka kufahamu lini Serikali itaanza ujenzi wa nguzo za Kilomita 2 katika Vijiji ambavyo mradi wa REA mzunguko wa Pili unatekelezwa.
WhatsApp Image 2024-10-29 at 13.31.43_5e43e520.jpg
"Kwa nyongeza ya umbali wa kilomita 2, REA kupitia Mkandarasi Central Electrical International Limited anaendelea na kazi na amefanikiwa kufikisha umeme kwenye vijiji 32 kati ya vijiji 76. Vijiji vilivyosalia vinatarajiwa kukamilika hivi karibuni", Amesema Kapinga.

Akijibu swali la Mbunge wa Kilombero, Abubakar Asenga aliyeuliza lini Serikali itaunganisha umeme katika Kitongoji cha Upendo, Tupendane, Ikwambi na Misheni katika mji wa Ifakara, Kapinga amesema vijiji hivyo vipo katika mradi wa vitongoji unaoendelea.

Amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha wanachi wote wanapata nishati ya umeme na hivi sasa upo mradi wa Vitongoji 15 kwa kila jimbo na kuongeza kuwa upo mradi mwingine wa Vitongoji unaotarajiwa kuanza.

Akijibu swali la Mbunge wa Mbarali, Keneth Ndingo aliyetaka kujua lini Vitongoji vya Igula A, Igula B na Mngolongolo vitapata umeme, Kapinga amesema vijiji hivyo vimeshafanyiwa mapitio na vipo katika mradi wa kupeleka umeme kwenye vitongoji 15.

Kapinga amesisitiza kuwa uunganishaji wa umeme utafanyika katika maeneo yote ya Vijiji.
 
Back
Top Bottom